Posts

Showing posts from September, 2023

UCSAF KUENDELEZA JITIHADA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO VIJIJINI. MASHIBA

Image
  MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa Huduma ya Mawasiliano Vijijini unaendelea ambapo Mfuko huo umesaini mkataba wa kupeleka huduma za Mawasiliano katika kata zaidi ya 1900 na mradi huo umefikia asilimia 90 katika utekelezaji wake. Ameyasema hayo wakati akielezea utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya UCSAF na kazi ambayo wameifanya ya kuboresha mawasiliano pamoja na kupeleka vifaa vya TEHAMA katika kijiji cha Msomera Mkoani Tanga. Ambapo amesema kuwa jukumu walilokasimiwa na serikali la kuhakikisha wanapeleka mawasiliano vijijini wanalitekeleleza vyema ambapo mpaka sasa kazi kubwa imefanyika ya ujenzi wa minara vijijini na lengo likiwa ni kuhakikisha vijiji vyote vinapata huduma ya mawasiliano ili kuchochea maendeleo kupitia uchumi wa kidijitali. Tutakapokamilisha ujenzi wa miradi hiyo ya mawasiliano wananchi wapatao milioni 15 watapata huduma za mawasiliano na hii ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo

WANANCHI WA KISIWA CHA RUKUBA WAFURAHIA KUANZA KUPOKEA VIFAA TIBA VYA KITUO CHAO CHA AFYA

Image
Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijni Profesa, Sospeter Muhongo, wamempongeza wananchi wa jim bo hilo kwa juhudi zake za kuwaletea maendeleo   Kisiwa cha Rukuba kimekamilisha ujenzi wa Kituo chake cha Afya na tayari kimeanza kupokea vifaa tiba vya Kituo hicho. Utoaji wa Huduma za Afya ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini unaendelea kuboreshwa na kuimarika. Kwa sasa tuna: (i) Hospitali ya Halmashauri Hii ina hadhi ya Hospitali ya Wilaya (ii) Vituo vya Afya sita (6) Murangi, Mugango, Bugwema, Makojo, Kiriba na  Kisiwa cha Rukuba (iii) Zahanati 42 *24 za Serikali *4 za Binafsi *14 zinajengwa Maombi yaliyopelekwa Serikalini *Wafanyakazi wa kutoa Huduma mbalimbali za Afya wapo wachache sana. Idadi iongezeke sana. Tunaomba idadi iongezeke hasa kwenye Hospitali yetu mpya na kwenye Vituo vyote vya Afya. *Vifaa tiba vinahitajika, ni pungufu sana. *Wingi wa dawa za aina mbalimbali uongezeke sana. Furaha & Shukrani Tafadhali sikiliza  CLIP/VIDEO ya kutoka Kisiwani Rukuba iliyoambatanishwa hapa Ofisi

NAPE NNAUYE: NCHI ITAENDELEA KUWA MUUMINI WA UHURU WA HABARI MTANDAONI

Image
SHARE Waziri wa habari mawasilino na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akiUngumza katika mkutano wa Jukwaa la Uhuru wa mtandaoni Barani Afrika jijini Dar ea Salaam. @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ Waziri wa habari mawasilino na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye amesema nchi itaendelea kuwa waumini wa uhuru wa mtandaoni huku akitoa rai kuwa uhuru huo unapaswa utumike kulinda tamaduni za nchi. Hayo ameyasema leo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la uhuru wa mitandao barani Afrika linalofanyika jijini Dar es salaam. Amesema pamoja na nchi kutoa uhuru wananchi wanapaswa kulinda tamaduni kwa kutumia mitandao hiyo katika shughuli za kuwaingizia kipato na si kutumia katika mambo ambayo yanaweza kuvunja amani ya nchi na kuchafua utu wa mtu. “Tumeweka katika sera zetu uhuru wa mitandao lakini sasa hivi Dunia imekua tumieni mitandao hiyo kufanya shughuli za kiuchumi na si kupiga umbea ambao haukusaidii chochote”amesema Nape. Amesema pamoja na kuwa na uhuru mtandaoni n

NAIBU WAZIRI KIKWETE ASISITIZA UTUMISHI WA UMMA NI POPOTE, AWAASA WAZAZI

Image
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mkoani Pwani, ikiwa ni ziara yake ya  kikazi mkoani humo ya kuzungumza na kusikiliza changamoto  zinazowakabili watumishi hao Sehemu ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza na leo wilayani  hapo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Maiko Mganga  akizungumza mbele Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete changamoto zinazokikabali Kitengo hicho katika kutimiza majukumu yake wakati  kikao na watmishi wa Halmashauri hiyo. Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Ramadhan Possi  akizungumza na Watumishi wa Halmashauri hiyo kabala

CWT GOGOLO LAKE KUMBE KUZUIA KUPIGWA BILIONI 16. RAMANI YA JENGO MILIONI 415 MAWAZIRI WATANO WAHUSISHWA

Image
Rais wa Chama cha Walimu Nchini (CWT), Komredi Leah Ulaya, akifungua kikao cha Kamati kuu ya chama hicho cha Dharula kilichofanyikia Makao Makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Japhet Maganga na Kulia ni Makamu Rais wa Chama hicho Suleimani Ikombe @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@   CWT GOGOLO LAKE KUMBE KUZUIA KUPIGWA BILIONI 16. RAMANI YA JENGO MILIONI 415 MAWAZIRI WATANO WAHUSISHWA Hatimaye imebainika kwamba Songombingo inayoendelea  katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Makao Makuu ni uzuiaji wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya chama hicho  ulioidhinishwa na uongozi uliopita. Ujenzi wa jengo hilo ulikuwa ufanyike jijini Dodoma, wajumbe wa  baraza Kuu la Chama hicho waliingizwa chaka baada ya kutakiwa kuidhinisha ujenzi huo bila kuambiwa utagalimu kiasi gani. bila kufahamu kiasi gani kitatumika katika ujenzi wa jengo hilo Viongozi wao walitumia mwanya huo na  kuingia mkataba wa ujenzi wa jengo  la golofa tatu ambalo lingetumia kiasi cha sh Bilio

KIKAO CHA DHARULA CHA CHAMA CHA WALIMU CWT CHAFANYIKA JIJINI DODOMA.

Image
Rais wa Chama cha Walimu Nchini (CWT), Komredi Leah Ulaya, akifungua kikao cha Kamati kuu ya chama hicho cha Dharula kilichofanyikia Makao Makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Japheth Maganga na Kulia ni Makamu Rais wa Chama hicho Suleimani Ikombe.. Kikao hicho pamoja na mambo mengine wameridhia maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho tangu kianzishwe  Novemba 1.1993 kitafanyika mkoani Mwanza ambapo walimu zaidi ya Elfu 60 wanatarajiwa kuhudhuria. Katibu Mkuu wa Chama hicho Komredi Japheth Maganga, akitoa maelezo kwa wajumb e wa kikao Wajumbe wa kikao hicho wakiwa kikaoni Meza kuu wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kikao  

SAKATA LA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WALIMU (CWT) LAFIKIA PATAMU

Image
Tangazo lililoleta kasheshe likiualifu umma kama mhalifu mwalimu huyu. Baadhi ya walimu mkoa wa Dodoma ambao ni wanachama wa Chama cha Walimu nchini (CWT), wamemwijia juu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kwa kitendo chake cha kusambaza kwenye mtandao nyaraka ya Serikali inayomhusu katibu Mkuu wa Chama chao, Japheth Maganga cha kukataliwa kuongezwa muda  wa kukitumikia chama hicho. Walimu hao Juma Ali, Hassan Bakari na Joseph Lupia wakizungumza na mwandishi wa gazeti hili mtandao  walidai wakati Maganga akiazimwa na chama hicho hakuna tangazo kama hilo lililotolewa lakini jambo la kushangangaza imekuwaje sasa nyaraka hiyo iliyotakiwa kuwa ya siri kwakua ni mali ya serikali isambazwe kwenye mitandao. Kufuatia kitendo hicho wao kwa mitazamo yao wanadai kwamba Katibu Mkuu huyo anapigwa vita na waliowahi kuwa viongozi wa Chama hicho waliotimuli kwa ulaji wa fedha aidha wamemuona anawazibia ulaji huo sasa wanahangaika huku na kule ili kumwondosha. Wakizungumza na mwandishi wetu wa gazeti mta

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Image
Naibu waziri wa fedha, Hamad Hassan Chande,.amewataka waumini kuendelea kuiombe amani nchi ya Tanzania ikiwemo kukemea kukiuka kwa madili ya kiafrika na kufuatwa kwa maadili ya nchi za maghalibi hasa katika kipindi hiki cha dunia kupolomoka kimaadili Ameyasema hayo katika ufunguzi wa IJITIMAI Kimataifa inayofanyika katika msikiti wa Gadaff jijini Dodoma.  Amesema amani ya nchi ni muhimu waumini na mashekh waisaidie Serikali kuombea amani kwani tupo katika  nyakati za  machafuko katika baadhi ya nchi tunazopakana nazo sisi Tanzania hatupo katika kisiwa. "Amani yetu tuilienda hata ikibidi kwa ncha ya upanga Aidha amewaoba wafanyabiashara kulipa kodi kwani  hiyo itainua Taifa, mnunuzi adai risti na muuzaji atoe risti, hakuna nchi iliyoendelea Duniani bila kulipa kodi " waumini wenzangu tukiyazingatia hayo yote niliyosema nchi yetu itakuwa imepiga hatua kubwa, hakuna haja ya kuwindana kama wanyama msituni nani hajatoa risti tumkamate", alisema Naibu waziri Chande. SHEIKH WA