CWT GOGOLO LAKE KUMBE KUZUIA KUPIGWA BILIONI 16. RAMANI YA JENGO MILIONI 415 MAWAZIRI WATANO WAHUSISHWA

Rais wa Chama cha Walimu Nchini (CWT), Komredi Leah Ulaya, akifungua kikao cha Kamati kuu ya chama hicho cha Dharula kilichofanyikia Makao Makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Japhet Maganga na Kulia ni Makamu Rais wa Chama hicho Suleimani Ikombe

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
 

CWT GOGOLO LAKE KUMBE KUZUIA KUPIGWA BILIONI 16.

RAMANI YA JENGO MILIONI 415

MAWAZIRI WATANO WAHUSISHWA

Hatimaye imebainika kwamba Songombingo inayoendelea  katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Makao Makuu ni uzuiaji wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya chama hicho  ulioidhinishwa na uongozi uliopita.

Ujenzi wa jengo hilo ulikuwa ufanyike jijini Dodoma, wajumbe wa  baraza Kuu la Chama hicho waliingizwa chaka baada ya kutakiwa kuidhinisha ujenzi huo bila kuambiwa utagalimu kiasi gani.

bila kufahamu kiasi gani kitatumika katika ujenzi wa jengo hilo Viongozi wao walitumia mwanya huo na  kuingia mkataba wa ujenzi wa jengo  la golofa tatu ambalo lingetumia kiasi cha sh Bilioni 16.

Kwa mujibu wa baadhi ya wajumbe hao ni kwamba ramani ya jengo ambalo lilitakiwa kujengwa  galama yake ni kiasi cha shilingi  milioni 415, aidha baadhi ya wajumbe wa Baraza kuu walikuwa wapewe katika mgao huo kila mjumbe Sh Milioni 100 endapo isingegundulika.

Ikumbukwe kwamba wajumbe wa Baraza kuu la chama hicho wapo 200 lakini katika mgao huo  ilikuwa wapate nusu yao baada ya wengine kugundua hawamo katika mgao huo ndipo siri zikaanza kuvuja na kufikia hatua ya kutimuliwa katika chama hicho.

Kutokana na taarifa hiyo hatimaye siri imefichuka leo katika vulumai la kutaka kuvunjwa mkutano ambao ulitakiwa kufanyika ndipo jeshi la polisi walifika katika mkutano huo na kuzuia  bila busra za Rais wa Chama hicho Leah Ulaya huenda hata umwagaji damu ungetokea.

Wajumbe wa Baraza Kuu la Chama hicho walipoanza kuingia  eneo la Kikao  Ofisi za Chama hicho zilizopo mtaa wa Jamhuri na kukuta polisi wenye silaha wakiwa wamefunga lango la kuingilia na  kuwataka waliomo ndani wabaki huko wale wa nje wasiingie.


Askari zaidi ya 12  walikuwa wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Kituo cha Polisi Dodoma Joram Samson huku polisi watano wakiwa na silaha za moto walifika kwa ajili ya kuzuia mkutano huo usifanyika

"Tumepokea maagizo ya mdomo kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu kwamba kikao hiki mnachotaka kukifanya kisifanyike tunaomba muondoke eneo hili", alisema kamanda huyo.


Kutokana na kauli hiyo ya jeshi la polisi  ndipo ukazuka  mvutano mkali baina ya Askari polisi na wanachama wa Chama hicho kuanza kurushiana maneno makali kati ya polisi na kusababisha baadhi ya walimu kukamatwa wakidaiwa kutoa lugha za matusi kwa askari hao.

Awali Baraza hilo lilikuwa lifanyike ukumbi wa St Gasper lakini ghafla baada ya kugundulika kwamba wanafuatiliwa wakaamua wafanyie ofisini kwao pamoja na kwamba walikuwa wameshalipia ukumbi huo huku wakidai kuwa endapo mkutano huo  ungefanyika katika ukumbu wa St.Gasper wangezuia  barabara kuu  ya Dodoma-  Morogoro  wangeifunga hadi  muafaka wa sakata hilo upatikane.Ikumbukwe barabara hiyo ndiyo ya kuingilia jijini Dodoma kutoka Morogoro.
 
Baadhi ya maneno yaliyosikika kutoka kwa wajumbe hao walikuawa wakisema kwamba amri kutoka ngazi za juu ni baadhi ya mawaziri ambao walikuwa katika mikono ya viongozi waliopita walikuwa wakipata mgao wa kila mwezi kutoka kwa viongozi waliopita sasa kisima chao kimekauka baada ya kuondoshwa ndio maana wanachochea mgogoro huo.

Kutoka  na kauli ya wajumbe hao baadhi yao wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutumia vyombo vyake ili kupata uhakika wa mawaziri wake wanaokisumbua chama chao aanzie na yule aliyemshauri kuwateua  viongozi wa chama hicho kuwa wakuu wa wilaya huku wakifahamu ni viongozi wa ngazi za juu wa chama chao.

"Hiyo ilikuwa janja ili waondoke waachie zipigwe fedha zao hizo bilioni 15
na ndiyo maana kila mara kundi hilo likitumia vyombo vya habari wakianzia na kuandika wale waliokaidi uteuzi wa Rais".ni maneno ya wajumbe wa CWT.

"Ndiyo maana Rais anabadilisha kila mara mawaziri hao baadhi yao ni wala rushwa ndiyo maana walishawahi kuitwa mizigo baadhi yao huko nyuma wanapeleka mizozo katika taasisi ili wanufaike wao na watu wao. Tutamlinda katibu wetu hata kumshauri atoe notsi ya kuacha kazi huko katika kituo chake ", walidai walimu hao.

Hata hilo Tangazo na kumtaka arejee kazini kwake wanalitilia shaka huenda ni la magumashi wakidai kwa hasira walimu hao wanaowawakilisha wanachama wao zaidi ya laki mbili nchi nzima.
Kwanini mkutano wa leo ulikuwa unazuiwa usifanyike, kwa sababu walishapata taarifa kwamba leo ndiyo kikao kilikuwa kinakutana kusitisha mkataba wa ujenzi wa jengo hilo la Bilioni 15. wameamua wajumbe bora wajenge jengo dogo lenye kutumia fadha kidogo kuliko fedha nyingi hizo za wanachama.

Aidha kwa kipindi kifupi cha viongozi hao wameweza kulipa walimu wastaafu zaidi ya 200 kwa kila mmoja zaidi ya Sh laki 4 achiliambali kutoa pole ya fedha taslimu  kwa wanaofariki wakiwa kazini kwa wanachama wao.



Wajumbe wa Kikao hico  wakisikiliza viongozi wao wakiendesha mkutano


 

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.