Posts

Showing posts from October, 2014

UN WASHIRIKI BURUDANI TEMEKE

Image
KITUO CHA HABARI CHA UMOJA WA MATAIFA WASHIRIKI ALHAMISI YA BURUDANI  Afisa habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akitoa mada kuu iliyokuwa inahusu malengo ya maendelea ya milenia na kuangalia imefikia wapi kwenye malengo hayo pamoja na kuwaelimisha kuhusu maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015(Post 2015 Sustainable Development) iliyotolewa kwa Mtandao wa vijana wa Temeke. Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jana iliandaa Alhamisi ya Burudani kwa ajili ya kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Kwa kila Alhamis ya mwisho wa mwezi Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa huandaa burudani kwa makundi mbalimbali na kujifunza kazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa. Alhamisi ya mwezi wa kumi kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kilitembelea Mtandao wa Vijana wa temeke na kujadili mambo makuu ya malengo ya Milenia pamoja na kuangalia ni jinsi gani vijana wanashiriki katika shughuri za kimaendeleo katika jamii zao  Mkutubi - Kituo cha Habari cha U

BEN KIKO AFARIKI DUNIA

Image
ALIEKUWA MTANGAZAJI NA MWANDISHI WA HABARI RADIO TANZANIA SASA TBC BEN KIKO AFARIKI DUNIA Katibu wa Rais maswala ya Habari, Issa Michuzi kulia akiwa na mtangazaji wa siku nyingi, Beni Kiko wakifurahia jambo wakati wa uhai wake katika tuzo za mwandishi bora  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenela Mukangara kuomboleza kifo cha aliyekuwa Mtangazaji na Mwandishi Mkongwe na Mahiri hapa nchini wa iliyokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo kwa sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko. Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 31 Oktoba, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akiendelea na matibabu ya figo baada ya kuhamishiwa hapo akitokea Hospitali ya Jeshi ya Milambo Mkoani Tabora. “Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kuto

Jenerali Honore Traore mkuu wa jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza rais mpya wa nchi hiyo

Image
Jenerali Honore Traore mkuu wa jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza Rais mpya wa nchi hiyo Jenerali Honore Traore Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza Rais mpya wa nchi hiyo Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore sasa amejitangaza kuwa rais baada ya aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kutangaza kujiuzulu. Jenerali Traore ameshinikizwa na waandamanaji ambao walikuwa wanamtaka kuchukua usukani baada ya kuondoka kwa Bwana Compaore.  Compaore amesema kuwa amekubali kuondoka madarakani ili kutii matakwa ya waandamanaji ambao hawamtaki kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kutawala kwa miaka 27. Compaore sasa ametaka uchaguzi mpya wa urais ufanyike baada ya siku 90. Awali msemaji wa jeshi alikuwa amewaambia waandamanaji kuwa bwana Compaore hayuko tena madarakani huko Ouagadougou. Maelfu ya waandamanji walik

ANAYEUA KWA UPANGA NAYE HUUAWA KWA UPANGA

Image
Rais wa Burkina Faso ameng'olewa mamlakani Kuna hofu kuwa rais Compaore anataka kuendelea kushikilia madaraka Msemaji wa jeshi amewaambia waandishi wa habari mjini Ouagadougou kuwa bwana Compaore hayuko mamlakani tena. Rais Compaore alikuwa ametangaza kuwa atajiuzulu baada ya kipindi cha serikali ya mpito ya mwaka mmoja . Lakini wanasiasa wa upinzani wakakataa kata kat kuendelea kwa utawala wake na wakamtaka ajiuzulu maramoja. Rais Compaore alikuwa ameongoza kwa zaidi ya miaka 27 tayari. Kumeripotiwa maandamano mapya nchini Burkina Faso ya kutaka kujiuzulu mara moja kwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore. Viongozi wa upinzani wanakutana kwenye mkji mkuu  Ouagadougou kukubaliana kwa pamoja hatua watakazochukua. Siku ya Alhamisi waandanamaji walikarisishwa na jitihada za rais za kuongeza kipindi chake chake miaka 27 madarakani na wakatekete

Makinda 36 Plenary Assembly of the SADC Zimbabwe

Image
The Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda adoring the speech from the Guest of honor during the official opening of the 36 Plenary Assembly of the SADC Parliamentary Forum in Victoria Falls Zimbabwe today. With her is the Tanzania Higher Commissioner to Zimbabwe Hon. Adad Rajab and the SADC PF treasure Hon.  Seleman  Said Jaffo Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda keenly listening attentively to the Opening speeches during the official opening of the 36 Plenary Assembly of the SADC Parliamentary Forum in Victoria Falls Zimbabwe today. With her is the Tanzania Higher Commissioner to Zimbabwe Hon. Adad Rajab Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda listening attentively to the Opening speeches during the official opening of the 36 Plenary Assembly of the SADC Parliamentary Forum in Victoria Falls Zimbabwe today. With her is the Tanzania Higher Commissioner to Zimbabwe Hon. Adad Rajab   .      M