Posts

Showing posts from June, 2022

RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA MKUU WA MAJESHI JENERALI MABEYO NA KUAGANA NAE KISHA KUTEUA MKUU MWENGINE WA MAJESHI

Image
-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo. Jenerali Mabeyo alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumuaga Mhe. Rais Samia wakati akimaliza kipindi cha Utumishi wake katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo Ikulu Jijini Dar es Salaam.  

Rais Samia akutana na Wajumbe wa bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku ambaye aliambatana na wajumbe wa Bodi hiyo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku ambaye aliambatana na wajumbe wa Bodi hiyo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Juni, 2022. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku ambaye aliambatana na wajumbe wa Bodi hiyo mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Juni, 2022.  

VIONGOZI WA WIZARA YA Utamaduni, Sanaa na Michezo WAKIWA BET AWARDS

Image
Picha za kipekee kutoka jijini Los Angeles nchini Marekani wakati Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa alipo udhuria tamasha la utoaji tuzo za BET kwa mwaka 2022, lililofanyika usiku wa kuamkia June 27 katika ukumbi wa burudani (arena) wa Microsoft theater. Katika ziara hiyo Waziri Mchenegerwa ameambatana na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi pamoja na Mkurugenzi wa Sanaa dkt. Emmanuel Ishengoma katika kutafuta ujuzi wa namna ya kuandaa tuzo kwa kiwango cha kimataifa, lengo likiwa ni kuunga mkono juhudu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuitangaza Tanzania wakati ambapo Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA – MTV African Music Awards 2023.  

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ALIAHILISHA BUNGE LA BAJETI 2022

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisoma hotuba ya kuliahilisha bunge la bajeti  leo lililokuwa likikutana jijini Dodoma kwa zaidi ya miezi mitatu huku mawaziri na manaibu mawaziri wao wakijibu maswali ya wabunge waliokuwa na kiu ya kufahamu nilini watapelekewa mahitaji ya maendeleo majimboni kwao yakiwemo mahitaji ya , barabara, maji na huduma nyingine  ambazo zinatakiwa kupelekwa na Serikali. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, akijibu maswali ya wabunge leo Mbunge wa Musoma Davida Mathayo akiuliza swali Mbunge wa Ismani, William Lukuvi, akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa   Dkt. Stergomena Lawrence Tax ndani ya ukumbi wa bunge leo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasili bungeni huku akizungumza na wabunge na mawaziri tayari kwa kuliahilisha bunge Wanafunzi wa shule moja kutoka jijini Dodoma wakiwa bungeni Kwaya ya utumishi ikitamnbulishwa bungeni Spika Dkt. Tulia Ackson Mwanasasu, akimkalibisha Waziri Mkuu kusoma hotuba yake A Askari wa  Blasbendi wakipi

NMB YAWATAKA WENYE ULEMAVU KUJIAMINI

Image
 Afisa Mkuu wa Rasilimali watu benki ya NMB, Emmanuel Akonaay akiwasilisha mada kwenye mkutano mkuu wa Kitaifa wa Wafanyakazi wenye ulemavu nchini uliofanyika Jijini Dodoma. NMB ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa mkutano huo uliolenga kujadili upatikanaji wa stahiki bora haki ya kuajiriwa na mazingira rafiki ya kazi kwa watu wenye ulemavu.Na Mpigapicha Wetu Mwandishi Wetu Dodoma.Sababu kuu tatu zimetajwa kuwa changamoto ya kuwakosesha ajira watu wenye ulemavu nchini licha ya kuwa wanakuwa na sifa zinazotastahili. Sababu hizo zilitolewa jana Jijini Dodoma na Afisa Mkuu wa Rasilimali watu katika benki ya NMB Emmanuel Akonaay kwenye Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa wafanyakazi wenye ulemavu ulioitishwa na taasisi ya Ikupa Trust huku NMB wakiwa moja ya wadhamini. Akonaay alitoa kauli hiyo alipozungumza kwa niaba ya waajiri juu ya changamoto wanazokutana nazo wakati wa kuajiri kwani wenye ulemavu huwa wachache ingawa alisema ndani ya NMB wenye ulemavu wapo. Afisa Mkuu wa Rasilimali watu katika ben

CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WANAWAKE NCHINI CHAWAPIGA MSASA WABUNGE

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chjama cha Wafanyabiashara Wanawake nchini Mwajuma Hamza, akitoa maelezo kwa wanachama wa Chama cha Wabunge Wanawake nchini waliokutana katika ukumbi wa Msekwa jijini Dodoma. Mkutano huo ulifunguliwa na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na kuhudhuliwa pia na Baadhi ya wabunge wanaume wanaounga harakati za wabunge wanawake. Baadhi ya wajumbe wa wanachama wa wafanyabiashara wanawake SSpika Dkt, Tulia, akifungua mkutano huo Mjumbe Mbunge Injini Aisha Lulenge akichangia Wajumbe wakipiga picha ya pamoja baada ya kumalizika mkutano huo