Posts

Showing posts from April, 2025

KATIBU WA NEC, SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA, RABIA AKUTANA NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs)

Image
Katibu wa NEC ,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia   Abdalla Hamid (katikati), akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga na Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Neema Lugangira. Mazungumzo hayo yalifanyika baada ya kumalizika mazungumzo   Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga akzungumzia ushirikiano uliopo kati ya serikali na NGOs. Mkurugenzi Mtendaji   wa   Umoja   wa   klabu za waandishi   wa habari   nchini ( UTPC ) Kenneth Simbaya , akizungmza   Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC),   Onesmo Ole Ngurumwa, akizungumza Baadhi ya washiriki kutoka NGOs wakiwa katika mkutano huo. Mbune wa viti Maalum Neema Lugangira akizungjmza Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi, Rabia Abdalla Hamid, amekutana na kufanya mazungumzo na mashirika yasiyo ya kiseri...

DKT.BITEKO AWASILISHA BUNGENI BAJETI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2025/2026

Image
📌 Yagusa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa asilimia 96.5 📌 Upatikanaji umeme wa uhakika. Nishati Safi ya Kupikia, Uendelezaji Gesi Asilia; Baadhi ya vipaumbele vya Bajeti 📌 JNHPP, Usambazaji Umeme Vijijini na Ufikishaji Gridi Kigoma; Baadhi ya mafanikio Bajeti 2024/2025 📌 Kamati ya Bunge yaridhishwa na utekelezaji wa Bajeti ya Wizara mwaka 2024/2025 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/2026 ya kiasi cha shilingi Trilioni 2.2 ambapo asilimia 96.5 ya Bajeti yote ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo  na asilimia 3.5 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Akiwasilisha Bajeti hiyo leo tarehe 28 Aprili, 2025 bungeni jijini Dodoma, Dkt. Biteko ametaja vipaumbele mbalimbali vya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/2026 ikiwemo kuendelea kuimarisha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme, pamoja na kufikisha Gridi ya Taifa katika mikoa iliyosalia ya Ruk...

WAKULIMA JIUNGENI NA VYAMA VYA USHIRIKA VILIVYOSAJILIWA------MAJALIWA

Image
Waziri Mkuu . Kassim Majaliwa,amewaomba wakulima na wananchi kwa ujumla wahakikishe wanajiunga na vyama vya ushirika vilivyosajiliwa, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali na wadau wa maendeleo. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo wakati akifungua  mdahalo wa Upatikanaji Mitaji ya Fedha za Maendeleo ya Ushirika ulioenda sambamba na ripoti ya Mwaka ya Kilimo kwa mwaka 2022/2023, 2023/2024 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma. “Wadau wote wa maendeleo, endeleeni kushirikiana na Serikali katika kutoa rasilimali, utaalamu na ubunifu unaohitajika katika kuendeleza sekta hii muhimu.”amesema .Majaliwa  Pia ameitaka Wizara ya Kilimo kuhakikishe maandiko ya taarifa zilizozinduliwa zinaandaliwa pia kwa lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kunufaika nazo.   Waziri Mkuu amesema Sekta ya Ushirika nchini inaendelea kuimarika kwa kasi, ikiwa ni mhimili muhimu wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hasa katika maeneo mbalimba...