DKT BITEKO KATIKA MAZISHI YA ASKOFU DKT SHAO

* Awataka Watanzania kuacha alama katika utumishi wao * Asema Serikali iko pamoja na wafiwa katika kipindi hiki cha majonzi *Askofu Malasusa ataka waumini kumshuhudia Kristo kwa vitendo Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ibada ya mazishi ya Askofu Mstaafu Dkt. Martin Fatael Shao aliyefariki Dunia Agosti 25, mwaka huu. Akizungumza katika ibada ya mazishi Septemba 4, 2025 yaliyofanyika katika kijiji cha Lole, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro Dkt. Biteko amesema Hayati Askofu Shao wakati wa uhai wake alifanya mambo mengi mazuri ya kukumbukwa hata baada ya kifo chake. “ Mzee wetu, Hayati Askofu Shao ameanza kazi za kanisa akiwa kijana na amefanya kazi kubwa ambayo kila mmoja anaishuhudia leo, ameacha alama inayotokana na kazi aliyoifanya, amesema “Mheshimiwa Rais amenituma niwaletee salamu zake za pole nyingi sana Wanafamilia, Vion...