Posts

Showing posts from October, 2017

UHAMIAJI WAFANYA USAFI NA KUTOA ZAWADI KWA WATOTO HOSPITALI YA TEMEKE

Image
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt Anna Peter Makalala ametoa zawadi kwa akina mama na watoto waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Temeke sambamba na kufanya usafi wa mazingira kuzunguka eneo hilo. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jhn Pombe Magufuli la kufanya usafi kila mwisho wa mwezi. Kamishna Jenerali Anna alimkabidhi kijarida chenye masuala mbalimbali yanayohusu uhamiaji kwa mganga mkuu wa hospitali ya Temeke na kumtaka kushirikiana nao kwenye kutoa elimu kwa wagonjwa wanaofika hapo pale pindi wapatapo muda. Mganga Mkuu wa hospitali ya Temeke Dr Amani Malima  amewashukuru sana kwa kuja kufanya usafi kwenye hospitali hiyo na kutoa zawadi kwa wakina mama na watoto huku akiwahakikishia kuwa watatoa elimu kwa wagonjwa wanaofika hapo kuhusiana na masuala ya uhamiaji. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter M