Posts

Showing posts from December, 2023

WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA ‘KUISAPOTI’ STARS AFCON 2023 – DKT. NDUMBARO

Image
  Na Brown Jonas – WUSM Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro ametoa rai kwa wadau wa Soka nchini kujitokeza kwa wingi katika kuiunga mkono timu ya Taifa ya mpira wa miguu Taifa stars inayojiandaa na Mashindano ya Afcon yatakayofanyika mapema mwezi Januari 2024 Nchini Ivory Coast. Mhe. Ndumbaro amesema hayo leo desemba 30, 2023 Jijini Dar Es Salaam kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo ameeleza umuhumi wa mashabiki katika kuiwezesha Stars kufanya vizuri. “Kwanza niwashukuru sana kwa siku za hivi karibuni hamasa imekua kubwa sana, sasa tunaomba hamasa iendelee hasa tunapoelekea mashindano ya Afcon tutumie mitandao ya kijamii kuisemea vizuri timu yetu ili kuipa hamasa” Aidha Mhe. Ndumbaro amesema kuwa Januari 30, 2024 wizara kwa kushirikiana na Shirikisho la soka nchini TFF itafanya harambee ya kuichangia Taifa Stars ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Ut

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AFUNGUA VIWANJA VYA MICHEZO VYA MATUMBAKU SPOTRS COMPLEX MIEMBENI WILAYA YA MJINI UNGUJA

Image
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kufungua Viwanja vya michezo vya Matumbaku Sports Complex Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 30-12-2023, ikiwa ni shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)udho. WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Hifadh ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Viwanja vya Matumbaku Spotrs Complex Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuufungua uwanja huo leo 30-12-2023 ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu) WAGENI waalikwa katika hafla ya ufunguzi wa viwanja vya michezo vya Matumbaku Spotrs Complex Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.

WITO WA KUTAMBUA MIILI YA MAREHEMU WALIOFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI NCHINI ZAMBIA

 TAARIFA KWA UMMA WITO WA KUTAMBUA MIILI YA MAREHEMU WALIOFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI NCHINI ZAMBIA Dodoma, 31 Desemba 2023.   Mamlaka za Jamhuri ya Zambia zilitoa taarifa kuhusu ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria aina ya Volvo la Kampuni ya Mukombe Luxury lenye namba za usajili DK72 HH GP linalofanya safari kati ya Afrika Kusini na Tanzania lililogongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T850 DSN la nchini Tanzania. Ajali hiyo iliyotokea katika Wilaya ya Serenje, Jimbo la Kati nchini Zambia tarehe 26 Desemba 2023, ilisababisha vifo vya watu 13 na majeruhi 42 wa mataifa mbalimbali, ikiwemo Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia, Afrika Kusini, Botswana na Zambia. Watanzania waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Bw. Oscar Mwamulima (37) mwenyeji wa Mbozi, Mbeya; Bw. Said Mohamed Dige (20) mwenye Hati ya Kusafiria Na. TAE403048, mzaliwa wa Ilemela, Mwanza; Bw. Peter Blass Munishi (48) mwenye Hati ya Kusafiria Na. TAE378465, mz

HOSPITALI YA MOUNT MERU YAPONGEZWA KWA UTOAJI WA HUDUMA BORA ZA AFYA

Image
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Ally Mwalimu (Mb), ameridhishwa na hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma za Afya, zinazotolewa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, na kuwapongeza Watumishi wote, kwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa, wanaofika hospitalini hapo kupata huduma. Mhe. Ummy, ametoa pongezi hizo, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua huduma za Afya, pamoja na kuzindua Maabara ya Patholojia inayohusika na upimaji wa magonjwa sugu ikiwemo Saratani hospitalini hapo. Mhe. Waziri, amekiri kuridhishwa na hali ya utoaji huduma za afya pamoja na shughuli za kitabibu zinazoendelea kutolewa katika mazingira safi na rafiki, hali inayosababisha kupanda hadhi hali ya utoaji bora wa huduma za Afya za wagonjwa. “Hospitali ya Mount Meru inafanya vizuri kati ya hospitali zote za Rufaa nchini, ninakupongeza Dkt. Alex na watumishi wote, niwasihi hospitali zote nchini kuiga mfano wa Hospitali ya Mount Meru, kuna vifaa vya kutosha, mazingira ni mas

NAIBU WAZIRI MKUU DKT. BITEKO AWASHUKURU WALIMU BUKOMBE KWA KUONGEZA UFAULU NA KUWAJALI WANAFUNZI

Image
  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye ni  Mbunge wa Jimbo la Bukombe, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kabuhima, Kata ya Uyovu wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ziara zake kwenye maeneo mbalimbali katika Jimbo la Bukombe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (kulia) ambaye ni  Mbunge wa Jimbo la Bukombe akiwa na Mkuu wa Geita, Martine Shigella wakizindua wodi mpya katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Charles Kulwa, iliyopo Runzewe wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita. Wananchi wa Kijiji cha Kabuhima, Kata ya Uyovu wilayani Bukombe mkoani Geita wakimsikiliza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye ni  Mbunge wa Jimbo la Bukombe, wakati akizungumza nao ikiwa ni sehemu ya ziara zake kwenye maeneo mbalimbali katika Jimbo la Bukombe. @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ *Akemea tabia ya kutopeleka watoto shule kwa kigezo cha kuwaozesha *Azindua wodi mpya katika Hospitali ya

POKEA SALAMU ZA MWAKA MPYA 2024 TOKA KWA MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI PROFESA SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO.

Image
 

NAIBU WAZIRI MKUU DKT. BITEKO. ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI KANISA KATOLIKI USHIROMBO

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akishiriki ibada katika Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Ushirombo inayofanyika wilayani Bukombe mkoani Geita leo Disemba 31, 2023.  

MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI IBADA YA KRISMASI DODOMA

Image
  SHARE Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Ibada ya Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma tarehe 25 Desemba 2023. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakizungumza na waumini mara baada ya kushiriki Ibada ya Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma tarehe 25 Desemba 2023. @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Sikukuu ya Krismasi leo tarehe 25 Desemba 2023. Ibada hiyo imeongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padre Emmanuel Mtambo

NAIBU WAZIRI PINDA JINBONI KWAKE KAVUU

Image
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda akizungumza na baadhi ya wananchi waliomtembelea nyumbani kwake Kibaoni katika jimbo la Kavuu tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mlele Wolfgun Pinda (Katikati) akiwa jimboni kwake tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi.                                                                               Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda (katikati) akizungumza na mmoja wa wananchi wa Kibaoni, Mlele wakati akiwa jimboni kwake tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mlele Wolfgun Pinda. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendele

VIKUNDI 8 VYANUFAIKA NA MFUKO WA JIMBO SONGEA

Image
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi mashine nane za kutotolesha vifaranga kwa vikundi nane vya jimbo hilo. Mhe. Ndumbaro amekabidhi mashine hizo Desemba 22, 2023 akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Ndg. Mwinyi Msolomi Pamoja na viongozi wengine wa chama hicho. Mashine hizo zimetolewa kupitia fedha za mfuko wa jimbo kwa lengo la kuwainua wananchi waliojumuika kupitia vikundi  vilivyosajliwa kisheria.  

WAZIRI SILAA ASIMAMISHA MATUMIZI YA KITUO CHA MAFUTA CHA BARREL DAR ES SALAAM

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akiozungumza na wananchi wa Mikocheni wakati akisimamisha matumizi ya Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni Desemba 23, 2023 jijini Dar es salaam. . Mwakilishi wa Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni Mhandisi Stanley Kitundu akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa (hayupo pichani) kwa niaba ya mmiliki wa kituo hicho ambacho kimesimamishwa kutoa huduma 23, 2023 jijini Dar es salaam   Na Eleuteri Mangi, WANMM   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesimamisha matumizi ya Kituo cha Mafuta cha Barrel Petrol Energy cha Mikocheni jijini Dar es salaam na kupiga marufuku ujenzi holela wa vituo vya mafuta nchi nzima vinavyojengwa kwenye makazi ya watu hatua inayohatarisha usalama wa watu na mali zao.   Waziri Silaa ametoa agizo hilo Desemba 23, 2023 alipoenda kukagua eneo kilipojengwa kituo hicho na aliambatana na