Skip to main content

UCSAF KUENDELEZA JITIHADA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO VIJIJINI. MASHIBA

 



MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa Huduma ya Mawasiliano Vijijini unaendelea ambapo Mfuko huo umesaini mkataba wa kupeleka huduma za Mawasiliano katika kata zaidi ya 1900 na mradi huo umefikia asilimia 90 katika utekelezaji wake.

Ameyasema hayo wakati akielezea utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya UCSAF na kazi ambayo wameifanya ya kuboresha mawasiliano pamoja na kupeleka vifaa vya TEHAMA katika kijiji cha Msomera Mkoani Tanga.

Ambapo amesema kuwa jukumu walilokasimiwa na serikali la kuhakikisha wanapeleka mawasiliano vijijini wanalitekeleleza vyema ambapo mpaka sasa kazi kubwa imefanyika ya ujenzi wa minara vijijini na lengo likiwa ni kuhakikisha vijiji vyote vinapata huduma ya mawasiliano ili kuchochea maendeleo kupitia uchumi wa kidijitali.

Tutakapokamilisha ujenzi wa miradi hiyo ya mawasiliano wananchi wapatao milioni 15 watapata huduma za mawasiliano na hii ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote na serikali ya Awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan na watoa huduma wengine wa mawasiliano nchini kwa namna wanavyopambana kuhakikisha huduma hizo zinawafikia Watanzania wote,”amesema Mashiba

Akielezea utekelezaji wa miradi katika eneo la Msomera Mashiba ameeleza kuwa ,UCSAF inatekeleza miradi mitatu ambopo imejenga mnara wa Mawasiliano katika kijiji cha Msomera kwa kushirikiana na TTCL na Kwa sasa eneo hilo huduma ya mawasiliano inapatikana kwa uhakika kwa mitandao yote .

"Pia kuna wanachi wengine kutoka Ngorongoro wanatarajiwa kuhamia Msomera na Ujenzi wa nyumba takribani 5000 unaendelea huko ila ni katika kijiji cha Mkababu na huko hapakuwa na Watanzania wanaoishi hivyo huduma ya mawasiliano hazipatikani kwa hivyo kwa kushirikiana na TTCL tunajenga Mnara wa Mawasiliano huko ambako mpaka ninavyozungumza ujenzi wa mnara huo unaendelea ili wananchi wale watakapo hamia wasipate shida ya mawasiliano", alisema Mkurugenzi

Mashiba

 

Jitihada kubwa ni kuwalithisha matumizi ya mawasiliano vijana wadogo hususan wanafunzi kama hawa ili taifa liwe na wajuzi wa Teknolojia




Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.