Posts

Showing posts from January, 2023

Rais Mhe. Samia azindua Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai nchini, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kabla ya kuzindua Tume ya kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai tarehe 31 Januari, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Naibu Spika Mhe. Mussa Azan Zungu, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini Mhe. Eng. Hamadi Masauni, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Zena Said pamoja na Wajumbe wa Tume ya kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 31 Januari, 2023.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jin

TAARIFA YA MWAKA YA SHUGHULI ZA KAMATI KWA KIPINDI CHA JANUARI, 2022 HADI JANUARI, 2023

Image
1  SEHEMU YA KWANZA 1.0 UTANGULIZI 1.1 Maelezo ya Jumla Mheshimiwa Spika, Kwa niaba ya Kamati ya Kudumu ya Bunge 2 1.2 Muundo wa Taarifa Mheshimiwa Spika, kanuni ya 142 ya kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020, imeweka masharti kuhusu Muundo wa Taarifa ya Kamati. Kwa kuzingatia masharti hayo, naomba kutambulisha muundo wa Taarifa kwa kutaja sehemu kuu kama ifuatavyo: - (i) Sehemu ya kwanza ni utangulizi inaotoa maelezo ya jumla, ikiwemo msingi wa shughuli za Kamati, njia na mbinu zilizotumika pamoja na orodha ya shughuli zilizotekelezwa; (ii) Sehemu ya pili inafafanua shughuli zilizotekelezwa na uchambuzi kwa yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji. Aidha, sehemu hii inabainisha mafanikio na changamoto zilizojitokeza; (iii) Sehemu ya tatu inatoa maoni ya jumla na mapendekezo ili kuliwezesha Bunge kuamua; na (iv) Sehemu ya nne inahitimisha na kutoa hoja kwa hatua ya Bunge lako tukufu kujadili na kufanya uamuzi. 1.3 Msingi wa Shughuli zilizotekelezwa na Kamati Mheshimiwa Spika, Msi

CHONGOLO ASEMEA MIGOGORO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA

Image
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mzee Maduruki Nangeleke (kulia) mara baada ya kumaliza mkutano na wanachama wa Tawi la Kibaoni uliofanyika kwenye uwanja wa Kololo. Katibu Mkuu ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji (Gavu) kwenye ziara ya mkoa wa Morogoro yenye lengo kukagua, kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 sambamba na kukagua uhai wa Chama. - Advertisement - Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Mvomero Ndugu Jonas Van Zeeland wakati wa mkutano wa Shina namba 18, Mikoroshini kata ya Dakawa mkoani Morogoro.

RAIS SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TAASISI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la  Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation  (EGPAF) linaloshughulikia kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, Chip Lyons Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Januari, 2023.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) linaloshughulikia kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, Chip Lyons pamoja na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Januari, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) Chip Lyons pamoja na ujumbe wa

WABUNGE NA WAFANYAKAZI WA BUNGE WAONYESHANA UBABE KATIKA BUNGE BONAZA

Image
Waziri Mkuu akiwa Sambamba na Spika Dkt. Tulia Ackson, wakifanya  mazoezi mepesi baada ya kuongoza matembezi ya kilomita 2.5 yaliyojulikana kwa jina la  Bunge Bonanza  yaliyoambatana na michezo mbalimbali na washindi kupatiwa vikombe na medali Wafanykazi wa bunge nao wakifanya mazoezi Wabunge nao wakichapa zoezi Wakishindana kwa kukimbia Wakishindana kwa kucheza karata Naibu Spika Zungu wakichuana mchezo wa bao na William Lukuvi Waziri Mkuu akikagua timu kwa ajili ya Bonanza Timu ya Wagunge Timu ya Wafanyakazi wa Bunge Wachezaji wa Mpira wa kikapu wakichuana Mbunge Mtatulu, akihamasisha timu yake iwaburute  wafanyakazi, walibeba kombe baada ya kiwashinda Mfanyakazi wa Bunge Kizingiti, akishangaa baada ya Timu yake kushindwa Wabunge wanawake wakichuana na wafanyakazi wa Bunge wanawake kwa mchezo wa kuvuta kamba Siyo wacheza sumo  wa Kijapani ni wabunge wakiwa tayari kuvuta kamba Mfanyakazi Kizingiti, akiihamasisha timu yake ishinde hata hivyo ilishindwa kwa awamu  ya pili  baada ya kwan