Posts

Showing posts from August, 2025

DKT NCHIMBI AMPOKEA DKT MIGIRO NA KUMKABIDHI OFISI MAKAO MAKUU YA CHAMA DODOMA LEO.

Image
Wanaccm na Mashabiki wa chama hicho wakiongozana na gari lililomchukua Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt Asha -Rose Migiro kwennda kukabidhiwa ofisi na Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake Dkt John Nchimbi makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo mchana. Mwenyekiti wa umoja wa Wanawake wa CCM, Mary Chatanda, akiongoza viongozi wa Chama  hicho kumpokea Katibu Mkuu Mpya wa Chama hicho Dkt. Asha -Rose Migiro, alipowasili leo Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dodoma kwa ajili ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa katibu Mkuu Dkt. Emmanuel Nchimbi Dkt. Migiro, akivalishwa skafu na chipukizi wa chama hicho baada ya kuwasili  Makada na wana Ccm wakiwa makao makuu ya Ccm Dodoma wakimlaki katibu mkuu wa Ccm Mpya  Dkt.Asha Rose Mingiro ambaye amefika ofisini kwa Mara ya kwanza na kupokelewa na katibu mkuu mstasfu na mgombea mwenza Comred Dkt Emanuel John Nchimbi Akivalishwa vazi la Kigogo  A  

KESHO WAGOMBEA URAIS KULEJESHA FOMU TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI KUANZIA SAA MOJA ASUBUHI.

Image
 

RITA KABATI AFUNIKA UCHUKUAJI FOMU JIMBO LA KILOLO

Image
  @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ MGOMBEA Ubunge jimbo la Kilolo na mwanamke Pekee mkoa wa Iringa kugombea ubunge, Rita Kabati amefunika katika zoezi la uchukuaji fomu kwa kupata wadhamini wengi kutoka Chama Cha Mapinduzi . Kabati anbaye alisindikizwa na makada mbalimbali akiwemo pacha wake Venance Mwamoto aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo alichukua fomu huku umati wa wananchi wa jimbo wakishuhudia zoezi hilo. Rita Kabati ambaye kabla ya kuchukua fomu kugombea jimbo amekuwa mbunge viti maalum mkoa wa iringa kwa miaka 15 hivyo kumwezesha kuwa mbunge mwenye uzoefu bungeni na CCM kumwamini kuwa mwakilishi pekee wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa ambaye ni mwanamke wa shoka. Akizungumza baada ya kuchukua fomu Dkt. Kabati aliwashukuru viongozi wa CCM kwa imani waliyoonesha kwake na kutoa wito wa mshikamano miongoni mwa wanachama wa chama hicho akisema huu ni wakati wa kuvunja makundi na kuungana kwa pamoja kuhakikisha ushindi wa CCM kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge hadi urais. “Naomba maku...

CP SHILOGILE AWAPONGEZA WATENDAJI WA DAWATI LA JINSIA – SONGWE

Image
  @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe wapongezwa kwa utendaji mzuri wa utoaji huduma bora kwa mteja. Kamishna wa Polisi Jamii CP Faustine Shilogile amehimiza utendaji wenye weledi na Uadilifu wakati akizungumza na Watendaji wa Dawati hilo akiwa ziarani Mkoani Songwe Agosti 25, 2025. CP Shilogile pamoja na ujumbe wake kwa watendaji hao, alipokelewa na tafrija maalum iliyopambwa na shampeni, kukata keki, pamoja na kupatiwa zawadi mbalimbali kama ishara ya shukrani na kuthamini mchango wao katika kulinda haki na ustawi wa watoto na wanawake. Kamishna Shilogile, amepongeza juhudi za watendaji hao na kusisitiza kuwa mafanikio ya Dawati la Jinsia na watoto yanatokana na moyo wa kujitolea, uadilifu na uwajibikaji wa watumishi hao katika kutatua changamoto mbalimbali za kijinsia zinazowakabili wananchi. Aidha, alisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuwa bega kwa bega na dawati hilo katika kuhakikisha kuwa huduma bora na...

WAZIRI RIDHIWANI KIKWETE AZINDUA MIONGOZO NA MIFUMO YA KIELEKTRONIKI YA OFISI YA WAZIRI MKUU

Image
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amezindua miongozo mitatu na mifumo ya kielektroniki miwili ambayo inalenga kuimarisha uratibu, usimamizi na uendeshaji wa masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu. Miongozo na Mifumo iliyozinduliwa ni pamoja na Mwongozo wa Majadiliano baina ya Serikali, Vyama vya Wafanyakazi na Vyama vya Waajiri wa Mwaka 2025, Mwongozo wa Uratibu wa Vyama vya Watu Wenye Ulemavu wa Mwaka 2025, Mwongozo wa Wakala Binafsi wa Ajira wa Mwaka 2025, Mfumo wa Kitaifa wa Kieletroniki wa Taarifa za Soko la Ajira wa Mwaka 2025 na Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mashauri ya Usuluhishi na Uamuzi wa Mwaka 2025. Akizindua 22 Agosti, 2025 jijini Dodoma, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema kuwa miongozo na mifumo itasaidia kujenga misingi ya majadiliano yenye tija na jumuishi, uimarishwaji wa haki za Watu wenye Ulemavu, usimamizi makini wa mawakala wa ajira, pamoja na uwepo wa mifumo ya...