Posts

Showing posts from September, 2022

MATOKEO YA TAFITI KUHUSU KUCHAGIZA HAKI ZA WAZEE

Image
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Taifa Lameck Sendo, akikata utepe kuzindua Taarifa ya Utafiti kuhusu wazee nchini Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dodoma leo.Wengine toka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Morogoro, Leah Nzali, Mjumbe wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma Mary Buregi na Katibu wa Baraza hilo Mkoa wa Dodoma Oswin Kachenje. Baadhi ya Viongoziwa Baraza la Wazee nchini wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Help Age,Tume ya Haki za Binadamu,Taasisi ya Mwalimu Nyerere na Waandishi wa habari wakiwa wameshikilia na lipoti hiyo. Mkutano huo umefanyika jijini Dodoma leo. Meneja Program, Haki,Sera na Ushirikiano wa wadau wa wazee Joseph Mbasha, akitoa mada katika mkutano huo Mkurugenzi wa masuala ya Wazee wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Joshua Taramo, akitoa mada iliyohusu mfumo wa muundo wa haki za wazee kwa kuzingatia itifaki ya haki za wazee. Kaatika warsha iliyofanyika jijini Dodoma leo. Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini Nevill

SHEIN AANZISHA MJADALA WA KUHUSU MASUALA YA WAZEE NCHINI LEO DODOMA

Image
Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt, Ally Mohamed Shein, leo jijini Dodoma amefungua mjadala wa wazee nchini , akisema hakuna aseti kubwa katika Taifa lolote bila wazee,  na nchi bila wazee ni kama taifa la wafu, amewataka vijana wale kuwapenda wazee wao kwani hata wao wakumbuke ni wazee wa kesho. Aidha amelaani tabia ya kuwashambulia wazee na wengine kuwashambulia na kuwasababishia mauti kwa kisingizio ni wachawi na sababu mbalimbali ambazo yeye ameziita hazina sababu  za msingi. Wazee wengi wa vijiji hasa katika nchi zetu za kiafrika hukumbwa na masahibu mengi baadhi kutokana na kutokuwa na nishati ya kueleweka hupikia kuni katika maisha yao yote na kusababisha baadhi kuwa na macho mekundu , mzee anapoonekana anamacho mekundu hudhaniwa ni mchawi kibaya zaidi hata katika familia yake hudhaniwa hivyo na baadhi kukimbia makazi yao kwenda kusikojulikana.. Rais huyo msaatu amesema muda umefika sasa kuwa na majadala wazee watunzweje  ili kuondokana na manyanyaso hayo katika nchi zao. Mjadala huo