Hii ni blog ya Wananchi, itakayokuwa na jukumu la kukupasha habari, kukufundisha na kukuelimisha pia.

Friday, September 22, 2017

WAFANYAKAZI WASHAURIWA KUPIMA AFYA MARA BAADA YA KUSTAAFU.


Na: Lilian Lundo – MAELEZO Dodoma.

Wafanyakazi nchini wameshauriwa kupima afya zao mara tu wanapostaafu ili kujihakikishia ikiwa hawajaathirika na kazi ambazo wamekuwa wakizifanya.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Eric Shitindi alipokuwa akifungua semina ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi juu ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, leo Mjini Dodoma.

“Kumekuwa na mazoea kwa wafanyakazi kupima Afya pale tu wanapoajiriwa na kutotilia maanani upimaji afya zao mara wanapostaafu ili kujua ikiwa kazi wanazozifanya zimewaathiri kwa kiasi gani,” amesema Shitindi.

Ameendelea kwa kusema kuwa, upimaji wa afya mara baada ya kustaafu utasaidia watumishi kujua afya zao na ikiwa watakuwa wameathirika upitia kazi walizokuwa wakizifanya basi mwajiri atawajibika mkulipa fidia mtumishi huyo.

Aidha amesema kuwa licha ya juhudi za Serikali katika kusimamia Usalama na Afya maeneo mengi ya kazi sio ya kuridhisha kutokana na waajiri wengi kutokuzingatia sheria na kanuni mbalimbaliza Usalama na Afya.

Hivyo basi kutokana na waajiri hao kutofuata sheria na kanuni hizo kumesababisha maeneo mengi ya kazi kulalamikiwa kutokana na ukiukwaji wa sheria hizo.

Vile vile amesema kuwa baadhi ya waajiri na wafanyakazi wana uelewa mdogo  kuhusu kuzingatia maelekezo ya Usalama na Afya Mahali pa kazi ikiwemo matumizi sahihi ya vifaa kinga.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda amesema kuwa, wameamua kuandaa semina hiyo kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi hapa nchini ili na wao wakatoe elimu hiyo kwa wafanyakazi wote nchini kutokana na wafanyakazi hao kutokuwa na uelewa mzuri juu ya masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda akiongea na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi Leo Mjini Dodoma.Kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi akiongea na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi ambapo aliwashauri wafanyakazi nchini kupima afya mara wanapostaafu ili kujihakikishia kama hawajaathirika na kazi walizokuwa wanafanya.Katikati ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule na Kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda 
 Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule akiongea naViongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi, kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi na kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Bi. Khadija Mwenda
 Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw.Qambos Sule (KUSHOTO) na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Jones Majura(KULIA) wakiteta jambo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi baada ya ufunguzi wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi leo Mjini Dodoma
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Semina kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi Leo Mjini Dodoma. PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO,DODOMA

HOSPITALI YA TEULE MUHEZA YAPATIWA MSAADA WA MASHUKA

Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Boniface Mhabe kushoto akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kwa Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Sub Agro Trading anda Engineering,Neema Ng'unda kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza jana ilkiwa ni kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika kilimo wa pili kutoka kushoto ni  
Afisa  Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli 

HOSPITALI ya Teule wilayani Muheza Mkoani Tanga imepata msaada wa mashuka 50 kwa ajili ya kukabiliana na uhaba uliopo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wanao kwenda kupata matibabu kutoka maeneo mbalimbali hasa vijijini.

Hatua ya uhaba huo unatokana na uchakavu wa wa mashuka unaotokana na
  kufubaa unaosababishwa na maji wanayotumia kufulia kutokana na uhaba wa maji hali iliyopelekea kuwepo uhitaji kila wakati ili kuweza kukithi mahitaji ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.

Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,
  Boniphace Mhabe wakati akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kampuni ya Suba Agro Trading na Engineering ambao ni mzalishaji wa mbegu bora zamahindi kwa kushirikiana na Cimmity taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mahindi na Ngano.

Shuka hilo zilitolewa kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito
  kwenye hosptali ya Teule Muheza,Hospitali ya wilaya ya korogwe na ile ya wilaya ya Handeni lengo kubwa likiwa kuwaondolea changamoto zinazowakabili.

"Vitanda vipo vingi lakini tatizo kubwa ni mashuka na hili linatokana
  na asilimia kub wa kuchakaa kutokana na maji lakini pia wakati mwengine yanabadilika rangi jambo ambalo limekuwa changamoto kwao.

Aidha alisema wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia
  msaada huo ambao umefika wakati muafaka kwa kusadia baadhi ya vikwazo wanazokutana navyo wakati wa utoaji wa huduma  za afya.

Awali akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Afisa Masoko na
  Mauzo wa Kampuni hiyo,Neema Ng'unda alisema alisema wamekuwawakishiriki katika kuhamasisha kilimo Tanzania hususani kwa wakina mama ambao ndio nguzo kubwa hapa nchini kufikia mafanikio.

Alisema wamelenga wanawake kwa sababu ndio muhimili muhimu kwenye
  jamii wa kuwawezesha wakina baba kwenye kulima kilimo bora ambapo kinaweza kuwainua kiuchumi.

"Lakini pia tunawashukuru wakulima wote Tanzania kwa kutumia mbegu zao
  kwa kulima kilimo cha kisasa ambacho kinaweza kuwa mkombozi kijiinuakimaendeleo na kukuza mitaji yao "Alisema.

Naye kwa upande wake,Afisa Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao
 makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli alisema zoezi hili limelenga kurudisha fadhila kwa wakina mama wa Tanzania maana ndio wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kilimo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

RAIS ABBAS: AIDHA UHURU AU HAKI KAMILI KWA WOTE, KATIKA NCHI YA PALESTINA YA KIHISTORIA

Rais wa Palestina “Mahmoud Abbas” amesisitiza kuwa uhuru  wa nchi yake upo karibu hauepukiki na kwamba uvamizi wa Israeli unafikia mwisho, akisema: "Aidha upatikane uhuru au haki kamili ya wote katika nchi ya Palestina ya kihistoria."

Rais Abbas Jumatano jioni akihutubia Mkutano wa 72 wa Umoja wa Mataifa, ameongeza kusema kwamba, imepita miaka ishirini na minne tangu kusainiwa kwa Mikataba ya mpito ya Oslo, ambayo ilionesha ukomo wa uvamizi wa Israeli na kuwapa matumaini Wapalestina, ya kuanzishwa kwa Dola yao huru, huku akihoji " Tuko wapi sasa na matumaini haya?."

Amesema:"Tumekubali uwepo wa Dola ya Israeli  kupitia mipaka ya mwaka 1967, lakini Israeli kutokubali uwepo wa Dola ya Palestina kunatupa maswali mengi. Badala ya kuzingatia sababu, inafanya juhudi kuteka misimamo ya kimataifa kwa masuala yasiyo na uzito wowote, yatokanayo na sera zake za kikoloni. Tunapoitaka na kutakiwa na jumuiya ya kimataifa kukomesha uvamizi wake, inadai ni uchochezi na kukosekana  ushiriki wa Palestina na kuwekwa kwa masharti yasiyowezekana."

Rais Abbas ameongeza kusema kuwa,anaelea machafuko ni Utawala wa kivamizi wa Israeli katika ardhi yetu,uvamizi ambao umefikia zaidi ya nusu karne,huku zaidi ya miaka kumi sasa tumekubaliana  kuunda kamati ya pande tatu ambazo ni Marekani,Israeli na Palestina, ili kumaliza suala la uchochezi.Kamati  imefanya kazi kwa muda, lakini tumekuwa tunatoa wito wa kufufuliwa wa kamati hiyo hatupati mrejesho. Hivi ni nani anaekaribisha hilo na kufanya juhudi ya kulifanya liwepo?.

Amesema pia,kuendelea kwa uvamizi ni aibu kwa Israeli na Jumuiya ya Kimataifa,ni wajibu wa Umoja wa Mataifa kumaliza uvamizi huo ili kuwezesha jamii ya Palestina kuishi kwa uhuru na ustawi katika ardhi yake,huku mji mkuu wake ukiwa ni Jerusalemu ya Mashariki.

"Kukomesha uvamizi na vitendo vyake vya kidhalimu, vitakuwa na athari kubwa mno katika kupambana na udaidi pia mashirika yake kukosa karatasi muhimu ambazo huzitumia kwa kuuza fikra zao."Tunatilia mkazo la kukaliza uvamizi ili kukamilisha juhudi zetu katika kukabiliana na mashirika hayo ya kigaidi,kwani Wapalestina wapo dhidi ya ugaidi wa ndani,kikanda na wa kimataifa.

"Tuliwasilisha mpango wa amani wa Kiarabu  unaoitaka Israeli kuondoka katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu tangu  mwaka 1967 lakini Israeli haikujibu,kama ilivyoufanyia ule mpango ujulikanao kama “Road Map” uliowasilishwa na pande nne na kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,hali inayoonekana kana kwamba Israeli ipo juu ya sheria. Vilevile ukaja mpango wa amani wa Ufaransa ukifuatiwa na mkutano husika mjini Paris,lakini juhudi zote hizi zilikataliwa na kupigwa na Israeli."

Ameongeza kusema:”Tulimuomba Waziri Mkuu wa Israeli akubali ufumbuzi wa dola mbili, kisha tukae kuzungumzia suala la mipaka akakataa,licha ya jitihada zetu kufikia amani ya kweli, lakini Israeli inaendelea kuvuruga na kuendeleza ujenzi wa makazi ya walowezi Ukingo wa Magharibi na kila mahali, hatimae hakuna tena nafasi kwa ajili ya taifa la Palestina.

"Vitendo viovu vya Israeli katika mji mtakatifu, vitachochea hisia za uadui wa kidini, ambao unaweza kugeuka mgogoro mkubwa wa kidini, tumeiomba serikali ya Israeli kuheshimu sheria na historia ya sehemu hizo takatifu lakini Israel tangu ilipoikalia kimabavu Jerusalemu mwaka 1976, imekuwa ikiihodhi kwa azimio la upande mmoja.

Rais Abbas amesema kuwa, “Jerusalemu imekaliwa kimabavu na hatua zote za Israeli ni batili kama ilivyo katika ujenzi wake wa makazi ya walowezi Jerusalemu ya Mashariki na maeneo mengine ya Palestina. Ieleweke wazi kuwa,ubadilishaji wa historia ya Jerusalemu na kuuchafua Msikiti wa Aqswa ni kuchezea hatari,pia ni kushambulia majukumu ya Palestina na yale ya Jordan.Tunaitahadharisha hilo, isijaribu kusababisha vita vya kidini wakati mgogoro wetu ni wa kisiasa”.

"Chaguo letu kama Waarabu na chaguo la dunia ni sheria za kimataifa, uhalali wa kimataifa na uwepo wa dola huru ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya 1967.Tutatoa ushirikiano wote katika kufanikisha hilo la kihistoria,ili tupate kuishi kwa amani pamoja na Israeli. Lakini kama ufumbuzi wa dola mbili utaharibiwa na kuimarisha dola moja yenye serikali mbili,hapatakuwa na linguine kwetu wala kwenu ila mapambano na kutaka kupata haki zetu kamili ndani ya Palestina ya kihistoria. Hivi si vitisho ila ni kutaka haki zetu kama wapalestina”.

Tatizo letu kwa utawala wa kivamizi wa Israeli sio Uyahudi kama dini, kwani hiyo ni dini ya Mungu kama Uislamu na Ukristo.Tumebeba majukumu yetu katika Ukanda wa Gaza,ambayo haiwezekani kuwepo Palestina bila hiyo,ninafarijika leo kuona kufikiwa kwa makubaliano mjini Cairo kufuatia juhudi nzuri za Misri.Yamekomesha vitendo vya Hamas vilivyoleta mgawanyiko na hatimae kufanyika kwa uchaguzi mkuu,hatimae serikali yetu mwisho wa wiki ijayo itakwenda Ukanda wa Gaza ili kufanya kazi huko.

"Ukimya wa jumuiya ya kimataifa juu ya vitendo dhalimu vya Israeli,ndio uliohamasisha vitendo hivyo tangu awali hadi inakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake, uko wapi Umoja huo na maazimio yake?Vipi unatendea mataifa kwa viwango tofauti? Basi huu ni wajibu wa Umoja wa Mataifa." Aidha ameuomba kumaliza uvamizi wa Israeli ndani ya muda maalumu,kwani haiwezi tena kutoa data huru kuhusu mpango wa amani wa kiarabu,hasa kuhusiana na faili wakimbizi kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa 194,huku akiashiria kuwa maazimio ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kupuuzwa na Israeli”.

Rais Abbas amesisitiza haja ya kusitisha shughuli za ujenzi wa makazi ya walowezi katika maeneo ya Palestina,kwani hatuna uwezo wa kulinda raia zetu chini ya utawala wa mabavu,Umoja wa Mataifa uitake Israeli kutambua mipaka Palestina ya mwaka 1967 na kupunguza mpaka na kuomba wajumbe wote wa Umoja wa Mataifa kutangaza kwamba kutambuliwa kwao kwa msingi wa mipaka ya 1967,pia wanachama wote wa Umoja huo kutambua mipaka hiyo ili kutilia mkazo maazimio ya sheria za kimataifa.

Amesema:"Iko wapi mipaka ya Israeli mlioitambua wakati Israeli yenyewe haijaikubali,sheria za kimataifa zinaitaka dunia kuweka hiyo mipaka". Aidha Rais ametoa wito kwa nchi zote duniani kutoshiriki katika ujenzi wa makazi ya kikoloni ulio kinyume na sheria,huku zikichukua hatua stahiki dhidi yake kama ilivyofanya jumuiya ya kimataifa dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Afrika ya kusini na tunataka kutangaza habari mbaya za mashirika ambayo yanafanya kinyume cha sheria na makazi."

Hivyo, amezihimiza nchi wanachama kuitambua dola ya Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967,huku akitilia mkazo kuwa hatua hiyo haitoathiri mpango wa amani,hasa hasa ikiwa Wapalestina wanaitambua dola ya Israeli. Tunauhimiza Umoja wa Mataifa kuikubali Palestina kama mwanachama wake kamili,huku tukiiomba jumuiya ya kimataifa kuendelea kuisaidia kiuchumi na kifedha ili iweze kujitegemea na kujiamini.  

Aidha Rais Abbas, ametahadharisha juhudi za kutaka kubadilisha majukumu ya shirika la misaada  UNRWA na kanuni zake,pia kufuta kipengele cha saba katika Baraza la haki za binaadamu au kuzuia kutoa orodha chafu ya mashirika yanayofanya kazi katika makazi ya walowezi wa Israeli nchini Palestina inayokaliwa kimabavu. 

Rais Abbas amehitimisha hotuba yake kwa kutilia mkazo msimamo wa nchi yake,katika kuheshimu haki za binaadamu na kutekeleza mikataba ya Umoja wa Mataifa na ile yote iliyosaini,kwani Palestina ni sehemu ya jumuiya ya kimataifa na si vingine. Huku nchi yake pia itaandaa matakwa hayo kwa maazimio yatayokwenda sambamba na misingi husika,kisha kuyawasilisha kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

TIMU YA NDANTO FC YATWAA KOMBE LA MICHUANO YA 'TULIA CUP 2017'

 Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Davis Mwamunyange, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Ndanto Fc, Peter Mwakingwa, baada ya kushika nafasi ya nafasi ya kwanza na kutwaa kombe la fainali za 'Tulia Cup 2017' kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO MEDIA GROUP)
 Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Davis Mwamunyange, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Isange, Frank Asilih, baada ya kushika nafasi ya pili katika fainali za 'Tulia Cup'kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya.
 Beki wa timu ya Isange Fc, Zawadi Andombwisye (kushoto) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Ndanto Fc, Erick Mwangoye, wakati wa mchezo wa Fainali za 'Tulia Cup' uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5.
 Beki wa timu ya Ndanto Fc,Fidelis Yeo (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Isange Fc, Hussein Thom, wakati wa mchezo wa Fainali za 'Tulia Cup' uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5.
  Wachezaji wa Isange Fc, Shadrack Kandrum (kushoto) na Hussein Thom (kulia) wakimdhibiti Mandela Chaile, wakati wa mchezo wa Fainali za 'Tulia Cup' uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5. 
 Beki wa timu ya Isange Fc, Shadrack Kandrum (kulia) akimdhibiti mshambuliaji wa Ndanto Fc, Julius Mtawala, wakati wa mchezo wa Fainali za 'Tulia Cup' uliochezwa jana Sept 21, 2017 kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Katika mchezo huo Ndanto walishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo kwa mwaka huu 2017 na kitita cha sh. milioni 1.5.
 Luteni General, James Mwakibolwa, akiongozana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tulia Ackson, kukagua timu ya Ndanto fc kabla ya mchezo wa fainali dhidi ya Isande Fc, katika mchezo wa fainali wa 'Tulia Cup' kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya.
 Luteni General, James Mwakibolwa, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Netiboli ya Kimo,Salome Sanyondo, baada ya kushika nafasi ya pili katika fainali za 'Tulia Cup'kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya. 
Luteni General, James Mwakibolwa, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Netiboli ya Wizara ya Mambo ya Ndani, baada ya kushika nafasi ya kwanza katika fainali za 'Tulia Cup'kwenye uwanja wa Tandale Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya. 

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA BODI YA PILI YA UONGOZI INSTITUTE

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema kuwa wakurugenzi walioteuliwa katika bodi ya Taasisi ya Uongozi  ni watu makini na wenye uzoefu wa muda mrefu katika nafasi mbalimbali hivyo watatoa ushauri mzuri kwenye taasisi hiyo.

Waziri Angellah aliyasema hayo katika uzinduzi wa bodi ya pili ya Taasisi  ya Uongozi uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini  Dar es Salaam. Amesema bodi ya wakurugenzi wa taasisi hiyo wamepita katika utumishi na wazalendo katika sehemu zao mbalimbali ambapo watakuwa msaada mkubwa kwa taasisi hiyo katika  kutoa ushauri.

Amesema kuwa Uongozi Institute ilianzishwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi wa Afrika katika kuangalia maendeleo endelevu ya bara la Afrika  hivyo wajumbe wa bodi ni wa kimataifa na wanatambulika.

Angellah amesema kuwa walioteuliwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli watatimiza majukumu yao na wataendelea kupewa ushirikiano pamoja na viongozi wengine wa Afrika katika kuwa na ajenda ya kuandaa viongozi.

Amesema uongozi Institute inatakiwa kutimiza mambo matatu moja ni bidhaa ya huduma iliyo na kiwango bora, kuangalia rasilimali  ya kuweza  kufanya taasisi hiyo ikue katika kuangalia vyanzo vya mapato pamoja na kujengea uwezo wa kuendelea kutekeleza ajenda ambazo zimeibuliwa.

Walioteuliwa katika bodi hiyo Mwenyekiti ni Balozi wa Finland Inchini Afrika Kusini, Kari Alanko , Makamu wa Rais Profesa Idris Kikula wengine ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora  Dk. Laureane Ndumbaro,  Katibu Mtendaji wa SADC Dk. Stergomena Tax, Profesa Penina Mlama wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Christina Duarte Waziri wa Zamani wa Fedha , Mipango na Utumishi wa Cape Verde, Mkurugenzi wa Nodic Afrika ya nchini Sweeden Lina Soiri, pamoja Mkurugenzi wa zamani wa shule ya utawala ya nchini Uingereza , David Walker.

Nae Afisa Afisa Mtendaji Mkuu wa Uongozi Institute, Profesa Joseph Semboja  amesema kuwa chombo hicho kilianzishwa katika kuwajengea viongozi wa Afrika ambao waliridhia kuundwa kwa chombo hicho.

Amesema kuwa Taasisi hiyo imetoa mafunzo mbalimbali tangu kuanzishwa kwake na itaendelea kutoa mafunzo kwa watumishi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki akizungumza katika uzinduzi wa bodi ya pili ya Wakurugenzi wa Uongozi Institute , uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Uongozi Insitute, Profesa Joseph Semboja akizungumza katika uzinduzi wa bodi ya Uongozi Institute  juu ya taasisi hiyo inavyofanya kazi  katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Uongozi Institute ,Balozi wa Finland Inchini Afrika Kusini, Kari Alanko akitoa shukurani kwa Waziri Kairuki  mara baada ya kuzinduliwa  bodi hiyo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki akigawa vitabu vya miongozo kwa wajumbe wa Bodi hiyo.
 Sehemu watendaji mbalimbali wa serikali waliohudhuria uzinduzi wa bodi ya pili ya oungozi institute.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na bodi ya ya wakurugenzi ya Uongozi Institute, jijini Dar es Salaam.

HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI ILIOANDALIWA NA KINANA KWA AJILI YA KIONGOZI WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM MJINI DODOMA JANA SEPTEMBER 21,2017
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Adamu Kimbisa akimtolea ufafanuzi wa zawadi ya kinyango Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam uku katibu Mkuu wa (CCM) akishuhudia zoezi hilo,wakati wa hafla ya Chakula cha Jion ilioandaliwa na kinana.
 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza kabla ya Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam kukabidhiwa zawadi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Adamu Kimbisa wakati wa hafla ya Chakula cha Jion.
 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza na balozi wa Vietnam Nguyen kim Doanh.


 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akifurahia jambo na wageni wake toka chama cha Kikomunisti cha Vietnam (VCP) jana wakati wa hafla ya chakula cha jion.
 Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Comred Abdurahman Kinana akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jion.
 Wajumbe wa Chama cha kikomunisti cha Vietnam (VCP) pamoja na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazaza CCM wa (pili toka kushoto) wakifuatilia mazungumzo ya Katibu mkuu wa CCM  katika hafla ya chakula cha jion.
Baadhi Wajumbe wa Sekretariet wakifuatilia mazungumzo ya Katibu mkuu wa CCM  katika hafla ya chakula cha jion.
 Katibu Mkuu wa CCM Comred Abdurahman Kinana na Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam wakinyanyua glasi kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri kabla ya chakula cha jion alicho mwandalia Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam Mjini dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaj Juma Kimbisa pamoja na Katibu wa idara ya SUKI kanal mstaaf Ngemela Rubiga wakinyanyua glasi kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri kabla ya chakula cha jion  Katibu mkuu wa CCM alicho mwandalia Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam Mjini dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar DKT.Abdallah Mabodi akiagana na Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam mara baada ya kumalizika hafla ya chakula cha Usiku ilioandaliwa na Katibu mkuu wa CCM Comred Abdulrahman kinana Mjini dodoma.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Comred Abdulrahman Kinana akiagana na Mgeni wake Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha vietnam (VCP) Comred Chau Van Lam mara baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula cha jion aliomwandalia mgeni wake   Mjini dodoma. (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)