Posts

Showing posts from September, 2017

Kituo cha Mabasi Ubungo kuzalisha ajira 20,000

Image
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na ugeni kutoka Jiji la Shanghai nchini China na kujadili mambo mbalimbali yamaendeleo jijini hapa ikiwemo suala la uboreshaji wa kituo cha Mabasi Ubungo. Ugeni huo uliambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Linghang Cathy Wang ambayo ndiyo imeingia mkataba na Halmashauri ya jiji kwa ujenzi wa kituo hicho.Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, Meya Mwita alisema kuwa ugeni huo umeridhia kuwekeza katika nyanja mbalimbali ikiwemo kituo cha mabasi ubungo. Alifafanua kuwa jiji la Dar es Salaam linakaribia kunza kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa kubadilisha kituo cha mabasi ubungo na kwamba hatua mbalimbli zimeshakamilika ili kupisha mradai huo.Alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo jumla ya watanzania 20,000 watapata ajira jambo ambalo litawezesha kuongeza kipato kwa wananchi na hivyo pia kuwe