Posts

Showing posts from August, 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Mifugo Tixon Nzunda, akutana na wafugaji Dodoma

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Mifugo Bw. Tixon Nzunda (kushoto), akaizungumza na Dkt. Moses Ole Sure, mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishugulisha na Chakula FAO, baada ya kufungua warsha ya wadau ya kupitia na kuthibitisha, rasimu ya Sera ya Taifa ya mifugo ya Mwaka 2022 . Warsha hiyi ya siku moja imefanyika jijini Dodoma na wakuhudhuliwa na wadau ,kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara Mfugaji Shamba Kubwa Longido akizungumza na waandishi wa habari katika kipindi cha mapumziko cha warsha hiyo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo, Venance Ntiyalundura, akizungumza na Waandishi wa habari akielezea warsha hiyo na kuwataka wafugaji waondokane na ufugaji wa kizamani usiokuwa na tija sasa wawe na mifugo michache yenye kutoa mazao mengi na kumletea faida kubwa mfugaji Katibu Mkuu, akaipiga picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo kutoka sekta mbalimbali Dkt. Moses Ole Sure, mwakilishi wa Shirika la Umoja

RAIS SAMIA AMUAPISHA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA MZEE RAMADHANI NYAMKA PAMOJA NA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza (SACP) Mzee Ramadhani Nyamka Cheo kipya cha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) kabla ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Jeshi hilo katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka kuwa Mkuu wa Jeshi hilo katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Majaji wa Mahakama Kuu kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. Majaji wa Mahakama Kuu pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka wakila kiapo cha Maadili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tar

RAIS DKT. MWINYI AMTEMBELEA MWANASIASA NA MFANYABIASHARA MAARUFU ZA,NZIBAR MOHAMMED RAZA

Image
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakizungumza na Mwanasiasa na Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar  Mhe. Mohammed Raza Daramsi, walipofika nyumbani kwake Kibweni Wilaya ya Magharibi “A” Unguja kumtembelea na kumjulia hali yake leo 28-8-2022 na (kushoto kwa Rais) mtoto wake Hassan Mohammed Raza.(Picha na Ikulu)  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mwanasiasa na mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar Mhe. Mohammed Raza Daramsi alipofika nyumbani kwake Kibweni Wilaya ya Magharibi “A” Unguja kumtembelea na kumjulia hali yake leo 28-8-2022.(Picha na Ikulu) 

RAIS SAMIA KUFUNGUA KIKAO KAZI CHA POLISI MJINI MOSHI

    NA.Abel Paul wa Jeshi la Polisi Jeshi la Polisi Tanzania lingependa kuwajulisha kuwa katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) iliyopo Moshi mkoa wa Kilimanjaro maarufu (CCP) kutafanyika kikao kazi cha Maafisa Wakuu waandamizi wa Makao Makuu, Makamanda wa Polisi Mikoa na Vikosi, kitakacho fanyika siku tatu Moshi Kilimanjaro. Akitoa taarifa hiyo msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP DAVID MISIME amesema Kikao kazi hicho kitaanza tarehe 30 Agosti hadi tarehe 01 Sepetemba 2022. Ambapo Kikao kazi hicho kitafunguliwa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 30 Agosti 2022. Aidha SACP MISIME amesema kuwa Jeshi la Polisi kila mwaka hufanya kikao kama hicho kwa ajili ya kufanya tathimini ya utendaji wake kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuona wapi Jeshi hilo limefanya vizuri na wapi halijafanya vizuri na sababu zake na kuweka mikakati mipya ya kutek

TFS WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO NA MSHIKAMANO SEHEMU ZA KAZI.

Image
  Mhifadhi Mkuu shamba la Wino  Glory Kasmir kushoto akiwa  na aliyekuwa mfanyakazi wa shamba hilo Theofrida Luoga wakati wa sherehe ya  kumuaga iliyofanyika jana  katika ukumbi wa Chandamali Resort unaomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania Brigedi ya 401 Songea. Kaimu Afisa utumishi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania kanda ya kusini Anderson Besisila akizungumza katika sherehe ya kumuaga aliyekuwa mfanyakazi wa shamba la miti Wino wilayani Songea Theofrida Luoga,kulia meneja wa TFS wilayani Songea Issa Mlela. Mhifadhi Mkuu shamba la miti Wino linalomilikiwa  na wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS) Glory Kasmir kushoto akimlisha keki ya upendo aliyekuwa mfanyakazi wa Shamba la miti Wino Theofrida Luoga ambaye amestaafu utumishi wa umma. WAFANYAKAZI wa wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS),wameaswa kufanyakazi kwa upendo,mshikamano na kutanguliza uzalendo kwa nchi yao ili kuongeza ufanisi  na huduma bora sehemu zao za kazi. Wito huo umetolewa

WAZIRI BALOZI DKT. CHANA AONGOZA KIKAO KAZI CHA WAKUU WA VYUO VYA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Image
  *********************** Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Agosti 27, 2022 ameendesha Kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kupokea taarifa za uendeshaji wa vyuo hivyo. Akizungumza na Wakuu wa Vyuo hivyo Waziri Balozi Dkt.Pindi Chana amesema Wizara anayoiongoza imedhamiria kuweka mfumo wa usimamizi wa vyuo hivyo pamoja na kuendelea kufanya maboresho ya miundombinu na mazingira ya kufundishia ili viendelee kutoa elimu bora kwa Watanzania “Ni dhahiri mabadiliko haya yatahitaji kuendana na utoaji wa elimu ya Uhifadhi na Utalii ili kuzalisha wataalam wenye uwezo wa kusimamia vyema sekta Sekta ya Wanyamapori, Misitu na Nyuki ambazo zimekua na mchango mkubwa katika uchumi wa nchi” . Alisisitiza Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Licha ya kuwapongeza viongozi wa vyuo hivyo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutoa elimu kwa Watanzania, Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameeleza kuwa juhudi zaidi zinah

RAIS , MWINYI AKABIDHIWA RIPOTO YA HESABU ZA SERIKALI IKULU

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2020/2021 na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Dkt.Othman Abass Ali, hafla hiyo iliyofanyika leo 27-8-2022, katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Mhe.Haroun Ali Suleiman. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2020/2021 na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Dkt.Othman Abass Ali, hafla hiyo iliyofanyika leo 27-8-2022, katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa m