TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAMIMINIWA SIFA NA WAGOMBEA URAIS
Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi imemiminiwa sifa na wagombea waliofika Makao Makuu ya Tume hiyo yaliyopo eneo la Njedengwa jijini Dodoma kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Tanzania.
Utoaji fomu ulioanza 9 Agosti 2025 hadi 15 agost 2025 ikiwa vyama 18 vimechukuwa fomu za kuomba ridhaa hiyo, kuna vilivyofika katika ofisi hiyo kwa mbwembwe na vigoma lakini kuna vingine vilifika kimya kimya.
Chama kilichofunguwa pazia kilikuwa Chama Tawala Chama cha Mapinduzi kikiongozwa na mgombea wake Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea wake Mwenza Dkt. John Nchimbi.
Chama kilichofunga pazia ni Chama cha ACT Wazalendo, kikiongozwa na mgombea wake Luhanga Mpina na Mgombea mwenza wake Fatma Abdulhabib Ferej.
Tume hiyo ikiongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele imeweza kutoa fomu za uteuzi kwa wanachama 36 kwa vyama 18 vya siasa kugombea nafasi
Wagombea hao kila walipokabidhi fomu na Mwenyekiti wa Tume hiyo na badae kuzungumza na wanahabari hawakusita kuipongeza tume hiyo kuanzia kwa maelezo ya Mwenyekiti wake na Mapokezi waliyopata kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima.
Ambaye hakutaka kuficha furaha yake ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini, baada ya mazungumzo na wanahabri hakusita kwenda kuteta kidogo na Mkurugenzi wa Uchauguzi wa Tume hiyo Ramadhani Kailima.
Selasini alisema amekuwa kwenye vyama hivi tangu chaguzi za vyama vingi vianze 1995 hajawahi kuona nidhamu kwa wajumbe kama hii na mwenyekiti wao wamekuwa na nidhamu ya hali ya juu hakika wakiendelea hivi hata kwenye kutangaza matokeo itakuwa vyema sana
Jaji Mwambegele kila alipokuwa akitoa fomu alikuwa akisema utoaji wa fomu hizo umezingatia masharti ya Ibara ya 39(1)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, ikisomwa pamoja na kifungu cha 34(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 na Kanuni ya 20(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025.
aji Mwambegele amewakabidhi wanachama waliopendekezwa begi maalum lenye nakala 40 za Fomu za Uteuzi wa Wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais – Fomu Na. 8A, nakala nane (8) za Tamko la Mgombea Kuheshimu na Kutekeleza Kanuni za Maadili ya Uchaguzi za Mwaka 2025 - Fomu Na. 10.
Nyaraka nyingine alizowakabidhi Mwenyekiti huyo ni nakala mbili (2) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, nakala mbili (2) za Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Nakala mbili (2) za Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024 na nakala mbili (2) za Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025.
Nyingine ni nakala mbili (2) za Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024, nakala mbili (2) za Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025 na nakala mbili (2) za Vitabu vya Maelekezo kwa Vyama vya Siasa na Wagombea na walipatiwa barua yenye kuonyesha namba ya akaunti kwa ajili ya malipo ya fedha za dhamana.
Jaji huyo alikuwa akiongea kwa uyenyekevu mkubwa "Waheshimiwa mliopendekezwa kugombea nafasi ya Kiti cha Rais na Makamu wa Rais, tunawasihi mkazisome nyaraka zote tunazowapatia leo, ili ziweze kuwasaidia katika ujazaji wa fomu za kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais, kufanya kampeni na michakato yote ya uchaguzi.” alisema. Jaji Mwambegele.
Mbali na kuwasihi kusoma nyaraka hizo, Jaji Mwambegele amewatakia kila la kheri wanachama hao waliopendekezwa kugombea nafasi hizo katika kukamilisha kazi kubwa iliyo mbele yao.
Wanachama waliopatiwa fomu za uteuzi ni Dkt. Samia Suluhu Hassan kugombea nafasi ya Kiti cha Rais na Dkt. Emmanuel Nchimbi (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Hassan Kisabya Almas (Kiti cha Rais) na Hamisi Ally Hassan (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA).
Wengine ni Kunje Ngombale Mwiru (Kiti cha Rais) na Shum Juma Abdalla (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP), Doyo Hassan Doyo (Kiti cha Rais) na Chausiku Khatib Mohamed (Kiti cha Makamu wa Rais) wa Chama cha National League for Democracy (NLD) na Coster Jimmy Kibonde (Kiti cha Rais) na Aziza Haji Suleiman (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Makini (MAKINI).
Wanachama wengine ni Twalib Ibrahim Kadege (Kiti cha Rais) na Abdalla Mohd Khamisi (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha United People's Democratic Party (UPDP), Georges Gabriel Bussungu (Kiti cha Rais) na Ali Makame Issa (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA), na Mwajuma Noty Mirambo (Kiti cha Rais) na Mashavu Alawi Haji (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD),
Yustas Mbatina Rwamugira (Kiti cha Rais) na Amana Suleiman Mzee (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), David Daud Mwaijojele (Kiti cha Rais) na Masoud Ali Abdala (Kiti cha Makamu wa Rais) wa Chama cha Kijamii (CCK), Salum Mwalimu (Kiti cha Rais), Devotha Mathew Minja (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma).
Wengine ni Abdul Juma Mluya (Kiti cha Rais) na Sadoun Abrahman Khatib (Kiti cha Makamu wa Rais) wa Chama cha Democratic Party (DP) na Majalio Paul Kyara (Kiti cha Rais) na Satia Mussa Bebwa (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU).
Aidha, wanachama wengine ni Gombo Samandito Gombo (Kiti cha Rais) na Husna Mohamed Abdalla (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Wilson Elias Mulumbe (Kiti cha Rais) na Shoka Khamis Juma wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).
Siku ya mwisho ya utoaji fomu za uteuzi ilikamilika kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele kutoa fomu kwa Saum Hussein Rashid (Kiti cha Rais) na Juma Khamis Faki wa Chama cha United Democratic Party (UDP), Haji Ambar Khamis (Kiti cha Rais) na Dkt. Eveline Wilbard Munisi (Kiti cha Makamu wa Rais) wa Chama cha National Convention for Construction and Reform – Mageuzi (NCCR-MAGEUZI), aliyefunga pazia ni Luhaga Joelson Mpina (Kiti cha Rais) na Fatma Abdulhabib Ferej (Kiti cha Makamu wa Rais) kupitia Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – WAZALENDO).
Pongezi hizo hazikuishia kwa wahgombea hao hata nkwa wanahabri nao walisikika wakiipongeza Tume hiyo kupitia kwa Mkurugenzi wake Ramadhani Kailima, ambapo aliwaandalia hema kwa ajili ya kuandika Habari zao vyema
Kama kusingekuwa na hema ingekuwa vigumu kwani kulikuwa na upepo na jua kali kipindi cha mchana na asubuhi ni baridi kali, kila siku walikuwa wagombea watatu wakichukua fomu kwa nyakati tofauti.
Comments
Post a Comment