WANANCHI WA KISIWA CHA RUKUBA WAFURAHIA KUANZA KUPOKEA VIFAA TIBA VYA KITUO CHAO CHA AFYA

Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijni Profesa, Sospeter Muhongo, wamempongeza wananchi wa jimbo hilo kwa juhudi zake za kuwaletea maendeleo
 

Kisiwa cha Rukuba kimekamilisha ujenzi wa Kituo chake cha Afya na tayari kimeanza kupokea vifaa tiba vya Kituo hicho.

Utoaji wa Huduma za Afya ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini unaendelea kuboreshwa na kuimarika. Kwa sasa tuna:

(i) Hospitali ya Halmashauri
Hii ina hadhi ya Hospitali ya Wilaya

(ii) Vituo vya Afya sita (6)
Murangi, Mugango, Bugwema, Makojo, Kiriba na  Kisiwa cha Rukuba

(iii) Zahanati 42
*24 za Serikali
*4 za Binafsi
*14 zinajengwa

Maombi yaliyopelekwa Serikalini
*Wafanyakazi wa kutoa Huduma mbalimbali za Afya wapo wachache sana. Idadi iongezeke sana.

Tunaomba idadi iongezeke hasa kwenye Hospitali yetu mpya na kwenye Vituo vyote vya Afya.

*Vifaa tiba vinahitajika, ni pungufu sana.

*Wingi wa dawa za aina mbalimbali uongezeke sana.

Furaha & Shukrani
Tafadhali sikiliza  CLIP/VIDEO ya kutoka Kisiwani Rukuba iliyoambatanishwa hapa

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 28.9.2023

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.