Dkt. Doto Biteko akizungumza katika mkutano huo Wanahabari wakiwajibika katika mkutamno huo * CCM yajivunia kuimarisha upatikanaji wa huduma bora kwa jamii *Rais Samia asema CCM kuzindua Ilani yake kesho * CCM yazalisha ajira 800,000 kwa vijana 2020/2025 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita aliyowasilisha ni ya mwisho katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020. Amesema hayo Mei 29, 2025 wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa – 2025 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa. Ametaja maeneo sita muhimu ya vipaumbele katika utekelezaji wa Ilani hiyo ya CCM kuwa ni pamoja na kulinda na kuimarisha misingi ya utu, usawa, haki na uongozi bora ili kudumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa. Dkt. ...