Posts

Showing posts from September, 2025

DKT, NCHIMBI AENDELEA KUKATA MBUGA KUOMBA KURA

Image
  Na Mwandishi Wetu MGOMBEA Mwenza wa Urais wa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ameendelea kunadi Ilani ya Chama hicho ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo. Dk.Nchimbi leo Septemba 9,2025 amewasili mkoani Katavi na kuhutubia wananchi katika Uwanja wa Maridadi,Mpanda mjini, kwenye mkutano wake wa hadhara wa Kampeni akitokea mkoani Rukwa. Baada ya kuwahutubia Wananchi wa Mpanda Mjini,Balozi Nchimbi amewanadi Wagombea Ubunge wa majimbo mbalimbali ya Mkoa huo,akiwemo Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini, Haidary Hemed Sumry pamoja na Madiwani. Awali, Dkt Nchimbi amewahutubia wananchi wa Majimoto,katika jimbo la Kavuu mkoani Katavi na kumnadi Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Laurent Deogratius Luswetula pamoja na Madiwani. Akiwa katika mkutano huo Dk.Nchimbi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Dk.Samia Suluhu Hassan, W...

DKT. BITEKO ASEMA KUMCHAGUA RAIS SAMIA NI KUCHAGUA MAENDELEO-

Image
  * Awahimiza wananchi wa Namonge kujitokeza kupiga kura Oktoba 29 * Asema shilingi bilioni 200 kukopeshwa kwa vijana Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto Mashaka Biteko amewaasa wananchi wa Kata ya Namonge, kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais kwa kuwa ndiye mwenye nia thabiti ya kuwaletea maendeleo. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 9, 2025 katika mkutano wake wa kunadi sera kwa wananchi wa Kata ya Namonge wilayani Bukombe mkoani Geita. Amesema awali sekta zote katika kata ya hiyo zilikuwa zikisuasua kimaendeleo ikilinganishwa na maendeleo yaliyofikiwa sas “Kata hii haikuwa na barabara ya kutoka Uyovu – Namonge – Nyalamandula haikuwa na zahanati wala shule za kutosha hivyo ilikuwa na maendeleo duni” amesema Dkt. Biteko. Amesema jitihada zilizofanywa na Serikali ya Rais Samia katika kuwaletea maendeleo wananchi hao ni kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati na kit...

DKT. NCHIMBI ATINGA BARIADI, AMNADI KADOGOSA NA WAGOMBEA UBUNGE WENZAKE NA MADIWANI

Image
  MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel  John Nchimbi  amepokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa CCM,wilaya ya Bariadi Vijijini  mkoani Simiyu kuendelea na mkutano wa Kampeni, leo Jumatatu Septemba 1,2025. Dk.Nchimbi aliyekuwa Mkoa wa Mara na sasa ameingia Mkoa wa  Simiyu kuendelea na kampeni,akianzia jimbo la Busega na baadae kuelekea  jimbo la Bariadi Vijijini na kufanya mikutano mikubwa ya hadhara.   Akiwahutubia wananchi wa Bariadi Vijijini  mkoani Simiyu, Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi Vijijini,Masanja  Kungu Kadogosa sambamba na wagombea ubunge wengine pamoja na Madiwani wa mkoa huo. Dkt. Nchimbi anaendelea na kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania  kuwaongoza katika awamu nyingine ya miaka mitano, kati...

WIZARA YA FEDHA YAJINOA UTOAJI WA TAARIFA KWA UMMA

Image
  Na Peter Haule, WF,  Dodoma Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Benny Mwaipaja amewataka wajumbe wa Kamati hiyo kuwa sehemu ya kufanikisha utoaji taarifa sahihi na kwa wakati kwa umma ili kutimiza haki ya wananchi kupata taarifa. Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma wakati wa Kikao kazi cha Kamati hiyo kinachohusisha wajumbe kutoka Idara na Vitengo vya Wizara kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa matumizi ya umma. Mwaipaja alisema kuwa Wizara ina jukumu la kutoa taarifa kwa umma kuhusu sera, program, mipango na matukio ya Wizara ili kuuwezesha umma kuwa na uelewa kuhusu majukumu ya Wizara na mambo mengine. “Nitoe rai kwa wajumbe wa Kamati hii kuhakikisha mnatoa ushirikiano kwa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa kuainisha kalenda za matukio muhimu kwa umma ili kitengo kiweze kuzifanyia kazi”, alisema Bw. Mwaipaja. Alisema taarifa zinazopati...

MAPOKEZI YA MGOMBEA MWENZA JIMBONI MBOGWE MKOA WA GEITA

Image
Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi. Dkt. Emmanuel Nchimbi akiteta jambo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko baada ya kuwasili katika Viwanja vya Shule ya Msingi  Masumbwe, Wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita leo Septemba 5, 2025.  

ZITO KABWE AWAOMBA KURA WANANCHI JIMBO LA KIGOMA MJINI

Image
  John Bukuku 13 hours ago Share Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo na mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma mjini Ndugu Zitto Zuberi Kabwe akihutubia maelfu ya watu waliojitokeza katika uzinduzi rasmi wa kampeni zake katika jimbo hilo leo wakati akitangaza sera za chama chake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote

DKT. NCHIMBI AWAHUTUBUA WANANCHI WA ISAKA KAHAMA MKOAMLNI SHINYANGA

Image
  Share Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wakazi wa mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama, jimbo la Msalala,kwenye mkutano mdogo wa hadhara leo Alhamis Septemba 3,2025,mkoani Shinyanga. Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Msalala Mabula Johnson Magangila pamoja na Madiwani. Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.              

DKT NCHIMBI AITIKISA KAHAMA AELEZA SABABU YA DKT SAMIA KUCHAGULIWA TENA

Image
Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi wa Kahama mjini, jimbo la Kahama, leo Alhamis Septemba 4,2025,mkoani Shinyanga. Dkt Nchimbi akihutubia Maelfu ya Wana kahama amesema Dkt Samia anayo kila Sababu ya kupigiwa kura ya ndio katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, kwa Sababu amejipambanua katika Kushughulikia kero na Changamoto mbalimbali za Wananchi, pamoja na kufungua fursa kwa Watanzania. Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama mjini,Benjamin Lukubha Ngayiwa ,pamoja na Madiwani. Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na...