MAVUNDE AZINDUWA KAMPENI ZA KUSAKA UBUNGE AISIMAMISHA DODOMA

Mgombea ubunge jimbo la mtumba Dodoma, Anthony Mavunde akwasili katika viwanja vya  Ofisi ya Mtendaji Ipagala kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni  kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo, kura hizo ni zake, za Rais na Madiwani. uzinduzi huo ulihudhuliwa na Katibu Mkuu Mstaafu na  Makamu Mwenyekiti  wa Chama hicho Tanzania Bara Mzee Philip Jafet  Mangula na Mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Tanzania Bara, John Mongela.


Wasanii wa Vikundi vya Burudani katika jimbo hilo wakimlaki mgimbea huyo












Mgombea Mavunde, akisalimiana na viongozi wa chama hicho 




Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, John Mongela, akiwasili katika eneo hilo akisalimiana na Mghombea ubunge jimbola Chamwino,Deogratius  Ndejembi  




Mgombea Ubunge wa Dodoma Mjini Paschal Inyasa Chinyele akiwasalimia wananchi
Umati wa wananchi wakisikiliza madini toka kwa Mavunde 




Ndejembi akisalimia wananchi


Mzee Mangula, akiwasisitiza Wanaccm na Mashabiki wa  chama hicho kujitokeza kwa wingi siku ikifika ya kwenda kupiga kura wasiishie kujazana kwenye mikutano badae kwenye umaliziaji wa kuwapata vingozi wasifike




Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mongela, (katikati), aakipiga makofi baada ya kumpokea  mwanachama mpya wa chama hicho aliyekuwa akiwasumbuwa katika jimbo hilo kutoka Chadema Benedict Komba (kulia), alikabidhi kadi ya Chadema na kukabidhiwa ya chama hicho. ameahidi kuwa Bega kwa bega na mgombea Mavunde hadi ushindi upatikane, Komba amesema kuna mgombea mmoja katika jimbo hilo haelewiki anakoishi ila yupoyupo wampuuze wapiga kura bila kutaja chama anachogombea.


Mongela ,akionyesha kadi ya Chadema










Baadhi ya Madiwani wa jimbo hilo
Mongela, amewaomba Wanamtumba, kutopuuzia chochote kwenye upigaji wa kura, hata wale madiwani waliokosa wagombea wenzao wajitokeze siku ya kupiga kura wakatekeleze wajibu wao, atashangaa mgombea yoyoye wa chama hicho akipigiwa kura nyingi za hapata na wapinzani huku wanaccm kindakidanki hawajaenda kutekeleza wajibu wao wa kupiga kura. Kuhusu Mavunde amesema anajitoshereza mwenyewe  wingi wa waliojitokea katika mkutano huo inaonyesha kiasi gani ni kipenzi cha watu , hana majivuno, ni mtu wa watu , mongela alisema alipofika  katika eneo hilo alidhani ni mkutano wa Mkoa kumbe wa jimbo moja tuu. "Hakika mavunde ni kijana wa watu siku ikifika mkamuonyesha mahaba mazito kura nyingi kwake na kwa Rais na Madiwani", aliomba Naibu Katibu huyo
Mavunde amewaomba Wanamtumba wampe kura awaonyeshe jinsi maendeleo yatakavyo kuja haraka , alisema ameweza kutekeleza ahadi zake zote wakati akiwa na kata zaidi ya 40 za jimbo la Dodoma kabla halijagawanywa na kuwa mawili hatashindwa kwa kata zilizobaki 20 kuzitendea haki  ataanza na kutekeleza maswala ya Maji, anataka iwe Historia kukosa maji jimboni kwake, Michezo na burudani atajenga studia ambayo wanamuziki na vikundi vyote vya sanaa watarekondi bure katika studio hiyo , ataongeza Zahanati  katika jimbo hilo  mikopo kwa akina mama na vijana hiyo itakuwa nje nje. Amewaomba wampe kura yeye Rais na Madiwani wa Chama hicho.




Akiwanadi Madiwani wa jimbo lake





 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA