WABUNGE NA WAFANYAKAZI WA BUNGE WAONYESHANA UBABE KATIKA BUNGE BONAZA

Waziri Mkuu akiwa Sambamba na Spika Dkt. Tulia Ackson, wakifanya  mazoezi mepesi baada ya kuongoza matembezi ya kilomita 2.5 yaliyojulikana kwa jina la  Bunge Bonanza  yaliyoambatana na michezo mbalimbali na washindi kupatiwa vikombe na medali


Wafanykazi wa bunge nao wakifanya mazoezi

Wabunge nao wakichapa zoezi




Wakishindana kwa kukimbia



Wakishindana kwa kucheza karata

Naibu Spika Zungu wakichuana mchezo wa bao na William Lukuvi

Waziri Mkuu akikagua timu kwa ajili ya Bonanza




Timu ya Wagunge
Timu ya Wafanyakazi wa Bunge
Wachezaji wa Mpira wa kikapu wakichuana




Mbunge Mtatulu, akihamasisha timu yake iwaburute  wafanyakazi, walibeba kombe baada ya kiwashinda
Mfanyakazi wa Bunge Kizingiti, akishangaa baada ya Timu yake kushindwa






Wabunge wanawake wakichuana na wafanyakazi wa Bunge wanawake kwa mchezo wa kuvuta kamba






Siyo wacheza sumo  wa Kijapani ni wabunge wakiwa tayari kuvuta kamba




Mfanyakazi Kizingiti, akiihamasisha timu yake ishinde hata hivyo ilishindwa kwa awamu  ya pili  baada ya kwanza walishinda




Waziri Mkuu akishuhuhudia mchezo wa kaba
Mbunge Kigwangala, akitafuta jinsi ya kuwapita wachezaji  wafanyakazi wa bunge
Vita Kawawa akiwa na mpira








Mchezo wa bao

Mchuano wa mchezo wa karata
Mchuano wa mpira wa miguu Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete, akimramba chenga stafu wa bunge
Stafu wakishuhudia mashindano
 Mchuano wa kukimbia kwa magunia

Mchuano  wa kukimbiza kuku



Mbunge Hawa Mchafu Chakoma, akiwa na kuku baada ya kumkamata

Vikombe na medali walizokabidhiwa washindi

Sahani za Ubwabwa na Maharage ukisubili walaji katika mchezo wake
Wakishindana kula ubwabwa


Waziri Mkuu akitoa hotuba yake kabla ya kutoa zawadi
Nahodha Mtaturu, akipokea  kikombe cha timu ya wavuta kamba
Nahodha Kigwangala,akipoke akikombe cha Timu ya mpira wa kikapu
Mchezaji wa timu ya bunge ya mpira wa miguu akichukua kikombe cha ushimdi baada ya kuwasasambua wqabunge kwa bao 4-1

Mbunge Sanga akipokea kikombe kwa washindi wa jumla ambao ni wabunge



Mbunge Swale, akiwa na kikombe
 @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@

 

WAZIRI MKUU AWASISITIZA WABUNGE WASHIRIKI MICHEZO

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Jumamosi, Januari 28, 2023 ameshiriki Bunge Bonanza lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi na sekondari ya John Merlin ya jijini Dodoma ambapo ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wabunge na wananchi wengine washiriki katika michezo ili kuipa miili yao nguvu na uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kikazi.

“…Michezo kwetu sisi wabunge ni muhimu zaidi kwa sababu inatufanya tuwe na afya bora zaidi na pia michezo inasaidia watu kukutana pamoja na kuimarisha undugu, kujenga urafiki pamoja na kukuza vipaji. Nampongeza Mheshimiwa Spika Dkt. Tulia Ackson kwa ubunifu huu wa kuanzisha Bunge Bonanza ambalo litakuwa linafanyika mara kwa mara.”

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na wabunge, baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Watumishi wa Bunge pamoja na maafisa wengine wa Serikali walio shiriki katika bonanza hilo. Amesema bonanza lingine kama hilo linatarajiwa kufanyika Juni 24, 2023.

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia amesema Bunge Bonanza litakuwa linafanyika mara nne kwa mwaka lengo likiwa ni kuhamasisha wananchi umuhimu wa kushiriki katika kufanya mazoezi ili jamii iweze kuwa na afya bora zaidi.

Naye, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Katibu wa Michezo wa Baraza hilo Mheshimiwa Nassor Salim Ali (Jazeera) ambaye amemuwakilisha Spika wa Baraza la Wawakilishi amesema baraza litaendelea kushirikiana na Bunge ili kudumisha undugu kupitia michezo pamoja na shughuli mbalimbali wanazozifanya. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kudumisha Muungano.”

Awali, Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Mheshimiwa Festo Sanga alisema pamoja na mambo mengine bonanza hilo limeanzishwa ili kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ambaye amekuwa akiihamasisha jamii kushiriki katika kufanya mazoezi kwa ajili ya kuupa mwili afya na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.

Timu zilizoshiriki katika bonanza hilo ni timu ya Bunge na ya watumishi wa Bunge ambapo timu ya Bunge ilipata kombe la mshindi wa jumla baada ya kuishinda timu ya Watumishi wa Bunge katika michezo mingi. Michezo ni pamoja na mpira wa miguu, mpita wa wavu, mpita wa meza, mpira wa mikono, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kula chakula, kunywa soda, kuvuta kamba na kurusha tufe.


Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.