BUNGENI LEO DODOMA


Msemaji wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni  Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Cecilia Paresso, akisoma hotuba mbadala ya wizara hiyo kwa mwaka 2017 na 2018 bungeni mjini Dodoma 


Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk.Charles Tizeba akisoma hotuba ya wizara hiyo ya makadirio ya mapato na Matumizi ya fedha  kwa mwaka 2017 na 2018, Bungeni Dododma 
SERIKALI imetakiwa kuongeza nguvu ili kukabiliana na uvuvi haramu nchini kwa kuwatumia askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Kauli hiyo imetolewa bungeni jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Dk Mary Nagu, alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara  ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/17 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18.

“Pamoja na wizara kupitia idara ya maendeleo ya uvuvi kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu ambavyo bado vinaendelea kushamiri mahali pengi nchini, bado vitendo hivyo vinaendelea kutokea.

“Kwa hiyo, kamati inashauri Serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya doria kwenye maeneo ya maziwa ikiwa ni pamoja na kushirikisha Jeshi la Wananchi katika kufanya doria ili kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu,” alisema Dk. Nagu.

Katika hatua nyingine, alisema kuna haja Serikali kuwa na kanda maalum ya kilimo cha umwagiliaji ili kND hiyo iweze kusaidia katika kuinua kilimo nchini.

Naye mseaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika wizara hiyo, Secilia Pareso, alisema kuna haja Serikali kuangalia sheria zake ili nyavu zinazotumika kuvulia samaki katika Ziwa 

Tanganyika, zitofautiane na zinazotumika katika Ziwa Viktoria kwa kuwa baadhi ya samaki wanatofautiana ukubwa hasa hasa dagaa.
 Pamoja na hayo, alitaka kujua Serikali itachukua hatua gani za kuwafidia wafugaji ambao mifugo yao ilikufa kutokana na ukame katika mwaka 2016/17.
Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.