Posts

Showing posts from July, 2014

RAIS WA ZANZIBAR ASHIRIKI SWALA YA IDD ZENJI

Image
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Waislamu mbali mbali na Viongozi katika Swala ya Eid el Fitri iliyoswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi katika kusherehekeka mfunguo wa Mwezi Mtukufu wa  Ramadhan   Baadhi ya waislamu waliomaliza Swala ya Eid el Fitri wakimasikiliza Sheikh Mziwanda  Ng'wali  Ahmed  (hayupo pichani ) alipokuwa akitoa Khutba baada ya swala hiyo ambapo aliwataka waislamu kusherehekea Sikukuu ya Eid kwa upendo na mashirikiano katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar  leo asubuhi   Sheikh Mziwanda  Ng'wali  Ahmed (aliyesimama) akitoa Khutba baada ya Swala ya  Eid el Fitri mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi mbali mbali wa Kitaifa na Wailslamu waliojumuika kwa pamoja katika viwanja  vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar leo asubihi. Rais wa Zanzibar na

RAIS KIKWETE ASWALI IDD DAR

Image
Rais.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mlemavu  baada ya kumalizika kwa swala ya Iddi katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali sala ya Iddi El Fitr katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi   Rais akisalimiana na waumini wenzake wakati wa kuondoka

TIMU YA STARS KAMBINI MBEYA

Image
  Kocha mkuu wa Timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars Mart Najool katikati akiwaongoza wachezaji kulihamisha goli jana katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Tukuyu wakati wa mazoezi ya kujiwinda   na   mchezo wa marudiano dhidi ya Msumbuji   Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars wakiwa katika mazoezi ya kuruka viunzi jana katika uwanja wa Chuo cha ualimu Tukuyu,mazoezi hayo ni kwa jili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Msumbiji   The Mambas kusaka tiketi kuelekea michuano ya Africon