Posts

Showing posts from October, 2022

*JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA*

Image
Vijana wa  Kisukuma wakichunga mifugo yao   *JUA AINA NNE ZA KABILA LA WASUKUMA* AINA ZA WASUKUMA NA KISUKUMA Lugha ya kisukuma ina lahaja kuu nne; *ginantuzu,* *ginang'weli,* *ginangw'agala* na *gidakama*. Vivyo hivyo, Wasukuma wamegawanyika katika *misingi  ya lahaja za lugha ya kisukuma.* 1. *Bhadakama*. Hawa wanapatikana sehemu za mji wa Shinyanga, sehemu za Gahama na sehemu za Igunga na Nzega. Kwa idadi, hawa ndiyo Wasukuma wachache sana. Ni watu wenye aibu, wakimya mno... wana muingiliano na utamaduni wa Wanyamwezi. Pengine hawa ndiyo Wasukuma masikini kuliko aina yoyote ya Wasukuma! 2. *Bhanang'weli.* Hawa ni Wasukuma wenyeji wa mikoa ya Mwanza, Geita, na kusini - Magharibi mwa Mkoa wa SIMIYU. Kiidadi, hawa ndiyo Wasukuma wengi sana... katika ongea yao, wana matumizi mengi ya 'shi'  kwa mfano, shikolo, shiliwa. Pia hawatumii 'ng'wadila' katika salamu za jioni. Wao hutumia 'gawiza' au 'dillo gawiza'  Kwa sababu wanaishi katika strat

WABUNGE WAPYA WA BUNGE LA AFRIKA WAAPISHWA

Image
  Wabunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Mhe. Anatropia Theonest, Mhe. Toufiq Salim Turkey na Mhe. Ng’wasi Damas Kamani wakila kiapo kuwa wabunge wa Bunge la Afrika wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika   Na Kadama Malunde – Midrand Afrika Kusini Rais wa Bunge la Afrika (Pan – African Parliament – PAP) Mhe. Chief Fortune Charumbira amefungua Kikao cha Kwanza cha Kawaida cha Bunge la Sita la Afrika huku Wabunge Wabunge 11 kutoka Burundi, Morocco, Msumbiji, Somalia na Tanzania wakiapishwa kuwa Wabunge wa Bunge la Afrika (PAP).   Mkutano huo wa Bunge unafanyika katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika Midrand Johannesburg Afrika Kusini ukiongozwa na Kauli Mbiu ya Umoja wa Afrika ya Mwaka 2022 “Kujenga Uthabiti kwenye Lishe katika Bara la Afrika : Kuongeza mtaji wa watu, maendeleo ya kijamii na kiuchumi”.   Wabunge wapya wa Bunge la Afrika waliokula kiapo ni Mhe. Anatropia Theonest, Mhe. Toufiq Salim Tu

DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI BUNGENI

Image
  Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha kamati ya uongozi cha kupokea na kujadili Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano wa Tisa wa Bunge leo tarehe 31 Oktoba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. Wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakiwa katika kikao cha kamati hiyo cha kupokea na kujadili Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano wa Tisa wa Bunge leo tarehe 31 Oktoba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya katibu na Sheria, Mhe. Joseph Mhagama na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali, Mhe. Japhet Hassunga. Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa mwihambi, ndc akishiriki katika kikao cha kamati ya uongozi cha kupokea na kujadili Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano wa Tisa wa Bunge leo tarehe 31 Oktoba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. Emmanuel Mwakilasa (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WATANZANIA SASA TUPO MILIONI 61,741,120

Image
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan,akizungumza na  Viongozi pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma waliofika kushuhudia uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  mwongozo wa matumizi ya takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Ally Mwinyi,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  mwongozo wa matumizi ya takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma. MWENYEKITI wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi na  mwongozo wa matumizi ya takwimu za Sensa kwa mwaka 2022 hafla iliyofanyika leo Oktoba 31,2022 jijini Dodoma. MAKAMO wa Pili wa Rais,Zanzibar na Mwenyekiti Mwenza wa

TANROADS YA MHANDISI ROGATUS MATIVILA YAMUONYESHA VIFAA VYA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA KISASA WA MSALATO RAIS SAMIA NA KUUZINDUA

Image
Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Rogatus Mativila, akieleza jinsi uwanja huo utakavyokuwa Mitambo ya kazi  uwanjani Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Rogatus Mativila, akieleza jinsi uwanja huo utakavyokuwa Zana za kazi zikiwa katika eneo la uwanja tayari kuanza kazi Wasanii wa bendi ya TOT, wakiingia stejini  kumwaga radhi Wasanii wa kundi la Mwinamila wakifanya vitu vyao TOT Taarabu chini ya Khadija Kopa, wakionyesha vitu vyao Markia wa Taarabu nchini Khadija Kopa, akiwapagawisha wageni waalikwa katika uzinduzi huo Baadhi ya wakuu wa mikoa Markia wa Taarabu nchini Khadija Kopa, akiwapagawisha wageni waalikwa katika uzinduzi huo Vijana wa hamasa  wa CCM wakitoa Burudani Rais Samia akisalimiana na viongozi baada ya kuwasili Watangazaji wa TBC nao walikuwepo wakiwajibika Nifuraha tupu Waziri Mchemba akienda kutunza fedha msanii Dula Rais Samia Sululu Hassan na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dk Patricia Laverley wakishuhudia wasanii wakitoa burudani Mwiguru Nchemb