WITO WA KUTAMBUA MIILI YA MAREHEMU WALIOFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI NCHINI ZAMBIA

 TAARIFA KWA UMMA
WITO WA KUTAMBUA MIILI YA MAREHEMU WALIOFARIKI DUNIA
KATIKA AJALI YA BARABARANI NCHINI ZAMBIA
Dodoma, 31 Desemba 2023.

 

Mamlaka za Jamhuri ya Zambia zilitoa taarifa kuhusu ajali ya barabarani
iliyohusisha basi la abiria aina ya Volvo la Kampuni ya Mukombe Luxury
lenye namba za usajili DK72 HH GP linalofanya safari kati ya Afrika Kusini
na Tanzania lililogongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T850
DSN la nchini Tanzania.
Ajali hiyo iliyotokea katika Wilaya ya Serenje, Jimbo la Kati nchini Zambia
tarehe 26 Desemba 2023, ilisababisha vifo vya watu 13 na majeruhi 42 wa
mataifa mbalimbali, ikiwemo Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC), Ethiopia, Afrika Kusini, Botswana na Zambia.
Watanzania waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Bw. Oscar Mwamulima
(37) mwenyeji wa Mbozi, Mbeya; Bw. Said Mohamed Dige (20) mwenye
Hati ya Kusafiria Na. TAE403048, mzaliwa wa Ilemela, Mwanza; Bw. Peter
Blass Munishi (48) mwenye Hati ya Kusafiria Na. TAE378465, mzaliwa wa
Siha, Kilimanjaro; Bw. Bashiru Salum Kiluwa (42) aliyekuwa dereva
msaidizi wa Basi mwenye Hati ya Kusafiria Na. TAE173695, mzaliwa wa
Lushoto, Tanga; Bw. Rashid Athumani Salehe, Dereva wa Lori mkazi wa
Tanga; na Hassani Abdallah Ramadhani, Utingo wa Lori mwenye Hati ya
kusafiria Na. TAE667038 mkazi wa Muheza, Tanga.
Miili ya Marehemu hao imetambuliwa na ndugu zao isipokuwa
marehemu wawili, Bw. Said Mohamed Dige na Bw. Peter Blass Munishi.
Ndugu wa marehemu hawa wanahimizwa kufika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kutambua miili ya wapendwa wao.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikal

Comments

Popular posts from this blog

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.