Posts

Showing posts from March, 2018

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu

Image
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu Wizara ya afya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria katika juhudi  zake za kupambana na ugonjwa wa Malaria kinakusudia kutoa vyandarua laki moja na 95 elfu kwa mama wajawazito na watoto waliochini ya miaka mitano nchi nzima . Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar juu ya uzinduzi wa Kampeni ya kubwa ya matumizi ya vyandarua ambayo inatarajiwa kufanyika April nne mwaka huu visiwani Zanzibar Meneja wa utaribu wa kazi za kumaliza Malaria Zanzibar Abdallah Suleiman Ali amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimokatika mchakato wa kumaliza Malaria ambapo kwa sasa ni zaidi ya miaka kumi Zanzibar imekuwa ikipambana na ugonjwa huo . Amesema Zanzibar kila kipindi kinachomaliza mvua za masika kumekuwa na kiwango kikubwa ugonjwa Malaria lakini jitihada mbali mbali zinachukuliwa ikiwemo kupiga dawa majumbani, kuhakikisha dawa zinapatikana katika vit

UMAKINI MKUBWA

Image
Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe (kushoto) na Waziri wa Fedha, Taro Aso, wakifuatilia mjadala katika Bunge la Juu mjini Tokyo juzi.

MIGUNA MIGUNA NA SAKATA NA SERIKALI YA KENYA

Image
  Dk. Miguna pichani   asimulia alivyojikuta Dubai DUBAI, UAE MWANASHERIA na mwanaharakati wa upinzani wa Kenya, Miguna Miguna, ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Dubai amesimulia namma alivyojikuta nchini hapa. Dk. Miguna pia ameitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia arudi Kenya kwa vile anateseka.   “Niliamka nikiwa hapa Dubai na bila kitu. Nahitaji jumuiya ya kimataifa na kila mtu kuingilia kati suala hili,” Dk.   Miguna alisikika akimwagiza mmoja wa wanasheria wake kwa simu kuvijuza vyombo vya habari vya kimataifa. Mwanasheria huyo alisisitiza atapanda tu ndege itakayoelekea Nairobi, si vinginevyo. “Sitarajii kukubali kupanda chochote, kwa sababu ni kinyume na matakwa yangu. Mimi ni mgonjwa na siwezi hata kutembea, walichukua miwani yangu na walichukua kila kitu,” alisema akiwa hospitali. Akisimulia jinsi alivyoamka asubuhi na kushangaa kujikuta akiwa Dubai, Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE), Dk. Miguna alisema: “Mimi ni abiria niliye katika eneo l