TADB YATOA MIKOPO YA RIBA NAFUU YA TRILIONI 1.129 KWA WAKULIMA KWA MIAKA KUMI

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
KATIKA
kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nanenane),ambayo kitaifa
yatafanyika mkoani Dodoma, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
imetoa mikopo ya riba nafuu yenye thamani ya jumla ya Shilingi Trilioni
1.129 katika kipindi cha miaka kumi kwa lengo la kuwawezesha wakulima
kiuchumi.
Akizungumza
leo Julai 31,2025 jijini Dodoma na waandishi wa habari kuhusiana na
maonyesho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Frank Nyabundege,
amesema benki hiyo imejikita kuunga mkono juhudi za Serikali katika
kuleta mageuzi ya kilimo kwa kumkomboa mkulima wa kawaida kupitia
upatikanaji wa mikopo nafuu.
“TADB
inaendelea kutekeleza wajibu wake wa msingi wa kuwezesha upatikanaji wa
fedha kwa wakulima, kwa masharti rafiki. Lengo letu ni kuona kilimo
kinakuwa cha kibiashara na chenye tija kwa maendeleo ya taifa,” amesema
Bw. Nyabundege.
Bw.
Nyabundege, amesema maonyesho ya mwaka huu yatakuwa ya aina yake kwa
kuwa yanaashiria mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ya kilimo
kupitia huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wakulima nchini.
“Rais
Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani, TADB ilikuwa na mtaji wa
shilingi milioni 60, lakini mtaji huo umeongezeka kwa kiasi kubwa hadi
kufikia shilingi milioni 442. Aidha, Rais Samia aliweka shilingi
trilioni moja Benki Kuu ya Tanzania ili Benki Kuu izikopeshe benki za
kibiashara kwa riba nafuu ya asilimia 3, na hatimaye mikopo kwa wakulima
ipatikane kwa riba ya chini ya asilimia 10, ikilinganishwa na kiwango
cha awali cha asilimia 20 hadi 30.”amesema
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, amesema
maonyesho ya mwaka huu yameboreshwa zaidi na yanatarajiwa kutoa elimu
muhimu kwa wakulima pamoja na wananchi kuhusu teknolojia, mbinu bora za
kilimo na fursa za kiuchumi zilizopo katika sekta ya kilimo.
“Nanenane
si tu maonyesho, bali ni jukwaa la elimu, mafunzo, na uhamasishaji kwa
wakulima wetu. Tunawakaribisha wadau wote kushiriki,” amesema Bw.
Mweli.
Maonyesho
ya Nanenane mwaka huu yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 1 Agosti, huku
mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maonyesho
hayo yatawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakiwemo
wakulima, taasisi za kifedha, watafiti, na makampuni ya pembejeo kwa
lengo la kubadilishana maarifa na kuonyesha mafanikio yaliyopatikana
kupitia mageuzi ya sekta ya kilimo nchini.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli,akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) leo Julai 31,2025 jijini Dodoma kuelekea
maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nanenane),ambayo kitaifa yanafanyika
kuanzia Agosti Mosi hadi 8 katika Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bw. Frank Nyabundege,akielezea mafanikio ya benki hiyo katika kipindi
cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita ambapo benki hiyo
imefadhili maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nanenane).Kushoto ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli.


Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Frank
Nyabundege, akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 400,000,000 kwa ajili
ya kudhamini maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nanenane) Katibu Mkuu wa
Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli,yanayotarajia kuanza Agosti Mosi
katika Viwanja vya Nanenane eneo Nzuguni jijini Dodoma.
Comments
Post a Comment