*SERIKALI YARIDHIA KUFUFUA MRADI MKUBWA WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDANI YA BONDE LA BUGWEMA*

Picha zinaonesha Timu ya Wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakiwa ndani ya Bonde la Bugwema, Musoma Vijijini. Baadhi ya Viongozi wa Musoma Vijijini walishiriki kwenye ziara hiyo.


 @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

 *Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikusudia kuanzisha kilimo kikubwa cha umwagiliaji ndani ya Bonde la Bugwema. Hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 70.

*Bonde la Bugwena ni kubwa mno. Eneo lililokusudiwa kulimwa wakati huo ilikuwa ni ndani ya hekta 10,000. Bonde lenyewe likichukuliwa kwa ujumla wake lina ukubwa wa zaidi ya hekta 20,000.

Miundombinu ya umwagiliaji ilijengwa miaka hiyo, lakini utekelezaji wake ukasimama!

Mazao makuu yanayolimwa ndani ya Bonde hilo ni mahindi, mpunga, alizeti, dengu na pamba.

*Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kuendeleza Mradi huo wa Bugwema.

Ombi hilo lilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo wakati Mhe Rais wetu alipotembelea Musoma Vijijini akizindua Mradi wa ujenzi wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama. Hii ilikuwa tarehe 6 Februari 2022.

Mbunge huyo alirudia kutoa ombi hilo kwenye Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Dodoma, tarehe 7-8.12.2022

*Jana, Alhamisi, 29.12.2022, Timu ya Wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ilitembelea Bonde la Bugwema. Timu hiyo iliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dr Raymond Mndolwa.

Viongozi kadhaa wa Musoma Vijijini waliambatana na Timu hiyo ya Wataalamu. Baadhi yao ni:

*Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
*Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Bugwema, Ndugu Ezekiel MacGudo
*Diwani wa Kata ya Bugwema, Mhe Clliford Machumu
*Mtendaji wa Kata ya Bugwema, Ndugu Josephat Phinias

*Taarifa iliyotolewa* na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ni kwamba matayarisho ya utekelezaji wa Mradi wa Bugwema yanaendelea vizuri  kwa ajili ya kuanza kufanya *"feasibility studies and designs*

Musoma Vijijini wanaendelea kutoa shukrani nyingi sana kwa Rais wetu, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuendeleza Mradi wa Kilimo kikubwa cha Umwagiliaji ndani ya Bonde la Bugwema.

Upatikanaji wa chakula kingi cha bei nafuu kunasaidia kushusha mfumuko wa bei kwenye soko la chakula!

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.