TFS WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO NA MSHIKAMANO SEHEMU ZA KAZI.

 

Mhifadhi Mkuu shamba la Wino  Glory Kasmir kushoto akiwa  na aliyekuwa mfanyakazi wa shamba hilo Theofrida Luoga wakati wa sherehe ya  kumuaga iliyofanyika jana  katika ukumbi wa Chandamali Resort unaomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania Brigedi ya 401 Songea. Kaimu Afisa utumishi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania kanda ya kusini Anderson Besisila akizungumza katika sherehe ya kumuaga aliyekuwa mfanyakazi wa shamba la miti Wino wilayani Songea Theofrida Luoga,kulia meneja wa TFS wilayani Songea Issa Mlela. Mhifadhi Mkuu shamba la miti Wino linalomilikiwa  na wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS) Glory Kasmir kushoto akimlisha keki ya upendo aliyekuwa mfanyakazi wa Shamba la miti Wino Theofrida Luoga ambaye amestaafu utumishi wa umma.


WAFANYAKAZI wa wakala wa huduma za misitu Tanzania(TFS),wameaswa kufanyakazi kwa upendo,mshikamano na kutanguliza uzalendo kwa nchi yao ili kuongeza ufanisi  na huduma bora sehemu zao za kazi.

Wito huo umetolewa jana na Mhifadhi  Mkuu  Shamba la miti Wino  mkoani Ruvuma Glory Kasmir, wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa mtumishi wa shamba hilo Theofrida Luoga iliyofanyika katika Ukumbi wa Chamali Resort  unaomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania Brigedi 401 Songea.

Alisema,watumishi wakipendana na kushirikiana wanaweza kufanya mambo makubwa katika taasisi zao na kuisaidia serikali kutatua baadhi ya changamoto bila kuhitaji msaada kutoka nje na kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika kwenye idara zao.

Aidha alisema,mtumishi wa umma kufanya kazi zaidi ya miaka 50 hadi kustaafu  siyo kitu kidogo na lazima  kumshukuru sana Mungu kwani muda wote anakabiliwa na kukutana na changamoto nyingi ambazo wakati mwingine zinakatisha tamaa.

“hadi kufikia hatua ya kustaafu katika utumishi wa umma kwa kweli lazima kushukuru Mungu,hapa katikati kuna milima na mabonde ambayo wakati mwingine yanakatisha tamaa,lakini mtumishi hautakiwi kukata tamaa bali unatakiwa kukabiliana nayo  ili uendelea kutekeleza majukumu yako”alisema Kasmir.

Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti Mpepo wilayani Mbinga Misana Magayane alisema,maisha ya utumishi ndiyo marefu zaidi kuliko maisha ya nyumbani au shuleni, hivyo watumishi wanatakiwa kuishi kwa furaha na amani wakati wote.

Magayane alisema, ili  mtu aishi muda mrefu katika utumishi wa umma ni muhimu kuwa amani na  upendo katika utumishi wako kwa sababu hakuna binadamu aliyekamilika.

Magayane aliongeza kuwa,hata wakiletwa malaika kutoka Mbinguni bado tutawakwaza kwa kuwa malaika ni watakatifu na sisi tumelizoea kuishi na jamii ile ile inayotuzunguka kila siku ambayo ina mapungufu na madhaifu makubwa.

Kwa upande wake Theofrida Luoga, amewaomba watumishi waliobaki kukumbuka suala la kumtanguliza Mungu wakati wote katika shughuli zao,kuondoa uwoga na kutoona kufanya kazi ngumu kama sehemu ya adhabu.

Amewataka watumishi wa ngazi za chini ,kuwaheshimu viongozi wao ili kujifunza kutoka kwao namna walivyofanikiwa hadi kufika ngazi za juu za uongozi  na kuacha tabia ya kushindana na kwani  kufanya hivyo hakuleti mafanikio  yoyote kazini.

Comments

Popular posts from this blog

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.