KATIBU WA NEC, SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA, RABIA AKUTANA NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs)


Katibu wa NEC ,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia  Abdalla Hamid (katikati), akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga na Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Neema Lugangira. Mazungumzo hayo yalifanyika baada ya kumalizika mazungumzo 


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga akzungumzia ushirikiano uliopo kati ya serikali na NGOs.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC) Kenneth Simbaya , akizungmza
 Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa, akizungumza


Baadhi ya washiriki kutoka NGOs wakiwa katika mkutano huo.


Mbune wa viti Maalum Neema Lugangira akizungjmza



Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi, Rabia Abdalla Hamid, amekutana na kufanya mazungumzo na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) katika Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM, Mjini Dodoma.

Katika kikao hicho,  Rabia alipata fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali pamoja na kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Asasi za Kiraia walioratibiwa na Mbunbe wa Viti Maalum kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM),  Neema Lugangira, Mbunge wa Viti Maalum CCM Kundi la NGOs. 


Miongoni mwa waliokutana naye ni pamoja na Baraza la Taifa la NGOs (NACONGO), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, wawakilishi wa Machinga, na Chama cha Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA).


Akizungumza katika kikao hicho, Rabia aliwataka wadau wa asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kuendeleza mshikamano na kushirikiana kwa karibu katika kuunga mkono juhudi za maendeleo. Alisisitiza umuhimu wa kuelekeza nguvu kwa pamoja katika kupambana na changamoto za umasikini, maradhi na ujinga, ili kujenga taifa lenye ustawi na haki kwa wote. Aidha na kuwaomba kuyatangaza mema yote yanayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani sasa hivi nchi inapaa na  uchaguzi wa mwaka huu wampe mitano tena.

















Katibu  Rabia akiwa katika picha ya pamoja na Lugangira, Nderiananga pamoja na baadhi ya viongozi wa NGOs.

Washiriki wa kikao hicho wakitoka  baada ya kumaliza

 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA