WAZIRI BALOZI DKT. PINDI CHANA AHIMIZA UHIFADHI ENDELEVU.

 

…………………

Wananchi wametakiwa kuyaheshimu maeneo yaliyohifadhiwa kisheria hapa nchini na kuacha tabia ya kuvamia maeneo hayo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuyahifadhi na kuyalinda kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Lindi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye ziara ya Kamati ya Mawaziri nane wa kisekta inayo shughulikia migogoro ya ardhi nchini na kutoa wito kwa Serikali za Vijiji na Kata ziendelee kutoa elimu Kwa wananchi juu ya umuhimu wa maeneo yaliyo hifadhiwa.

Mhe. Balozi Dkt. Chana amesisitiza kuwa maeneo yaliyohifadhiwa yana umuhimu mkubwa katika uhai na uendelevu wa maisha ya binadamu hivyo yasipolindwa na kutunzwa ipasavyo madhara ni makubwa kwa kizazi kilichopo na kitakuwa hakijakitendea haki kizazi kijacho.

Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameendea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa kwa wananchi kwa kuridhia wapewe sehemu za baadhi ya maeneo ya hifadhi ili wayatumie kwa shughuli za kijamii huku akiwataka wasivamie maeneo mengine yaliyohifadhiwa

“Maeneo haya yanategemewa na Watanzania wote katika kutupatia mvua, hewa safi, ajira, maji ya Kilimo, umeme kwa matumizi ya nyumbani. Natoa rai kwa wananchi wote muhakikishe mnayalinda maeneo haya, msiyavamie na kuingiza mifugo wala Kuchoma moto” Amesisitiza Waziri Balozi Dkt. Chana

Amewapongeza Wakuu wa Mikoa kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha Uhifadhi huku akiwaomba waendelee kusimamia maeneo hayo kwa maslahi mapana ya Taifa

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.