Posts

Showing posts from May, 2017

LEO BUNGENI DODOMA

Image
Wabunge ambao ni mashabiki wa timu ya yanga, wakipiga picha na wachezaji wa yanga pamoja na kombe baada ya kutambulishwa bungeni  leo   Wachezaji wa Timu ya Mbao kutoka Mwanza wakipiga picha na baadhi ya wabunge   baada ya kulitembelea leo Mbunge wa Newala George Mkuchika akizungumza na Meneja wa Shirika la Taifa la Nyumba wa Huduma za Jamii, Muungano Saguya wakati wa kipindi cha mapumziko cha wabunge, Kulia ni Afisa Habari wa Shirika hilo Yahya Chalahani   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba, akizungumza na wachezaji wa mbao baada ya kupiga nao picha jana katika viwanja vya bunge Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye ni Mbunge wa Hai Freeman Mbowe na Mbunmge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe wakiwa wameshika kombe lililotwaliw na Yanga moja kwa moja   baada ya kulitwa mara tatu mfululizo. 

BUNGENI LEO DODOMA

Image
Msemaji wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni   Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Cecilia Paresso, akisoma hotuba mbadala ya wizara hiyo kwa mwaka 2017 na 2018 bungeni mjini Dodoma  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk.Charles Tizeba akisoma hotuba ya wizara hiyo ya makadirio ya mapato na Matumizi ya fedha   kwa mwaka 2017 na 2018, Bungeni Dododma  SERIKALI imetakiwa kuongeza nguvu ili kukabiliana na uvuvi haramu nchini kwa kuwatumia askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). Kauli hiyo imetolewa bungeni jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Dk Mary Nagu, alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara   ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/17 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18. “Pamoja na wizara kupitia idara ya maendeleo ya uvuvi kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu ambavyo bado vinaendelea