Posts

Showing posts from June, 2025

SOPHIA MWAKAGENDA ACHUKUWA FOMU YA UBUNGE WA TUKUYU

Image
Aliyekuwa Mbunge wa Chadema Sophia Mwakagenda, sasa rasmi amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM) na amechukua fomu ya kuomba kugombea jimbo la Tukuyu  

WABUNGE WATALAJIWA WA MAJIMBO YA BUSANDA, SENGEREMA NA GEITA MJINI

Image
William Mganga  Ngeleja aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Sengerema mwaka 2005 hadi 2020 ametia nia ya Ubunge jimbo la sengerema kupitia CCM ,Ngeleja amewahi kuwa waziri wa madini na nishati William Mganga Ngeleja baada ya wananchi  kufunga njia wakati akirudi kutoka kuchukua fomu wakimshinikiza asalimiane nao hatua iliyomlazimu kushuka ndani ya gari lake na kusallimiana nao kwa madai nidhamu na uwajibikaji bado wanaukumbuka Wakili Malogoi achukua fomu tena jimbo la Geita mjini Mhandisi Robert Gabriel achukua fomu kumtoa Kanyasu Geita Mjini  Mhandisi Gabriel Luhumbi Robert mkuu,wa mkoa mstaafu ametia nia nae ubunge jimbo la Geita mjini kupitia chama  cha mapinduzi. Dkt. Busanda atia nia ya kugombea jimbo la Busanda nafasi ya ubunge Mh. Costantine Kanyasu aomba tena ridhaa jimbo la Geita Mjini  Wakili Malogoi achukua fomu tena jimbo la Geita mjini

DKT. BITEKO AOMBA RIDHAA YA KUTETEA JIMBO LA BUKOMBE

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea Ubunge katika Jimbo la Bukombe. Dkt. Biteko amechukua fomu hiyo na kuirejesha kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe, Ndugu. Leonard Yesaya Mwakalukwa mapema leo Juni 29, 2025. Zoezi la uchukuaji fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) linaendelea nchi nzima ambapo watia nia tofauti wameendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchukua fomu za Ubunge na Udiwani.  

RAIS MWINYI AIKABIDHI YANGA SH MILIONI 100 AYAONA MAKOMBE 5 ILIYOBEBA

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Yanga Afrika ilitowa Ubingwa wa Kombe la NBC Premer League 2024-2025, wakati wa kukabidhiwa Makombe mbalimbali ya Ubingwa ya Timu hiyo iliyoyanyakuwa katika msimu huu, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 30-6-2025.(Picha na Ikulu)  

JIMBO LA DODOMA MJINI LAPATA MGOMBEA WA KIKE KIJANA-----FATUMA YUSUFU

Image
 Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Sophia Kibaba (kushoto), akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge FatumaYusufu, ambaye anagombea jimbo la Dodoma mjini. amechukua fomu hiyo baada ya kuvutiwa na kauri ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoisema wakati akifunga bunge hivi karibuni akiwataka vijana wajitokeze na wapewe kipaumbele . Alisema Akifanikiwa kuchaguliwa atawatumikia Wanadodoma mjini kwa moyo mmoja na kuwa nao bega kwa bega. Fatuma Yusufu, akionyesha fomu yake kwa wanahabari baada ya kukabidhiwa  

MBUNGE WA BAHI ANAYEMALIZA MUDA WAKE KENNETH NOLLO ACHUKUWA FOMU YA UBUNGE

Image
Mbunge  Jimbo la Bahi,   Kenneth Ernest Nollo, akijaza kumbukumbu zake katika daftari la wageni lililopo katika Ofisi za Chama cha Mapunduzi Wilaya ya Bahi baada ya kuwasili na mkewake kwa ajili ya kuchukuwa fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo hilo katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu. huu ni mchakato wa mwanzo kwenye chama chao cha CCM, akizungumza baad2a ya kuchukua fomu alisema yeye bado anahamu ya kuwatumikia wanabahi chama chao kinawapa uhuru mwanachama yeyote aliyetimiza vigezo anaweza kuomba kura kwa wananachi Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Paulina Deus Bupamba (kulia), akimkabidhi fomu za kuomba kugombea ubunge wa jimbo hilo Mbunge wa sasa wa jimbo hilo Kenneth Nollo, makabidhiano hayo yalifanyika mchana leo huku akiwa ameambatana na mkewe (kushoto).  Hadi leo saa 7 mchana wagombea 7  walikuwa wamechukuwa fomu za ubunge.  

DODOMA KUMEKUCHA FOMU ZA UBUNGE NA UDIWANI ZAANZA KUTOLEWA KAMA NJUGU.

Image
 Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Sophia Kibaba (kushoto), akimkabidhi Fomu ya kugombea ubunge Wakili Erick Kidyalla, Makabidhiano hayo yalifanyika leo asubuhi WAKILI Eric Kidyalla ni moja ya makada waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania kugombea ya Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jimbo la Dodoma Mjini. Alisema sababu iliyomsukuma kuchukua fomu hiyo ni kwa kuwa yeye ni kada wa Chama hicho hivyo aliona ni vyema kutumia haki yake ya kikatiba ili akifanikiwa aweze kutoa mchango wake katika kulitumikia Chama na wanaDodoma mjini akishirikiana na watendaji wengine. Pia ampongeza Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Jimbo la Dodoma mjini liweza kugawanyika jambo ambalo limetoka fulsa kubwa kwa wanaCCM wengi kujitokeza kugombea. "Jimbo la Dodoma mjini kijiografia lilikuwa kubwa hivyo kuridhiwa ligawanywe,  Rais, Samia amefanya jambo jema na itatoanfulsa kubwa kwa wananchi,"alisema Kidyalla Joyce Kingerenge, akizungumza na wanahabari baada ya kutoka ku...