Posts

Showing posts from January, 2024

VITABU VINAVYOELEZEA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Image
 VITABU VINAVYOELEZEA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI ILANI 2020-2025 Vitabu viwili vimechapishwa na vinasambazwa. Uchapishaji wa vitabu vingine unaendelea hadi 2025. Unaweza ukavisoma kupitia TOVUTI ya Jimbo letu: www.musomavijijini.or.tz ILANI 2015-2020 Vitabu viwili vilichapishwa na kusambazwa. Unaweza kuvisoma kupitia TOVUTI ya Jimbo letu: www.musomavijijini.or.tz Ofisi ya Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini www.musomavijijini.or.tz Tarehe: Jumatatu, 29.1.2024

CHAMA CHA WALIMU TANZANIA-CWT IDARA YA WALIMU WENYE ULEMAVU. CHAMPONGEZA SPIKA DKT. TULIA

Image
Spika Dkt. Tulia Ackson, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania Mwalimu Japhet Maganga, baada ya kuwasili katika ukumbi wa Pius Msekwa kwa ajili ya hafla ya kupongezwa leo jijini Dodoma. Katibu Mkuu Maganga, akimkalibisha Spika Dkt. Tulia kuzungumza na wajumbe wake Kulia ni Ulumbi Shani Mwenyekiti wa Idara ya walimu wenye ulemavu CWT Makao Makuu, Spika Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na viongozi hao Spika Dkt. Tulia akipiga picha na wageni wake pamoja na ujumbe wao pamoja na Wenyeviti wa kamati za Kudumu za bunge waliohudhulia hafla hiyo Spika, akiagana na wageni wake baada ya kumalizika hafla hiyo  RISALA  YA KUKUPONGEZA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA RAIS WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI MH DK TULIA AKSON MWANSASU.                                                                                                               Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

SPIKA DKT.TULIA AKSON AWATAMBULISHA VIONGOZI WA YANGA NA SIMBA BUNGENI LEO

Image
Rais wa Yanga Eng. Hersi Said, akitambulishwa bungeni na Spika leo. Rais huyo alikuwa ameelikwa katika Bonanza la Timu za yanga na Simba za Wabunge na Stafu wa bunge hilo na Yanga kuibuka kidedea Bonanza hilo lilifanyika Jumamos katika uwanja wa Jamhuri Msemaji wa Yanga Alli Kamwe akitambulishwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Imani Kajula, akitambulishwa bungeni Msemaji wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally,akitambulishwa bungeni. Mbunge wa Knondoni Abbas Tarimba akizungumza na viongozi hao.  

WAZIRI MKUU ITALIA AKISALIMIANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE TANZANIA JANUARY MAKAMBA

Image
Waziri Mkuu wa Italia, Mhe. Giorgia Meloni akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) katika ukumbi wa mkutano jijini Roma, Italia. Waziri Makamba yupo Roma kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia ulioanza tarehe 28 – 29 Januari 2024.

NHC, SEKTA BINAFSI KUJENGA MIRADI 21 YA NYUMBA YENYE THAMANI YA BILIONI 271

Image
Shirika la Nyumba la Taifa NHC kwakushirikiana na Sekta binafsi watajenga miradi ya majengo ya biashara na makazi katika eneo la Kariakoo lililopo Jijini Dar es Salaam yenye thamani ya bilioni 271. Hayo yameelezwa leo Jumatatu Januari 29, 2024 na Mkurugenzina Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ahmad Abdalla wakati akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miradi hiyo kwa ubia na sekta binafsi iliyofanyika Upanga makao makuu ya Shirika hilo. Amesema miradi hiyo itakuwa na tija kubwa kwenye Shirika la Nyumba kutokana na kuongeza wigo wa wafanyabiashara katika nyanja mbalimbali. “Katika eneo la Kariakoo ambapo tunavunja nyumba 16 kwaajili ya kujenga miradi hiyo awali kulikuwa na wapangaji 190 ambapo maduka yalikuwa 118,vyumba vya makazi 72 hivyo tunategemea baadaya ujenzi kukamilika tutakuwa na wapangaji 2011, wapangaji wa maduka watakuwa 1258, vyumba vya makazi 253 na vyumba vya kuhifadhia mizigo 500”, Amesema Abdalla Ameeleza kuwa Se

MAWAZIRI WA NISHATI TANZANIA, ZAMBIA WAJADILI UJENZI WA BOMBA JIPYA LA MAFUTA

Image
  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Masuala ya Nishati wa Zambia, Mhe. Peter Kapala wakati wa kikao kilicholenga kujadili nia ya Serikali ya Tanzania na Zambia kuanza ujenzi wa bomba la inchi 24 la kusafirisha mafuta safi kutoka Tanzania kwenda Zambia leo Januari 29, jjini Dodoma. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Waziri wa Masuala ya Nishati wa Zambia, Mhe. Peter kapala wakati wa kikao kilicholenga kujadili nia ya Serikali ya Tanzania na Zambia kuanza ujenzi wa bomba la inchi 24 la kusafirisha mafuta safi kutoka Tanzania kwenda Zambia leo Januari 29, jijini Dodoma. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (Wa Tatu kushoto) akizungumza na Waziri wa Masuala ya Nishati wa Zambia, Mhe.Peter Kapala na ujumbe wake (kulia) wakati wa kikao kilicholenga kujadili nia ya Serikali ya Tanzania na Zambia kuanza ujenzi wa bomba la i

WIKI YA SHERIA JIJINI DODOMA NJONI BRELA MPATE ELIMU YA UANZISHAJI WA MAKAMPUNI

Image
Afisa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni mkoa wa Dodoma Winifrida Gaundence John akiwafafanulia jaambo wanahabari kuhusu shughuli zinazofanywa na wakala hao, mazungumzo hayo yalifanyika leo katika viwanja vya Nyerere Square   kwenye maonyesho ya wiki ya Sheria inayoendelea. Afisa huyo amewaomba wananchi wa mkoa huo kufika katika banda lao kupata ufafanuzi wa uanzishaji wa makampuni  na upataji wa leseni bila konakona. Winifrida akimhudumia mteja aliyefika katika banda la wakala hao Naibu Msajili wa Mmahakama nchini Hawa Mgaluka, akiwafafanulia jambo wajumbe wa Tume ya uchaguzi nchini waliotembelea banda la Mahakama kuu lililopo katika maonyesho ya Wiki ya Shdria nchini katika viwanja vya Nyerere Square Mjumbe wa Tume hiyo Balozi Ramadhani Mapuli, akiuliza ufafanuzi kwa Naibu msajili Mratibu wa Chama cha Majaji na Mahakimu mkoani Dodoma Jamila Mkabarah akiwafafanulia jambo wajumbe wa tume  hiyo baada ya kufika katika banda hilo  

CHUO CHA TEHAMA KUJENGWA DODOMA CHENYE UWEZO WA KUCHUKUA ZAIDI YA WANAFUNZI 15000

Image
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla akiagana na  Washauri Elekezi wa Chuo Kikuu cha Hanyang Consoltium cha Korea Kusini baada kumalizika kwa  kikao  cha ufunguzi wa kuanza ujenzi wa Chuo Mahiri cha TEHAMA Nala Dodoma, pamoja na kutangaza nafasi za ufadhili wa mafunzo ya TEHAMA kwa watumishi Umma Januari 29,2024.. Katibu Mkuu, Mohammed Khamis Abdulla  akiwa katika picha ya pamoja na washauri elekezi wa Chuo Kikuu cha Hanyang Consoltium cha Korea Kusini   pamoja na maafisa wengine wa serikali. Baadhi ya wakuu wa vyuo vikuu vya Tanzania wakijitambulisha. Baadhi ya maafisa wa serikali wakiwa katika mkutano huo Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Izabela Katondo akiongoza mkutano wa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mohammed Khamis Abdulla  na wanahabari katika Mji wa Kiserikali Mtumba Dar es Salaam.  Katibu Mkuu wa wizara hiyo,  Mohammed Khamis Abdulla