KASI NDOGO YA UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME WA CHALINZE- DODOMA YAMKASIRISHA DKT. BITEKO


📌 Asikitishwa mradi huo aliouzindua Novemba 2024 kuwa nyuma kwa asilimia Saba

📌 Asema Rais Samia alitoa agizo mradi usichezewe kutokana na umuhimu wake katika  mikoa mbalimbali ikiwemo ya Magharibi

📌 Asema sababu zilizotolewa na mkandarasi (TBEA) za kusuasua kwa mradi hazikubaliki

📌 Atoa maagizo kwa Mkandarasi kuwasilisha mpango kazi mpya kwa Katibu Mkuu  Wizara ya Nishati  ili kufidia muda uliopotezwa

📌;Aagiza TANESCO kutumia mapato ya ndani kulipa fidia wananchi wanaopisha mradi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekagua mradi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 400 kutoka Chalinze  hadi Zuzu Dodoma na kueleza kutoridhishwa kwake na utekelezaji wa mradi huo ambao  ulipaswa kuwa umefikia asilimia 31 lakini kwa sasa  umefikia asilimia 24 tangu kuzinduliwa kwake Novemba mwaka 2024. 

Hali ya kusuasua kwa mradi imebainika wakati Dkt. Biteko akikagua mradi huo katika Kijiji cha Manchali wilayani Chamwino mkoani Dodoma tarehe 20 Agosti 2025 ambapo Dkt. Biteko amemuagiza mkandarasi kampuni ya TBEA ya China kuhakikisha kuwa anafidia muda wa kazi uliopotezwa wa asilimia Saba ili mradi ukamilike kwa wakati kutokana na umuhimu wake nchini.

Mwezi Novemba, 2024 Serikali ilikubaliana na mkandarasi kuwa mradi huo ufanyike ndani ya miezi 19 tu badala ya miezi 22 kwani wakati mradi unazinduliwa tayari kazi kubwa za awali zilikuwa zimeshafanyika ikiwemo za upembuzi yakinifu na utoaji wa maeneo. 

“ Leo ni miezi saba imepita tangu tuzindue mradi sawa na asilimia 32 ya muda wote tuliokuwa tunahitaji  kutekeleza mradi huu, na tulitegemea mradi kwa sasa ufikie asilimia 31 lakini katika hali ya kushangaza mradi umefikia asilimia 24 tu jambo ambalo halikubaliki.” Amesema Dkt. Biteko

Dkt. Biteko ameeleza kuwa, sababu zilizotolewa na Mkandarasi za kuchelewesha mradi ikiwemo ya wananchi kugoma kutoa maeneo kwa madai ya fidia na kukutana na miamba katika mkuza wa mradi hazikubaliki kwani  wananchi  hao wana haki na  lazima walipwe fidia.

Kutokana na hali hiyo, ameagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  kutumia mapato  ya ndani.
                   














 

Comments

Popular posts from this blog

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?