Posts

Showing posts from April, 2017

TLS KULINDA UTAWALA WA SHERIA, KUMSHTAKI MAKONDA TAARIFA KWA UMMA

Image
 Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika  (TLS), Tundu Lissu, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuhusu maazimio yaliyofikiwa na Baraza la Uongozi la chma hicho na hatua  za kuchukus dhidi ys Serikali. Kushoto ni Makamu wa Chama hicho Godwin Ngwilimi na Kulia ni Wakili na Mwenyeji wao Stephine Kuwayawaya.  Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) limemaliza kikao chake cha kawaida cha siku mbili kilichofanyika Dodoma kwa kuazimia kuchukua hatua kadhaa zenye lengo la kulinda Utawala wa Sheria na uwajibikaji katika nchi yetu.  Akitangaza maazimio ya Baraza hilo, Rais wa TLS na Mwenyekiti wa kikao hicho, Mh. Tundu A.M. Lissu, alizitaja hatua zitakazochukuliwa kuwa ni pamoja na TLS kufungua mashtaka binafsi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda aka Daudi Albert Bashite, kwa tuhuma za makosa mbali mbali ya jinai ikiwamo kutumia vyeti feki, ujambazi wa kutumia silaha, matumizi mabaya ya madaraka, n.k.   Mh. Lissu alisema:

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI KWA WATUMISHI WA UMMA LEO MJINI DODOMA

Image
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti    kwa Watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe katika vitabu hivyo vya taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti    kwa watumishi wa umma alivyopokea kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma. Katikati ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na wakwanza kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Idris Kikula.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa kitabu cha Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti    kwa watumishi wa umma alivyopokea kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Um