NAIBU KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA (MSTAAFU) ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU WA CCM
DKT. Asha-Rose Migiro ameteuliwa kumrithi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye ni Mgombea Mwenza wa urais wa Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Desemba 29,2025.
Uteuzi huo uliothibitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, yametangazwa mbele ya vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla mara baada ya kutangaza uteuzi wa mwisho wa wagombea ubunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi leo katika Ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Pia, Makalla amechukua fursa hiyo kutangaza mabadiliko mengine ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi ameteuliwa kuchukua nafasi yake ya Katibu Mwenezi.
Comments
Post a Comment