Posts

Showing posts from November, 2023

NAIBU WAZIRI KAPINGA AWASHA MIRADI YA UMEME YA 20-BILIONI MOROGORO KUSINI

Image
Na.Issa Sabuni na Zuwena Msuya, Morogoro Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amewasha umeme kwa mara ya kwanza katika vijiji viwili vya jimbo la Morogoro Kusini na kuwahamasisha wananchi kusuka umeme (Wiring) kwenye nyumba zao ili kuutumia katika kuleta maendeleo. Naibu Waziri amesema hayo leo, Novemba 30, 2023 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya umeme vijini na kuwasha Umeme Tayari (UMETA) katika Kata ya Mvuha wilaya ya Morogoro Vijijini. Naibu Waziri Kapinga amewahamasisha wananchi hao kuunganisha umeme kwani serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika miradi lengo likiwa ni kuwainua kiuchumi. Amewapongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kutekeleza miradi ya umeme vijijini na kuwaahidi wananchi kuwa serikali itahakikisha kuwa vijiji vyote vinafikiwa ifikapo Juni 30, 2024. Aidha amewashauri Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme nchini, TANESCO kuja na mpango mkakati utakaowawezesha wananchi wengi kusuka waya kwenye nyumba (wirin

FEDHA ZA NDANI ZIWE TEGEMEO KATIKA MAPAMBANO YA UKIMWI – DKT. BITEKO

Image
SHARE *Asema Serikali inaendelea na juhudi za kutokomeza UKIMWI Nchini Morogoro Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wadau mbalimbali wanaohusika na mapambano dhidi ya UKIMWI nchini kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kuhakikisha kuwa wanatenga fedha za kutosha kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI nchini badala ya kutegemea wafadhili kwa kiasi kikubwa. Dkt. Biteko amesema hayo wakati wa Mkutano Maalum wa Wadau wanaoshughulikia Udhibiti wa UKIMWI Tanzania uliofanyika tarehe 30 Novemba, 2023 mjini Morogoro na kuhusisha viongozi wa Serikali, Wadau wa Maendeleo na Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI. “Tanzania imepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya UKIMWI na nawataka TACAIDS na wadau kuhakikisha mnashirikiana kwa pamoja dhidi ya mapambano ya Ukimwi kwa kuongeza ushiriki wa wananchi pia” Amesisitiza Dkt. Biteko Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Tanzania, kupitia Serikali ya Awamu ya Sita, imeend

CHONGOLO AJIUZULU UKATIBU MKUU WA CCM----- MWENYEKITI DKT. SAMIA ARIDHIA

Image
  Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, na ameridhia ombi hilo.  Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.  Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hicho nchini na kimefanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan aongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ikulu Jijini Dar es salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 29 Novemba, 2023 Ikulu Jijini Dar es salaam, Awali kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 29 Novemba, 2023 Ikulu Jijini Dar es salaam, Awali kikao hicho kilitanguliwa na  kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 29 Novemba, 2023 Ikulu Jijini Dar es salaam, Awali kikao hicho kilitanguliwa na  kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.  

MASAUNI AKUTANA NA MABALOZI WA NCHI TATU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Nabil Hajlaoui(kushoto) muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu Ushirikiano juu ya Masuala ya Ulinzi na Usalama kati ya wizara na nchi hiyo.Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kenya hapa nchini, Isaac Njenga(kushoto) muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu Ushirikiano juu ya Masuala ya Ulinzi na Usalama kati ya wizara na nchi hiyo.Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Qatar hapa nchini,Fahad Rashid Al-Marekhi(kushoto) muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu Ushirikiano juu ya Masuala ya Ulinzi na Usalama kati ya wizara na nchi hiyo.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan asalimiana na Wananchi ndani ya Meli ya MV Kilimanjaro 8 alipokuwa akisafiri kutoka Zanzibar kwenda Dar es salaam

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wafanyakazi wa Meli ya MV Kilimanjaro 8 kabla ya kuingia ndani ya Meli hiyo alipokuwa akisafiri kutokea Visiwani Zanzibar akielekea Jijini Dar es salaam  tarehe 28 Novemba, 2023.  

KINANA USO KWA USO NA MAKONDA

Image
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Katibu wa NEC Siasa, Uenezi, Itikadi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda mara baada ya kufunga Mafunzo ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Wajumbe Wamefundishwa Mada Tofauti zinazohusu Uongozi na Maadili ili kuongeza Uwezo na Ufanisi kwa Viongozi hao kuwajibika kwa Chama na Wananchi Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Katibu wa NEC Siasa, Uenezi, Itikadi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda na mara baada ya kufunga Mafunzo ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Wajumbe Wamefundishwa Mada Tofauti zinazohusu Uongozi na Maadili ili kuongeza Uwezo na Ufanisi kwa Viongozi hao kuwajibika kwa Chama na Wananchi

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAIBUKA NA USHINDI KATIKA MBIO ZA NYIKA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Image
  Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, U kimwi  na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais ,  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Mwanaamani Mtoo  akimpongeza mtumishi wa ofisi hiyo Bw. Kokolo Lusanda aliyepata ushindi wa pili katika mbio za Km. 5 wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, 2023 yanayoendelea mkoani Morogoro. Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakishiriki mbio za nyika zinazofanyika mkoani Morogoro.   Wa kwanza kulia ni  Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, U kimwi  na Magonjwa Yasiyoambukiza ,  Bi. Mwanaamani Mtoo . Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifurahia jambo mara baada ya kuhitimisha mbio za nyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani, 2023 yanayoendelea mkoani Morogoro. Na. Veronica Mwafisi-Morogoro Watumishi wawili wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utaw

MAJALIWA ATAKA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUTENGA FEDHA KWA SEKTA YA ARDHI

Image
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau kujadili Utekelezaji Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi tarehe 28 Novemba 2023 jijini Dodoma . Na Munir Shemweta, WANMM        Serikali imewataka wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya sekta ya ardhi katika kipindi hiki cha maandalizi ya bajeti ya mwaka 2024/2025 kwa yale maeneo yasiyotengewa fedha za mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi nchini. Hayo yamebainishwa tarehe 28 Novemba 2023 na Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa wakati wa Mkutano wa Kitaifa wa Wadau Kujadili Utekelezaji Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi uliofanyika jijini Dodoma. Kupitia hotuba yake hiyo, Mhe. Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini zinazotekeleza mradi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa timu

KINANA AFUNGUA MAFUNZO YA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM YA TAIFA JIJINI DAR

Image
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Abdulrahman Kinana amefungua Mafunzo (Semina) ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, ambapo Wajumbe Watafundishwa Mada Tofauti zinazohusu Uongozi na Maadili ili kuongeza Uwezo na Ufanisi kwa Viongozi kuwajibika kwa Chama na Serikali, Mafunzo yanafanyika Dar Es Salaam tarehe 28 Novemba 2023. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Wakifuatilia Mafunzo  (Semina) ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, ambapo Wajumbe Watafundishwa Mada Tofauti zinazohusu Uongozi na Maadili ili kuongeza Uwezo na Ufanisi kwa Viongozi kuwajibika kwa Chama na Serikali, Mafunzo yanafanyika Dar Es Salaam tarehe 28 Novemba 2023. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Komred Abdulrahman Kinana Akifungua Mafunzo ya   (Semina) ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, ambapo Wajumbe Watafundishwa Mada Tofauti zinazohusu Uongozi na Maadili ili kuongeza Uwezo na Ufanisi kwa Viongozi kuwajibika kwa Chama na Serikali, Mafunzo yana

WAZIRI DKT. JAFO ATUNUKU VYETI WAHITIMU WA CHUO CHA AFYA CHA CITY COLLEGE JIJINI DAR

Image
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala amewatunuku vyeti wahitimu wa ngazi ya Diploma ya Ufamasia na Utabibu Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwatunuku vyeti wahitimu wa Diploma ya Ufamasia na Utabibu alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam.  Wahitimu wa Diploma ya Ufamasia na Utabibu wakiwa katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala Novemba 25, 2023 jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akinutunukiwa Tuzo na Chuo cha Afya cha City College Kampasi ya Ilala ya kutambua mchango wake katika elimu, wakati wa mahafali ya