Posts

Showing posts from January, 2017

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)

Image
KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –PRESS RELEASE HATIMAYE NJIA YA RELI KATI YA DAR ES SALAAM NA RUVU YAFUNGULIWA ! Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa kuanzia saa 9 alasiri   leo Januari 30, 2017 njia ya reli kati ya Kituo Kikuu cha   Dar es salaam na Ruvu imefunguliwa rasmi kwa shughuli za uendeshaji wa reli. Taarifa hiyo imesema kuwa kazi ya ufunguaji njia imewezekana baada ya Wahandisi na   Mafundi wa reli kuyaondoa Mabehewa yaliopata ajali l kutoka relini   na pia kuikarabati sehemu iliyo haribika . Kazi hiyo imefanyika kuanzia usiku wa Januari 29, 2017   hadi mchana wa Januari 30, 2017. Aidha treni ya abiria iliyoahirisha safari   ya kuondoka kwenda bara jana imeondoka leo   saa 9:05 alasiri kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam kwenda bara.. Wakati huo huo imefahamika kuwa msafiri mmoja aliyetambulikana kama Nd Basekena O. Bango kutoka Bujumb

MAJALIWA Azitaka zisiwe pango la wezi, wazembe

Image
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akihutubia leo wakati wa kufungua baraza la ushauri (RCC) Mkoa wa Dodoma ambapo lilishirikisha Wizara,Idara na Wadau mbalimbali wanaoratibu ujio wa Serikali kuhamia Makao makuu Dodoma Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma ( Picha na PMO) 30 JANUARI, 2017   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI HALMASHAURI ZIFANYE KAZI KWA WELEDI-MAJALIWA            * Azitaka zisiwe pango la wezi, wazembe WAZIRI MKUU Kassm Majaliwa amesema wakati umefika wa kuwa na watumishi wenye weledi wa kutosha kwenye Halmashauri zote nchini na pia hazitakiwi kuwa pango la wezi, wazembe au jalala la kutupa wabadhilifu walioshindikana kwingineko. Aidha, Waziri Mkuu amesemma Serikali za Mitaa na Halmashauri zote nchini zinatakiwa zianze kujitathmini na kujipanga vizuri zaidi kuona ni kwa namna gani zitakuwa chachu ya maendeleo ya viwanda vinavyotarajiwa. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 30, 20

WACHEZAJI YANGA WAKISHANGILIA MABAO YAO

Image
 Chirwa akishangilia baada ya kuifungia timu yake ya Yanga bao la Pili Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na mshumbuliaji wa timu hiyo Obrey Chirwa, dhidi ya Mwadui FC, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana.Picha na Joh Dande

UOKOAJI WA WALIOFUKIWA KWENYE MACHIMBO GEITA

Image
  Baadhi ya wachimbaji wadogo waliokuwa wamefukiwa katika mgodi wa RZ Union wakiwa hospitali ya Mkoa wa   Geita wakiendelea na matibabu baada ya kuokolewa jana. Picha na Lordrick Ngowi                                                                                                                                                                                          Ndugu wakiwakumbatia wachimbaji wadogo waliokuwa wamefukiwa katika mgodi wa RZ Union walipowatembelea hospitali ya Mkoa wa   Geita wakiendelea na matibabu baada ya kuokolewa jana. Baadhi ya wachimbaji wadogo waliokuwa wamefukiwa katika mgodi wa RZ Union wakiwailiana na jamaa zao kwa simu walipokuwa katika hospitali ya Mkoa wa   Geita wakiendelea na matibabu baada ya kuokolewa  Mmoja wa wachimbaji wadogo waliokuwa wamefukiwa katika mgodi wa RZ Union, Dicksoni Morris akiwasimulia ndugu na jamaa waliofika katika hopitali ya Mkoa wa Geita kuwajulia hali jana tabu walizozipata mgodini kwa s