UHAMIAJI WAFANYA USAFI NA KUTOA ZAWADI KWA WATOTO HOSPITALI YA TEMEKE


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt Anna Peter Makalala ametoa zawadi kwa akina mama na watoto waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Temeke sambamba na kufanya usafi wa mazingira kuzunguka eneo hilo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jhn Pombe Magufuli la kufanya usafi kila mwisho wa mwezi.
Kamishna Jenerali Anna alimkabidhi kijarida chenye masuala mbalimbali yanayohusu uhamiaji kwa mganga mkuu wa hospitali ya Temeke na kumtaka kushirikiana nao kwenye kutoa elimu kwa wagonjwa wanaofika hapo pale pindi wapatapo muda.

Mganga Mkuu wa hospitali ya Temeke Dr Amani Malima  amewashukuru sana kwa kuja kufanya usafi kwenye hospitali hiyo na kutoa zawadi kwa wakina mama na watoto huku akiwahakikishia kuwa watatoa elimu kwa wagonjwa wanaofika hapo kuhusiana na masuala ya uhamiaji.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akifanya usafi katika Hosptali ya Temeke ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli ya kufanya usafi kila mwisho wa mwezi, usafi huo umefanyika kwa pamoja na wafanyakazi wa Uhamiaji Dar es Salaam Oktoba 28, 2017.

 

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala pamoja na Mkuu wa Wilaya ya emeke Felix Lyaviva wakifanya usafi katika Hosptali ya Temeke ikiwa ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli ya kufanya usafi kila mwisho wa mwezi, usafi huo umefanyika kwa pamoja na wafanyakazi wa Uhamiaji Dar es Salaam Oktoba 28, 2017.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akijadiliana jambo na mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaviva baada ya kuwasili katika Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli.

Kamishna Jeenerali akitoa zawadi ya pampers na sabuni kwa wakina mama waliojifungua watoto walio chini ya muda wake (njiti) walipowatembelea kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala akitoa zawadi kwa wakina mama walipowatembelea kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala  akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kufanya usafi katika hospitali ya Temeke sambamba na kutoa zawadi kwa watoto na wakina mama waliokuwa wamelazwa kwenye hospitali hiyo, hilo ni katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli ya kufanya usafi kila mwisho wa mwezi. Kushoto ni Mganga mKuu wa Hospitali ya Temeke Dr Amani Malima.
Kamishna Jenarali wa Uhamiaji Dkt Anna Peter Makakala akimkabishi jarida la Uhamiaji navifaa vya usafi kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Dr Amani Malima  ikiwa ni siku ya usafi wa kila mwisho katika kutilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mafuguli,  usafi huo umefanyika kwa pamoja na wafanyakazi wa Uhamiaji
Kamishna Jenarali wa Uhamiaji Dkt Anna Peter Makakala akisaini katika kitabu cha wageni.

Kamishna Jenarali wa Uhamiaji Dkt Anna Peter Makakala akijadiliana jambo na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Dr Amani Malima pamoja na kufurahi pamoja baada ya kumaliza kufanya usafi,

Wafanyakazi wa uhamiaji wakiwa wanafanya usafi.
Kamishna Jenarali wa Uhamiaji Dkt Anna Peter Makakala na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Dr Amani Malima wakiwa wanaelekea katika wodi za kina mama na watoto baada ya kumalizika kwa usafi.
Kamishna wa Uhamiaji- Pasi na Uraia, Gerald Kihinga akitoa zawadi kwa watoto waliolazwa kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Kamishna wa Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Samwel Magweiga kitoa zawadi kwa watoto waliolazwa kwenye Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Kamishna wa Sheria Hanerole Manyanga akitoa pole na zawadi kwa mama aliyetoka kujifugua walipotembelea  Hospitali ya Temeke walipokwenda kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.Picha zote na Zainab Nyamka.

NELLY KAZIKAZI ATWAA TAJI LA MISS HIGHER LEARNING 2017

 Miss Higher  Learning 2017, Nelly Kazikazi, akipunga mkono kwa furaha akiwa na washindi wenzake baada ya kutangazwa rasmi na kuvishwa Taji katika shindano la Miss Vyuo Vikuu lililofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye Ukumbi wa King Solomon Namanga Dar es Salaam. Kulia ni mshindi wa pili, Queen Elizabeth Makune (kushoto) ni mshindi wa tatu,  Melody Thomas. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Shindano hilo pia lilipambwa na burudani kutoka kwa wasanii tofauti kama JK Comedian Jukwaani, Msaga sumu na Barnaba Boy.
 Sehemu ya wageni waliofika kushuhudia shindano hilo wakiwa katika meza za VIP
 Shoo ilianza kama hivi kwa kufungua na shoo ya pamoja
 Hatimaye warembo walianza kupita jukwaani na vazi la ubunifu....
 
 
 
 
 Msaga Sumu akitoa burdani
 Hatimaye Warembo walianza kupita jukwaani wakia na vazi la Ufukweni

 Majaji wakijadiliana jambo
 Dj John Dilinga naye akionyesha shoo, kuigiza umiss

 Miss Talent akinyesha jinsi alivyochukua taji hilo.
 Hatimaye ukafika muda wa Warembo kupita jukwaani na vazi la usiku.
 Ulifika muda wa Barnaba Boy kuwarusha wadau wa urembo ukumbini hapo
 Dj Denso kutoka Mafoto City Sound akiwarusha kwa ngoma za Barnaba alipopanda jukwaani
 Huku ni nyumba ya Stage warembo wakishoo love
 Barnaba Boy akiwachezesha warembo kwa ngoma zake
 Warembo wakiwa nyuma ya stage nao wakifuatilia shoo ya Barnaba Boy
 Hawa ndiyo warembo wote walioshiriki shindano hilo
 Mkurugenzi na mratibu wa shindano hilo, Joseph Musendo akizungumza jukwaani, akiwa na msaidizi wake
 Ilipoanza kutangazwa tatu bora
 Miss Highlearning 2016, Laura Kway, akimvisha Taji Miss Highlearning 2017, Nelly Kazikazi, baada ya kutangazwa mshindi.
Miss Higher Learning 2017, Nelly Kazikazi, akipunga mkono kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi.

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.