Posts

Showing posts from December, 2022

SERIKALI KUMEGA HEKTA 33,132.24 ZA HIFADHI KUWAPATIA WANANCHI RUVUMA

Image
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza katika kikao baina ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Ruvuma tarehe 30 Desemba 2022. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza katika kikao baina ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Ruvuma tarehe 30 Desemba 2022. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas. Sehemu ya washiriki wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta na uongozi wa mkoa wa Ruvuma tarehe 30 Desemba 2022.  Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakiongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa tatu kulia) wakiondoka mkoani Ruvuma baada ya kumaliza kazi ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika mkoa huo 30 Desemba 2022. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

*SERIKALI YARIDHIA KUFUFUA MRADI MKUBWA WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDANI YA BONDE LA BUGWEMA*

Image
Picha zinaonesha Timu ya Wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakiwa ndani ya Bonde la Bugwema, Musoma Vijijini. Baadhi ya Viongozi wa Musoma Vijijini walishiriki kwenye ziara hiyo.  @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@  *Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikusudia kuanzisha kilimo kikubwa cha umwagiliaji ndani ya Bonde la Bugwema. Hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 70. *Bonde la Bugwena ni kubwa mno. Eneo lililokusudiwa kulimwa wakati huo ilikuwa ni ndani ya hekta 10,000. Bonde lenyewe likichukuliwa kwa ujumla wake lina ukubwa wa zaidi ya hekta 20,000. Miundombinu ya umwagiliaji ilijengwa miaka hiyo, lakini utekelezaji wake ukasimama! Mazao makuu yanayolimwa ndani ya Bonde hilo ni mahindi, mpunga, alizeti, dengu na pamba. *Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kuendeleza Mradi huo wa Bugwema. Ombi hilo lilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo wakati Mhe Rais wetu alipotembelea Muso

ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA TABORA ATAKIWA NA MAHAKAMA KULIPA FIDIA MILIONI 80

Image
  @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ Mahakama ya Mkoa wa Tabora imemtaka aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Elick Komanya Kitwala,  kulipa mdai wake Alex Ntonge kiasi cha  Shilingi million 80 kutokana na vitendo vya udhalilishaji. Akitoa hakimu wa makahakama ya mkua wa Tabora akitoa  hukumu hiyo leo Jovith Kato hukumu hiyo iliyoaanza majira ya saa 9.30 hadi saa 10 .34 alisema kwamba mahakama imuona mshitakiwa  kuwa na hatia baada ya kufanyia vitendo vya udhalilishaji. .

RAIS DKT.MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI KWENYE SWALA YA IJUMAA KATIKA MASJID AL SWAFAA

Image
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akisalimiana na Viongozi wa   Masjid AL Swafaa  Gongoni  Wilaya ya Mjini, Mkoa Mjini Magharibi  alipowasili na kushiriki katika     Swala ya Ijumaa na Waumini waliuofika katika Msikiti huo .[Picha na Ikulu] 30/12/2022. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiagana na Sheikh Omar Abdi Abdalla aliyetoa khutba ya Swala ya Ijumaa,  M asjid Al Swafaa uliopo   Gongoni  Wilaya ya Mjini   Mkoa Mjini Magharibi  mara baada ya  kujumuika na   Waumini mbali mbali  katika Swala ya Ijumaa  leo (katikati) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi. [Picha na Ikulu] 30/12/2022. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiagana na  Waumini mbali mbali na  Viongozi  mara baada ya  kujumuikanao    katika Swala ya Ijumaa   katika  M asjid Al Swafaa uliopo   Gongoni  Wilay

ASKARI POLISI MTWARA ATWAA BODABODA NMB MASTABATA

Image
***************** Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, WP Husna Juma Baraka, ameibuka mshindi wa pikipiki katika droo ya saba ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’ inayoendeshwa na Benki ya NMB, ambayo hadi sasa imeshatoa zawadi zenye thamani ya Sh. Milioni 138 kati ya zaidi ya Sh. Mil. 300 zinazoshindaniwa. NMB MastaBata Kote Kote ni kampeni inayohamasisha matumizi ya kadi za NMB Mastercard na Lipa Mkononi (kuscan QR), badala ya pesa taslimu, ambako droo hiyo ilisimamiwa na Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Irene Kawili na kufanyika katika Tawi la Bank House. Akizungumza kabla ya droo hiyo, iliyoambatana na makabidhiano ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya sita, Charles Shemsanga, Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Faraja Ng’ingo, alisema licha ya kuchagiza matumizi ya kadi, lakini pia wanaitumia MastaBata Kote Kote kuwazawadia wateja wao msimu huu wa sikukuu. Aliwataka wateja wa NMB kuendelea kufanya miamala m

WAZIRI BALOZI DKT. PINDI CHANA AHIMIZA UHIFADHI ENDELEVU.

Image
  ………………… Wananchi wametakiwa kuyaheshimu maeneo yaliyohifadhiwa kisheria hapa nchini na kuacha tabia ya kuvamia maeneo hayo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuyahifadhi na kuyalinda kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho. Kauli hiyo imetolewa mkoani Lindi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye ziara ya Kamati ya Mawaziri nane wa kisekta inayo shughulikia migogoro ya ardhi nchini na kutoa wito kwa Serikali za Vijiji na Kata ziendelee kutoa elimu Kwa wananchi juu ya umuhimu wa maeneo yaliyo hifadhiwa. Mhe. Balozi Dkt. Chana amesisitiza kuwa maeneo yaliyohifadhiwa yana umuhimu mkubwa katika uhai na uendelevu wa maisha ya binadamu hivyo yasipolindwa na kutunzwa ipasavyo madhara ni makubwa kwa kizazi kilichopo na kitakuwa hakijakitendea haki kizazi kijacho. Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameendea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa kwa wananchi kwa ku

WAZIRI MKUU: ANZISHENI MAJUKWAA YA KIUCHUMI

Image
  Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Afrika Kusini alipoutembelea Ubalozi huo ulioko jijini Pretoria, Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi na wa pili kulia ni Kaimu Balozi wa Afrika Kusini Balozi, Peter Shija (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Afrika Kusini alipoutembelea Ubalozi huo ulioko jijini  Pretoria  Ijumaa Desemba 30, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Afrika Kusini alipoutembelea Ubalozi huo ulioko jijini  Pretoria, Desemba 30, 2022. wa kwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Afrika Kusini Balozi, Peter Shija (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza viongozi na watumishi katika balozi waendelee kufanya tathmini ya fursa za kiuchumi ambazo Tanzania inaweza

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ DK.HUSSEIN MWINYI AJUMUIKA KATIKA KISOMO CHA DUA NA HITMA KUMUOMBEA MAREHEMU SALIM AHMED BAKHRESSA MSIKITI WA MCHANGANI UNGUJA

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Wanafamilia ya Bakhressa katika kisomo cha hitma na dua ya kumuombea Marehemu Salim Ahmed Salim Bakhressa, iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Mchangani Wilaya ya Mjini Unguja na (kulia kwa Rais) Said Salim Bakhressa na Baba Mzazi wa Marehemu Ahmed Salim Bakhressa na (kushoto kwa Rais) Sheikh Mohammed Omar Al Sheikh.(Picha na Ikulu)  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa pole kwa Baba Mzazi wa Marehemu Salim Ahmed Bakhressa, Bw. Ahmed Salim Bakhressa na Said Salim Bakhressa, baada ya kumalizika kwa kisoma cha Dua na Hitma, ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Mchangani Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)  

Mambo 5 usiyoyajua kuhusu Pele, mfalme wa soka

Image
  Chanzo cha picha, KEYSTONE Saa 5 zilizopita Kuna mijadala mingi kuhusu nani mwanasoka bora wa wakati wote: Maradona, Messi, Ronaldo, Cruyff... Lakini hakuna anayepinga mfalme ni nani: Edson Arantes do Nascimento, Pele. Nyota huyo wa Brazil, aliyefariki Alhamisi hii, Desemba 29 akiwa na umri wa miaka 82, alizaliwa Tres Corazones, mji ulioko takriban kilomita 200 mashariki mwa Sao Paulo, Brazil, Oktoba 23, 1940. Katika maisha yake ya kina kama mchezaji wa soka, Pelé alivunja rekodi zote, licha ya ukweli kwamba hizo zilikuwa nyakati ambapo wachezaji wa soka walipimwa zaidi na upeo wa vipaji vyao kuliko rekodi ya idadi yao. Amedai zaidi ya mabao 1,200 -1,283 kuwa sawa- lakini FIFA inampatia mabao 757. Iwe hivyo, ndiye mfungaji bora wa timu ya Brazil na ana idadi kubwa zaidi ya hat-trick katika historia: 92. Pia alikuwa mchezaji mdogo zaidi kushinda Kombe la Dunia, akiwa na umri wa miaka 17 pekee. Na mwanasoka pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu: Sweden 1958, Chile 19

Pele: Nyota wa soka wa Brazil afariki akiwa na umri wa miaka 82

Image
  Chanzo cha picha, Getty Images 29 Disemba 2022 Gwiji wa soka wa Brazil Pele, ambaye bila shaka ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82. Anasifiwa kwa kufunga mabao 1,281 katika rekodi ya dunia katika mechi 1,363 katika kipindi cha miaka 21 ya maisha yake, yakiwemo mabao 77 katika mechi 92 za nchi yake. Mchezaji pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, akinyakua taji hilo mnamo 1958, 1962 na 1970, Pele alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Karne wa Fifa mnamo 2000. Alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo na kibofu katika miaka ya hivi karibuni. Pele alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye utumbo wake mnamo Septemba 2021 katika Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo, baada ya uvimbe huo kugunduliwa katika vipimo vya kawaida. Alirejeshwa hospitalini mwishoni mwa Novemba 2022. Binti yake Kely Nascimento amewafahamisha mashabiki kuhusu hali ya babake kwa taarifa za mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii kutoka hospital

MADEREVA WANAOENDESHA VYOMBO VYA MOTO WAKIWA WAMELEWA WAPEWA ONYO

Image
  Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi , ARUSHA Madereva wanaotumia vyombo vya moto wakiwa wamelewa katika Mkoa wa Arusha wamepewa angalizo endapo watabainika kuendesha magari hayo wakiwa wamelewa. Hayo yamesemwa na Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO wakati akizumgumza na Madereva wa mabasi mapema leo decemba 30.2022 katika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani na Nchi jirani. Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye bainika anaviashiria vya pombe atashugulikiwawa kwa mujibu wa sheria ambapo amewataka madereva wa magari hayo kutotumia vyombo hivyo wakiwa wameleva. Ameongeza kuwa kikosi hicho hakimkatazi mtu yeyote kutumia pombe ambapo amewataka madereva kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka mkono wa dola.  SP Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye kamatwa kwa makosa hayo atafungiwa leseni yake na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kuhatarisha Maisha ya watu na uharibifu wa miundo m

MARUFUKU WANANCHI WA VIJIJJ 11 KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU MAENEO YA HIFADHI -DKT MABULA

Image
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mtepera wilayani Kilwa mkoa wa Lindi wakati Kamati ya Mawaziri wa Wizara ya Kisekta walipotembelea kijiji hicho Desemba 29, 2022. Wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack. Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Mtepera wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi (hayupo pichani) wakati Kamati ya Mawaziri wa Wizara ya Kisekta walipotembelea kijiji hicho Desemba 29, 2022 kwa ajili ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi. Naibu Waziri wa Maji Meryprisca Mahundi akizungumza na katika Kijiji cha Mtepera wilayani Kilwa mkoa wa Lindi wakati Kamati ya Mawaziri wa Wizara ya Kisekta ilipotembelea kijiji hicho  Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde akizungumza wakati Kamati ya Mawaziri nane wa Wizara za Kisekta ilipotembelea Kijiji cha Mtepera wilayani Kilwa mkoa wa Lindi  Naibu Wazir