Kituo cha Mabasi Ubungo kuzalisha ajira 20,000


NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na ugeni kutoka Jiji la Shanghai nchini China na kujadili mambo mbalimbali yamaendeleo jijini hapa ikiwemo suala la uboreshaji wa kituo cha Mabasi Ubungo.
Ugeni huo uliambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Linghang Cathy Wang ambayo ndiyo imeingia mkataba na Halmashauri ya jiji kwa ujenzi wa kituo hicho.Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, Meya Mwita alisema kuwa ugeni huo umeridhia kuwekeza katika nyanja mbalimbali ikiwemo kituo cha mabasi ubungo.

Alifafanua kuwa jiji la Dar es Salaam linakaribia kunza kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa kubadilisha kituo cha mabasi ubungo na kwamba hatua mbalimbli zimeshakamilika ili kupisha mradai huo.Alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo jumla ya watanzania 20,000 watapata ajira jambo ambalo litawezesha kuongeza kipato kwa wananchi na hivyo pia kuwezesha vijana kuondokana kwenye makundi ambayo sio salama.

Alisema kufanikisha kwa mradi huo, utasaidia pia kuongeza mzunguko wa fedha jijini hapa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kibiashara.“ Leo nimekutana na ugeni ambapo kwa kiasi kikubwa mnafahamu ndugu zetu hawa wamekuwa na urafiki mkubwa katika nchini yetu, tumejadiliana mambo mengi ambayo yote ni yakuleta maendeleo katika jiji letu.

“ Lakini kubwa zaidi ni kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi Ubungo, ambapo hivi karibuni tunatarajia kuanza kwa mradi huo, na wananchi pia watajulisha, nitumie fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa jiji linafuata utaratibu katika kutekeleza mradi huo” alisema Meya Mwita.

“ Fursa hii ni kubwa ambayo tumeipata, watanzania watapata ajira, mzunguko wa fedha kwenye jiji letu utaongezeka, kama Meya wa jiji hili nimewakaribisha tufanye kazi pamoja, lengo likiwa nikuweka jiji kwenye muonekano mzuri” aliongeza.Kwaupande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Linghang Cathy Wang alimpongeza Meya Mwita kutokana na aina ya utendaji wake wa kazi nakuahidi kuonyesha ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo.

Alisema kuwa Meya Mwita ni kiongozi anayefanya kazi kwa bidii na umakini na kwamba kutokana na jitihada hizo za kulijenga jiji , kampuni yao itafanya  kazi na kumuhakikisha kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA MAKUMBUSHO MAPYA YA OLDUVAI NA ONESHO LA CHIMBUKO LA MWANADAMU

Morogoro, Septemba 28, 2017.

Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya imekamilisha ujenzi wa Makumbusho mapya ya Olduvai ambayo yanaonesha Chimbuko la Binadamu (The Cradle of Humankind) katika Bara la Afrika.
Makumbusho hayo mapya pamoja na Onesho la Chimbuko la Binadamu, yatafunguliwa rasmi na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tarehe 03 Oktoba, 2017 katika eneo la Olduvai, ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Onesho hilo ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu uliofanyika katika Bonde la Olduvai na Laetoli katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Wananchi, viongozi mbalimbali wa kitaifa na Mabalozi wanatarajiwa kuhudhuria kwenye hafla hiyo.
Idadi kubwa ya vioneshwa katika Makumbusho hiyo, vilipatikana katika bonde la Olduvai na Laetoli nchini Tanzania kupitia utafiti wa kisayansi wa muda mrefu na vilikuwa vimehifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. Vioneshwa hivi ni pamoja na masalia ya zamadamu, zana za mawe na masalia ya wanyama walioishi takribani miaka milioni 4 iliyopita.
Makumbusho hayo yamepangwa kuonesha sehemu kuu nne zinazowiana.  Sehemu ya kwanza inahusu ushahidi wa nyayo za zamadamu zilizongunduliwa huko Laetoli mwaka 1978 na mtafiti Dr. Mary D. Leakey.  Nyayo hizi ziliachwa na zamadamu anayeiitwa Australopithecus afarensis na ndio ushaidi usiopingika wa zamadamu kutembea wima kwa miguu miwili takribani miaka milioni 3.6 iliyopita.
Sehemu ya pili inahusu hadithi ya kusisimua ya kuwa binadamu (Genus Homo); ambapo kutakuwa na masalia ya zamadamu wanaoitwa Zinjanthropus au Paranthropus boisei na Homo habilis, zana za mawe za mwanzo zilizotumika (Oldowan) katika kujipatia chakula na ushahidi wa kale wa ulaji wa nyama katika historia ya mabadiliko ya binadamu, takribani miaka million 2 iliyopita.
Sehemu ya tatu inahusu maisha ya jamii ya Homo erectus.  Jamii hii ilikuwa inafanana zaidi na binadamu wa sasa kuliko jamii zilizotangulia. Kutakuwa na masalia zamadamu Homo erectus, zana za mawe (Acheulian) na ushahidi wa ulaji wa wanyama wakubwa kama vile Nyati na tembo katika historia ya mabadiliko ya binadamu, takribani miaka million 1.7 iliyopita.
Sehemu ya nne inaonesha kipindi cha mwanzo cha binadamu wa sasa (Homo sapiens) walioanza kutokea hapa Afrika miaka laki 2 iliyopita. Sehemu hii pia itaonesha mila na utamaduni wa makabila mbalimbali kama vile Wahadzabe, wamasai na Datoga.  Kutakuwa na mavazi ya asili ya jamii hizo, zana za kuwinda na vifaa mbalimbali wanavyovitumia katika maisha yao ya kila siku.
Wizara ya Maliasili na Utalii inawakaribisha wananchi wote kuhudhuria ufunguzi huo ambapo watapata pia fursa ya kutembelea vivutio vingine vilivyopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kujifunza na kufurahia urithi huu wa asili na kiutamaduni wa Taifa letu.
Imetolewa na;

Prof. Jumanne Maghembe
Waziri wa Maliasili na Utalii
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani Morogoro kuhusu uzinduzi wa Makumbusho Mapya ya Olduvai na Onesho la Chimbuko la Mwanadamu ambayo yatazinduliwa tarehe 03 Oktoba, 2017 na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Olduvai wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. 

 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani Morogoro kuhusu uzinduzi wa Makumbusho Mapya ya Olduvai na Onesho la Chimbuko la Mwanadamu ambayo yatazinduliwa tarehe 03 Oktoba, 2017 na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Olduvai wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. (Picha na Hamza Temba - WMU).

KIITEC LAUNCHED SOLAR POWER PLANT AND SOLAR LABORATORY

Excellency Malika Berak, Ambassador of France in Tanzania (C) cuts a ribbon to officiate the launch of Solar Power plant and laboratory at KIITEC in Arusha, others in photo are senior officials from the partners institutions supporting the Institute. 
FTE President Fransis Bronchon,(R) briefing invited guests on Solar Project at KITEEK during the launch event at Arusha. 
Excellency Malika Berak, Ambassador of France in Tanzania(C) got briefing on project from, Albert Mtana, (R)-Teacher of Electrical and Solar Photovoltaic System (L) is Michel Ramser-VP Strategic Marketing and Sponsorship (ADEI). 
Solar panel installed at the centre. The Kilimanjaro International Institute for Telecommunications, Electronics and Computers (KIITEC) has launched 30KW solar power plant and solar laboratory at its training centre in Arusha recently. The Guest of Honour at launch event was Her Excellency Malika Berak, Ambassador of France in Tanzania, also the event brought together the partners that have supported KIITEC for many years. 

These are: Schneider Electric East Africa, the Schneider Electric Foundation, ADEI, EDF Help and the Foundation for Technical Education (FTE). Speaking during the event, KIITEC Director of studies, Mr. Daniel Mtana, said the opening of this solar power plant speaks to the accomplishment of institute’s vision to become the centre of training excellence for renewable energy, particularly solar photovoltaic systems in East Africa. 

“Committed to true hands-on experience, KIITEC has now invested heavily in photovoltaic solutions and strives to be recognized as the premier provider of quality technical education in a student-centered community.” General manager at Schneider Electric East Africa, Mr. Mr. Edouard Heripret, said in most sub-Saharan countries, the rate of enrolment in formal secondary technical and vocational training and education (TVET) does not exceed 5%. 

“Vocational training has always been at the heart of Schneider Electric’s DNA. In East Africa, we have been committed to support technical training since 2009. Kiitec was one of our first training partners and I am pleased today to participate in the inauguration of the solar plant and laboratory, as these new components will allow students to have a full set of competencies to enter the labour market and will support access to energy for everyone.” Mr. 

Heripret added “At Schneider Electric, we are building sustainable communities through energy knowledge and leadership, thanks to the Schneider Electric Foundation. Its aim is to contribute to the development of people and societies through education, innovation, awareness-raising and vocational training related to energy. 

It acts, anywhere in the world where the company is present, through its three programmes. KIITEC is an international technical institution, was founded in 2004 by French engineers and has produced some of the most competent technicians in the country. Two NGOs, the Foundation for Technical Education (FTE-Swiss) and Action Development Education International (ADEI-French), support the institution. Schneider Electric assists ADEI in its support of KIITEC. 

The institute is a pilot centre, with the goal of transposing and exporting its model from Tanzania, to Kenya. It provides its students with the basic skills in telecommunications, electronics, information science, networks and industrial automation systems. 

The training lasts over two years. It comprises lectures complemented by practical training, project design, and a three-month outplacement in a company. As of today, 350 young people, comprising 90% of the students, have obtained their diploma, the ‘National Technical Award’, which is recognized by the local government, and have all found jobs, mainly in the industrial maintenance sector.

Serikali Kuzichukulia Hatua Taasisi Zilizokiuka Taratibu za Manunuzi 2016/2017

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga (kushoto) akiongea wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma,  Kulia ni Mjumbe wa Bodi hiyo Prof. Sufian Bukurura.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga wakati wa makabidhiano ya Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akikata utembe baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akionesha kwa wanahabari na wajumbe wengine wa Bodi(hawapo pichani) kitabu cha Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, , Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma ambapo ameahidi kuzichukulia hatua taasisi zote zilizokiuka taratibu za manunuzi zilizoainishwa kwenye Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
 Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Dkt. Laurent Shirima akiongea, wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA).PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO.

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Serikali imesema itazichukulia hatua Taasisi zote zilizokiuka sheria na kanuni za manunuzi ya Umma pamoja na zile zenye viashiria vya rushwa ambazo zimebainika katika ripoti ya tathmini ya utendaji iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa mwaka wa Fedha 2016/17.

Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa akipokea ripoti ya tathimini ya utendaji wa Taasisi za Serikali katika sekta ya Manunuzi iliyofanywa na PPRA kwa mwaka wa Fedha 2016/17.

“Tutazichukulia hatua na kuziwajibisha taasisi zote ambazo zimebainika katika ripoti hii kuwa na viashiria vya rushwa au kufanya malipo yenye utata katika manunuzi yao,” alisema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango amesema kuwa, zaidi ya 70% ya fedha za Umma zinatumika kununua vifaa na huduma mbalimbali hivyo Serikali haitavumilia kuona fedha hizo zinatumika bila kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA Balozi Dkt. Matern Lumbanga amezitaja taasisi ambazo zimekiuka sheria na taratibu za manunuzi kwa mwaka 2016/2017 kuwa ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi ya Mifupa (MOI) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Taasisi nyingine ni Shirika la Bima la Taifa (NIC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya Anga (TCAA), Wizara ya Fedha na Mipango na Halmashauri ya Wilaya Kondoa. 

Balozi Lumbanga amesema kuwa uchunguzi wa zabuni mbili zenye thamani ya shilingi bilioni 160.5 ambazo zilikuwa zinatekelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja TCAA haukubainika mapungufu ya msingi na PPRA ilipendekeza utekelezaji wa miradi hiyo uendelee kama ilivyopangwa.

“Uchunguzi uliofanywa katika taasisi sita zilizobaki ulibaini kuwa Serikali ilipata hasara ya takribani shilingi milioni 12.15 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo, ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi uliosababisha ongezeko la riba pamoja na faini zilizotokana na ukiukwaji wa taratibu za kijamii na mazingira kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa kazi za ujenzi,” alisema Balozi Lumbanga.

Balozi Lumbanga amezitaja Taasisi zilizobainika na malipo yenye utata kuwa ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Halmashauri ya Kwimba. Ukaguzi wa kupima upatikanaji wa thamani ya fedha ulibaini malipo yenye utata katika taasisi hizo tatu ambazo ni kiasi cha shilingi milioni 483.44 zililipwa kwa wakandarasi kwa kazi ambazo hazikuwa zimefanyika.

Vile vile amesema kuwa, miradi 33 katika taasisi 17 ilibainika kuwa na kiwango kikubwa cha viashiria vya rushwa. Taasisi hizo ni Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka za Moshi (Muwasa), Mwanza (Mwauwasa) na Arusha (Auwasa) pamoja na Halmashauri ya Wilaya za Wilaya za Msalala, Kibondo na Moshi.

Taasisi byingine ni Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Chuo cha Ufundi Arusha, Halmashauri ya Mjia wa Kahama, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Halmashauri ya Mji wa MAsasi pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Ripoti hiyo ni ripoti ya 11 kuwasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango tangu PPRA ilipoanzishwa.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI YAFANYIKA ZANZIBAR

Muakilishi wa Jimbo la Mpendae Said Mohd Dimwa wapili kushoto akifuatana na Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika Maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliofanyika katika Ofisi ya Jumuiya ya watu wenye maradhi yasioambukiza (ZNCDA)Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja
Maandamano yalioongozwa na Bend ya Chipukizi yakielekea katika Ofisi ya Jumuia ya watu wenye maradhi yasioambukiza katika maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja
Vikundi mbalimbali vya mazoezi vikishajiisha suala zima la ufanyaji mazoezi ili kulinda afya na maradhi mbalimbali, katika siku ya maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
Makamo mwenyekiti wa ZNCDA Ali Zubeir Juma akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
Mgeni rasmi katika maadimisho ya siku ya Moyo Duniani Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Said Mohd Dimwa akitoa hotuba kuhusiana na kujikinga na maradhi mbalimbali yanayotokana na Ulaji,Unywaji wa Pombe na Uvutaji wa Tumbaku katika maadhimisho hayo yliofanyika katika Ofisi ya Jumuiya ya watu wenye maradhi yasioambukiza (ZNCDA)Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kupimwa afya zao katika maadhimisho ya Siku ya moyo Duniani 29/09/2017.Mpendae Wilaya ya Mjini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Airtel yatoa mafunzo ya TEHAMA kwa Walimu Dar


Kampuni yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi)  imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa waalimu katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama Manispaa ya Kinondoni. 
Mafunzo hayo kwa waalimu yameanza kufuatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa mafunzo hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za msingi,sekondari, vyuo vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia kuvumbua application mbalimbali, kuwapatia vijana ujuzi katika mswala ya Tehama na pia kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara kwa kutumia technologia za kisasa. 
Akiongea kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde alisema,
‘Hapo awali tulikuwa tumeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi lakini tumeona ni bora na waalimu wa hapa shule hii Kijitonyama nao waanze kupata mafunzo. Hii itasaidia kwani kwa baadae ndio watakaokuwa wakitoa mafunzo kwa wanafunzi na hii itatupa nafasi ya kuendelea kuwezesha shule zingine.
Waalimu wamepokea hatua hii kwa furaha na wanao hamasa kubwa kwenye mafunzo. Hii inathibitisha nia ya kampuni ya Airtel ya kutoa fursa kwa kila Mtanzania, aliongeza Matinde.
Hata hivyo, Matinde alisema kuwa mafunzo kwa wanafunzo ambao walikuwa washaanza yataendelea vile vile. ‘Utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wale wanafunzi ambao walikuwa washaanza utaendelea vile vile. Kilichofanyika ni chukua hatua ya ziada ya kuwapa walimu mafunzo ya Tehama ili nao waweze kuwa kwenye nafasi ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi hawa’ alisema Matinde. 
Matinde aliongeza kuwa bado tunapokea maombi ya kujiunga hivyo tunatoa wito kwa vijana wa sekondari , wale waliomaliza darasa la saba , wafanyabiashara kutumia vyema maabara hii yenye lengo la kuwezesha jamii  hususani vijana kuongeza ujuzi na ueledi kwenye maswala ya technologia na Tehama kwa ujumla. 
Kwa upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Agape Jengela alisema “ Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa walimu wa shule ya Kijitonyama. Tuhahakisha kuwa walimu wamepata mafunzo na kuelewa kabisa ili nao waanze kutoa mafunzo na elimu kwa wanafunzi. 
Jengela alisema mafunzo hayo ni pamoja na lego Robotics, program za uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects”  msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali. 
Bado tunapokea maombi,   Tunato wito kwa wazazi na walezi kuwaandikisha vijana wao kwa kupitia  www.teknohama.or.tz na  www.airtelfursa.com  au kwa kutembelea maabara  iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama

MBUNGE AZZA HILAL AWAPIGA JEKI WANAFUNZI WENYE ULEMAVU SHULE YA MSINGI ALIYOSOMA SHINYANGA

Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu (hatembei wala haongei) katika shule ya msingi Tinde-Picha na Said Nassor-Malunde1 blog Tinde

Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) ametembelea shule ya msingi aliyosoma Tinde iliyopo katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga kisha kutoa msaada kwa wanafunzi nane wenye ulemavu wa viungo akiwemo kijana ambaye hawezi kuongea wala kutembea. Mbunge huyo ametembelea shule hiyo jana Jumatano Septemba 27,2017. 
Mheshimiwa Hilal ametoa msaada wa baiskeli kwa kijana ambaye hawezi kutembea wala kuongea anayesoma katika shule hiyo huku akijitolea kuwanunulia wanafunzi hao nane mahitaji yao yote ya shule mpaka watakapomaliza masomo yao ya shule ya msingi. 
“Hii shule nimesoma,baada ya kufika hapa nimeambiwa kuna watoto wenye ulemavu,baada kumuona kijana huyu nimempatia baiskeli lakini pia nimejitolea kuwahudumia wanafunzi hawa wanane ambao wana ulemavu wa viungo,nitawanunulia mahitaji yao ya shule na watakuwa wanakunywa uji kila siku kwa gharama zangu”,ameeleza Mbunge huyo. 
Mbali na kutoa msaada huo Mheshimiwa Azza Hilal ameshiriki zoezi la Upandaji miti katika wilaya ya Shinyanga lililoanzishwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro lenye kauli mbiu ya "Shinyanga Mpya, Mti Kwanza". 
Akiwa katika kata ya Tinde,mbunge huyo aliungana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kupanda miti katika shule ya msingi Tinde,pia katika barabara kuu ya kutoka Tinde kwenda Kahama na barabara ya kutoka Tinde kwenda Nzega mkoani Tabora.
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal (CCM) akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo katika shule ya msingi Tinde,aliyeshikilia kipaza sauti ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akiwa na mwanafunzi aliyepata msaada wa baiskeli kutoka kwa Mheshimiwa Azza Hilal 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akipanda mti katika shule ya msingi Tinde.


Picha na Said Nassor-Malunde 

PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA NCHI 21 DUNIANI KWA AJILI YA KUJADILI UKUKUZAJI WA SEKTA YA UPANDAJI WA MITI KIBIASHARA

Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. Aliwataka wajumbe hao kujadili namna ya kuwawezesha wakulima wa miti wakati wanasubiri kuvuna mazao yao waweze kujishuulisha na kilimo cha mazao ya muda mfupi kwa kutumia mbinu bora za kisayansi ili waweze kujikimu kimapato.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi 21 duniani wakifuatilia mkutano huo. Nchi hizo ni Burkina Faso, Chad, Ethiopia, Gambia,Ghana, Italy, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sudan, Liberia, Cameroon, Swaziland, Finland, Zambia, Canada,Mozambique, Zimbabwe, Kenya na Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Steven Kebwe akizungumza katika mkutano huo. Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili na kuishauri dunia namna bora ya kutunza na kuendeleza misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho ikiwemo utekelezaji wa sheria za usimamizi wa misitu.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wajumbe kujadili kwa uwazi kuhusu mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto za sekta ya misitu na kwamba Serikali kupitia Wizara itapokea maoni na mapendekezo yao kwa ajili ya kuyafanyia kazi ili kuimarisha ustawi wa sekta hiyo. 
Waziri Maghembe akieleza jambo kwenye ka mkutano huo ambapo aliwataka wajumbe wajumbe wajadili namna bora ya kuwafundisha wakulima wa miti kufanya kilimo bora ikiwa ni pamoja na mafunzo uvunaji wa hewa ukaa ili kuwainua kimapato. Aliwataka pia kusaidia wakulima wa miti katika upatikanaji wa masoko ya uhakika.
  Prof. Maghembe akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza mkoani Morogoro jana na baadhi ya viongozi waliondaa mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika muda mfupi kabla ya kufungua mkutano huo wa siku mbili uliowashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
  Baadhi ya wajumbe walishiriki mkutano huo kutoka nchi 21 duniani.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na Mbunge kutoka Kenya, Chariti Katambi mkoani Morogoro jana baada ya kufungua mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro jana baada ya kufungua mkutano wa pili wa Mashirika yanayohamasisha upandaji wa miti kibiashara na uzalishaji wa mazao ya misitu barani Afrika, mkutano huo wa siku mbili umewashirikisha wajumbe kutoka nchi 21 duniani kwa lengo la kubadilishana mawazo juu ya kuboresha uzalishaji na upatikanaji wa masoko. 
Picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

"Mafunzo ya Elimu ya ufundi yana nafasi ya kukuza ajira"- Rutayuga

Mafunzo ya elimu ya ufundi yananafasi kubwa ya kuongeza, kusaidia na kukuza ajira kwa vijana wanaosoma masomo hayo kwenye vyuo vya ufundi kwa kuajiriwa au kujitengenezea ajira wao wenyewe.
 
 Kaimu katibu mtendaji wa baraza la taifa elimu ya ufundi (Nacte), Dkt, Adolph Rutayuga amesema hayo leo jijini dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO.
 
Akizungumza kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia, Dkt, Rutayuga amesema nia kubwa ya mradi huo ni kuangalia ufundi unaumuhimu gani kwenye sekta ya uchumi hasa unapozungumzia sekta ya uchumi wa viwanda. Aidha tunaangalia ubora wa mafunzo yanayotolewa kwenye elimu ya ufundi sababu kukiwa na vyuo vingi ambavyo vinaendeshwa katika ubora usiotakiwa, wanafunzi wanaotoka kwenye vyuo hivi hawatakuwa wazuri. 
 
“Tunalenga kujenga mazingira ya kutoa mafunzo bora kwenye elimu ya ufundi, elimu iliyobora kwa kusapoti walimu wanaofundisha,miundombinu ya kujifunza na kufundishia na pia kujaribu kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya viwanda na soko la ajira kwa kile kinachotolewa kwenye vyuo vya ufundi.
 
 Ameongeza,kama suala zima la mambo ya mitaala, linaweza kuboreshwa, na ile dhana potufu ya kizamani iliyokuwepo kwamba kwamba Tivet ni kwa wale walioshindwa,inapaswa iondoke, watu wajue kwamba mchango mkubwa kwenye uchumi unafanywa na hawa watu kwenye sekta ya kati “Malengo makubwa ni kujaribu kuinua ubora wa mafunzo yanayotolewa na vyuo vya ufundi, kuinua umuhimu mafunzo ya ufundi na Jinsi inavyoweza kisaidia kwenye maendeleo ya kukuza uchumi,” amesema. 
 
Naye, Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe amesema warsha hiyo itajadili kwa undani vitendo vya ufanisi, utekelezaji na jukumu la uwezo ambao kila wadau watafanya katika mradi uliopendekezwa chini ya maeneo matatu umuhimu, ubora na mtazamo wa elimu na ujuzi wa kiufundi. “Elimu bora kwa Afrika itatekelezwa kuanzia mwaka huu hadi 2021 kwa lengo la kukuza elimu na ujuzi wa kitaaluma na mafunzo ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya watu binafsi na jamii”amesema Plathe. Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii .Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza washiriki wa warsha ya kuzindua Mradi wa mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Rutayuga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Unesco ya kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washririki na Meza kuu wakiwa katika warsha ya uzinduzi wa Mpangowa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya washririki wa Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Mtoa maada akizungumza na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.