Posts

Showing posts from July, 2023

FUNDISHENI VIJANA WAKITOKA HAPA WAKAJIAJILI SERIKALINI AJIRA HAKUNA....DKT .MPANGO

Image
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji, wakifunua kitambaa kuashiria  ufungizi wa Kampasi na Majemgo ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya uliofanyika leo  Akizungumza huku akimtazama Kaimu  Mkuu wa Chuo hicho Profesa, Edda Lwoga  alimwambia wakati umefika sasa wa kwenda na Teknolojia haipaswi kukosa vitabu chochote cha kujisomea au kufundiashia katika chuo hiki kikubwa katika ukanda huu wa Afrika mashariki, vitabu vipo kwenye mitandao nendeni na wakati. "miaka ya nyuma kulikuwa na changamoto za kukosa vitabu  kwa sababu hakukuwa na mitandao hata ile ya jamii", alisema Mpango. Naye Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Eda Lwoga, alisema  Chuo cha Elimu ya Biashara ni Chuo cha Serikali  kipo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara Kilianzishwa rasmi tarehe 21 Januari, 1965 kikiwa na Kampasi moja tu ya Da, Iringa na Lindi.r es Salaam, Kutokana na uhitaji wa elimu ya biashara na ujasiliamali Tanzania Chuo kilifungua kampa

CCM MKOA WA TANGA IPO IMARA====== MWENYEKITI RAJAB

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman akipandisha bendera ya CCM kuashiria ufunguzi wa Shina la Wakereketwa  wa CCM Vatican City Kata ya Msambweni Jijini Tanga wakati wa ziara yake juzi,Picha na mpiga picha wetu  

HAKUNA UHABA WA DAMU SALAMA UNAOITESA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA -BOMBO

Image
Na Mwandishi Wetu, TANGA. UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo umesema hakuna uhaba wa damu kama ilivyoandikwa na mmoja ya gazeti kwamba unaitesa kutokana na uwepo wa jitihada mbalimbali Jitihada hizo ni pamoja na kutumia taasisi mbalimbali za kiserikali na kidini kuhamasishaji wa kuchangia kwa hiari jambo ambalo limekuwa likifanyika kwa nyakati tofauti tofauti na limekuwa na mwamko mzuri wa wananchi kuchangia Pia katika taarifa hiyo iliyotoka kwenye chombo hicho cha habari ilionekana kuwa na mapungufu kwa kukosa mikakati iliyoelezewa wakati wa halfa hiyo. Akizungumza leo na waandishi wa Habari Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo-Dkt Naima Yusuf alisema kwamba uhaba upo lakini hospitali imeweka mchakato wa upatikanaji wa damu kwa wakati kupitia uchangishaji katika halfa mbalimbali.  Alisema sio kwamba uhaba wa damu unaitesa hapana bali kuna mpango ambao upo kwa upatikanaji wa damu kwa mwaka na bado wanasisitiza wananchi kujitokeza kuja kuchangia

DUWASA KUMALIZA MGAO WA MAJI JIJI LA DODOMA---------MHANDISI ARON

Image
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Rodney Thadeus, akizungumza kabla ya kumkalibisha Mkurugenzi wa Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma Mhandisi Aron Joseph (kulia) kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari leo. Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imesema muda wa wananchi wa jiji hilo kupata huduma ya maji utaongezeka kutoka saa 13 hadi 19 mwishoni mwa mwaka 2024. Hayo ameyasema leo Julai 28.2023 jijini Dodoma  na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2023/2024.  Amesema kuwa hatua  hiyo itakuja baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa miradi ya muda mfupi ya uchimbaji wa visima pembezoni mwa mji. “Water Service coverage ni asilimia 91, na muda wa utoaji huduma za maji ni saa 13 kwa siku , lengo ni kufikia coverage ya asilimia 93 ifikapo

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI INAHITAJI WAFANYAKAZI 170O---- MNDOLWA

Image
Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji nchini  Raymond Mndolwa, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dododma leo., akielezea utekelezaji wa  Majukumu ya Tume hiyo na  Mwelekeo wa Ujenzi wa Miradi ya Umwagiliaji mwaka wa Fedha 2023 na 24 M KURUGENZI MKUU WA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI, RAYMOND MNDOLWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA TUME YA UMWAGILIAJI NA MWELEKEO WAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24 KATIKA UKUMBI WA IDARA YA HABARI - MAELEZO JIJINI DODOMA* #Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanzishwa kwa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji Sura 435 kama Idara ya Serikali inayojitegemea chini ya Wizara inayohusika na Umwagiliaji. # Majukumu makuu ya Tume ni kuratibu, kuendeleza na kusimamia Maendeleo ya kilimo cha Umwagiliaji nchini. #Mafanikio ya Tume kwa mwaka wa fedha 2022/23. Hadi kufikia Juni 2023, Tume imesaini mikataba 48 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 234.1 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa skimu n