Posts

Showing posts from May, 2024

POKEA ZAWADI TOKA JWTZ

Image
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman amemkabidhi zawadi Rais wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) Kanali Nilton Gomes Rolim wakati wa hafla ya kuhitimisha Mkutano Mkuu wa Baraza hilo uliofanyika Jijini Dar Es Salaam. Mnadhimu Mkuu amemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda kuhitimisha hafla ya kufunga Mkutano huo wa 79 wa Baraza hilo tarehe 19 Mei 2024 ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati ya JWTZ na Majeshi mengine Duniani.

WAZIRI GWAJIMA ALIOMBA BUNGE SH . BILLIONI 67.9 BAJETI YA WIZARA YAKE 2024/2025 HATA HIVYO YAPITA KWA MBINDE

Image
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum,  Dkt Dorothy Onesphoro Gwajima.  (MD/MPH).. akisoma hotuba ya bajeti ya wizara yake bungeni akiomba kuidhinishiwa  Sh, Bilioni 67.9 kwa mwaka wa bajeti ya 2024 na 2025. bajeti hiyo iliyosomwa kwa siku moja hata hivyo ilikumbana na wachangiaji matata waliopinga utendaji kazi wa wizara hiyo . Wabunge wengi waliochangia walihoji iweje kitabu chake alichokiandaa kwa wabunge na hotuba yake yote isitaje kukemea janga linalolisakama dunia la kutaka kuladhimishwa kuwa na ushonga. Hawa ni baadhi ya wabunge waliomtoa jasho waziri Gwajima Kabura Shitobelo, watoto wa kiume wanahalibiwa, wengi wakiwa shule za bording au na nyumbani kwa kupokea wageni wasiokuwa na maadili kulala chumba kimoja, wazazi wawajibike kuwa karibu na watoto wao. Sophia Mwakagenda Sophia Mwakagenda, tukatae watoto kutumiwa kuombaomba mitaani , tufikilie ni adhabu gani ili iwafae watu hawa katili wanaowafanyia hivyo watoto wetu, tusimamie maadili ya wat

UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2020-2025 NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI:

 Mbunge wa Jimbo apewa Tuzo ya Heshima atunukiwa tuzo ya heshima kwa utendaji kazi wake uliotukuka jimboni kwake Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Mara imempa Tuzo ya Heshima Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa kutambua mchango wake mkubwa sana kwenye utekelezaji wa miradi iliyoainishwa ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Mkoa wa Mara, Ndugu Julius Masubo Kambarage ndiye aliyeikabidhi Tuzo hiyo. CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa ina taarifa zaidi, tafadhali isikilize. Ofisi ya Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini www.musomavijijini.or.tz P. O. Box 6 Musoma Tarehe: Jumatano, 15.5.2024

WAZIRI NAPE ALIOMBA BUNGE LIMUIDHINISHIE SH BILIONI, 180

Image
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara yake  kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025  bungeni Dodoma leo.Wizara hiyo imeidhinishiwa zaidi ya sh. bil. 180.  na bunge baada ya kusomwa kwa siku moja na kupita bila kupingwa huku ikishuhudiwa na wadau wa Tasinia hiyo wakiwemo waliowahi kuwa watanzangazaji maarufu  mika aya 70. Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Bunge na Uratibu Jenista Mhagama, akizungumza na waandishi wa habari bungeni leo huku akitaja mkoa unaoongoza kwa dawa za kulevya kuwa ni Dar es Salaam Waziri akizindua taarifa ya hari ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2023 Kulia ni Aletasi Lyimo Kamisna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti dawa za kulevya nchini Waziri Mkuu akikagua maonyesho ya wadau wa Mawasiliano bungeni leo Waziri Mkuu akijibu maswali ya wanahabari baada ya kutembelea maonyesho hayo  

MAFANIKIO YA CMSA YAMELIHESHIMISHA TAIFA------Nicodemus Mkama

Image
AFISA   Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),  Nicodemus Mkama ( pichani hapo juu) amesema  “Mafanikio ya utoaji na kuorodheshwa kwa Hatifungani ya Tanga UWASA kwenye Soko la Hisa la Dar es salaam, unaimarisha nafasi ya masoko ya mitaji ya Tanzania kwenye ramani ya masoko ya mitaji ulimwenguni, yanayotoa bidhaa bunifu na endelevu, zinazovutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa. Sambamba na hilo amesema kuwa Mamlaka hiyo imeweza kuwa na mafanikio makubwa na kuvuka lengo ambalo walikuwa wamejipangia. Aidha amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi madhubuti wa  Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisaidiwa na  Waziri wa Fedha kuisimamia Sekta ya Fedha, Masoko ya Mitaji Tanzania yamekuwa imara, himilivu na yenye mafanikio makubwa, licha ya uwepo wa athari za janga la UVIKO-19 na migogoro ya kimataifa. Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa Thamani ya uwekezaji katik