MKOA WA KATAVI WANEMEKA NA UONGOZI WA RAIS DKT. SAMIA------MWAMVUA MRINDOKO
Naibu Mkurugenzi wa Idarayahabari MAELEZO, Zamaradi Kawawa, akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Katavi kuzungumza na wanahabari leo Mkuu wa Mkoa wa Katavi M wanamvua Hoza Mrindoko, akizungumza na wanahabari leo katika ukumbni wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dodoma. Akizungumzia mafanikiao ya mkoa huo kwa kipindi cha miaka 5 ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Ndugu Wananchi, Naomba kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwasilisha mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka MITANO ya uongozi wa Dkt. SamiaSuluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 2.0 HALI YA MAENDELEO YA MKOA WA KATAVI. Ndugu Wananchi, Mkoa wa Katavi katika kipindi cha Miaka MITANO ya Uongozi wa awamu ya sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan umepokea Jumla ya Shilingi 1,345,153,585,254.20 ( Trilioni 1.345) kwa ajili ya shughuli za kukuza uchumi, miradi mbalimbali ya maendeleo, kuboresha maisha na ustawi wa Jamii, utawala bora na uwajibikaji ndani ya Mko...