DKT NCHIMBI AITIKISA KAHAMA AELEZA SABABU YA DKT SAMIA KUCHAGULIWA TENA

Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi wa Kahama mjini, jimbo la Kahama, leo Alhamis Septemba 4,2025,mkoani Shinyanga.
Dkt Nchimbi akihutubia Maelfu ya Wana kahama amesema Dkt Samia anayo kila Sababu ya kupigiwa kura ya ndio katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, kwa Sababu amejipambanua katika Kushughulikia kero na Changamoto mbalimbali za Wananchi, pamoja na kufungua fursa kwa Watanzania.
Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi pia aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama mjini,Benjamin Lukubha Ngayiwa ,pamoja na Madiwani.
Balozi
Dkt.Emmanuel Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya Kampeni Mkoani
Shinyanga ya kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo
inalenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika
miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua
mgombea Urais wa CCM, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani
wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
Comments
Post a Comment