DODOMA KUMEKUCHA FOMU ZA UBUNGE NA UDIWANI ZAANZA KUTOLEWA KAMA NJUGU.

 Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Sophia Kibaba (kushoto), akimkabidhi Fomu ya kugombea ubunge Wakili Erick Kidyalla, Makabidhiano hayo yalifanyika leo asubuhi

WAKILI Eric Kidyalla ni moja ya makada waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania kugombea ya Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jimbo la Dodoma Mjini.

Alisema sababu iliyomsukuma kuchukua fomu hiyo ni kwa kuwa yeye ni kada wa Chama hicho hivyo aliona ni vyema kutumia haki yake ya kikatiba ili akifanikiwa aweze kutoa mchango wake katika kulitumikia Chama na wanaDodoma mjini akishirikiana na watendaji wengine.

Pia ampongeza Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Jimbo la Dodoma mjini liweza kugawanyika jambo ambalo limetoka fulsa kubwa kwa wanaCCM wengi kujitokeza kugombea.

"Jimbo la Dodoma mjini kijiografia lilikuwa kubwa hivyo kuridhiwa ligawanywe,  Rais, Samia amefanya jambo jema na itatoanfulsa kubwa kwa wananchi,"alisema Kidyalla



Joyce Kingerenge, akizungumza na wanahabari baada ya kutoka kuchukua fomu yakugombea ubunge wa viti maalum CCM Dodoma

Waziri wa Madini Anthon Mavunde, akijaza jina lake kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombe ubune baada ya kuwasili ofisi za CCM wilaya ya Dodoma leo. 
Mavunde achukua fomu kwa ajili ya kuomba ubunge tena, amesema bado ananguvu za kuwatumikia wananchi wa Dodoma , hakuwa na maneno mengi wakati akichukua leo asubuhi.amesema atazungumza badae baada ya kupitishwa kwenye mchujo



Akizungumza na wanahabari
Samuel Kisalu, akisubili kupewa fomu ya kugombea ubunge jimbo la Dodoma mjini, 

Akipatiwa fomu hiyo amesema  nia yake ni kuwatumikia Wanadodoma
Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Dodoma Mjini Mengi Mwakisole, akimpatia Britony Machange, fomu ya kugombea Udiwani wa Dodoma Makulu, Kijana huyo mtanashati amejinasibu kwamba anayo ali ya kuwatumikia wananchi Makulu bila hiana , amewaomba vijana wenzake kujitokeza kwa wingi kuacha malalamiko kwamba vijana wametengwa , Sasa hivi kunamsemo wa  Vijana na Taifa la leo na siyo kesho.


 

Comments

Popular posts from this blog

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?