MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO HADI SONGEA UNAOFADHIRIWA NA NCHI YA SWEDEN WAFUNGWA MAHESABU YAKE.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo na Balozi wa Swedeni nchini  kuhusu kufunga mahesabu ya mradi wa umeme kutoka Makambako hadi Songea . mradi huo ulikuwa ukifadhiliwa na nchi hiyo,  Katibu Mkuu aliipongeza nchi hiyo kwa kuweza kuinufaisha Tanzania kwa ufadhili wake. Katibu hyo alibainisha kwamba nchi hiyo imebakiza ufadhili wake katika maswala ya Umeme ni umeme wa Hale ambapo wanafanyia matengenezo makubwa , alibainisha kwamba  umeme wa hale ulianza kutumika tangu mwaka 1964 sasa Sweden inakalabati ili uweze kutumika vyema kwa mikoa ya jirani na Tanga. Kushoto ni Balozi wa Sweden nchini  Bii  Charlotta Ozaki-Macias. Mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2017 ulizinduliwa na Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Joseph Magufuli, mradi huo ulifadhiliwa kwa mkopo na serikali ya swedeni na leo hii umefungwa rasmi, Mramba alibainishwa kwamba nchi hiyo imefadhili Tanzania kwa miradi mingi ya nishati ya umeme nchi hiyo imehusika sana na umeme vijijini  karibu nchi nzima kusambaza. Aidha kwa bwawa la Mtela napo nchi hiyo imehusika kikubwa aidha hata mikoa mingine imeweza kupatiwa miradi ya  umeme wa Sola. Mramba aliipoingeza nchi ya Sweden kwa kuweza kuendelea sana kwa umeme wa maji", Tunaipongeza Sweden kwa ufadhili wake wa umeme  nchini na miradi mingine, nchi hiyo imeendelea sana kwa umeme wa maji hakika tumenufaika nayo tunaishukuru sana, sasa tumebaki kusaidiwa ukarabati wa umeme wa hale ambako nako kunafanyiwa matengenezo makubwa ili tuzidi kunufaika na umeme huo wa maji". alisema Katibu Mkuu Mramba. Mazungumzo hayo yalifanyika jijini Dopdoma leo na kuhudhuliwa na Maofisa kutoka  Shirika la Umeme Tanesco ,  REA na Makambako ,Songea na Hale



Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Mhandisi ,Gissima NMyamo-Hanga, (kushoto), akisisitiza jambo katika kikao hicho


Katibu Mkuu Mramba (kushoto), akisisitiza jambo katika kikoa hicho









Balozi wa Sweden nchini  Bii  Charlotta Ozaki-Macias (wapili kulia), akisisitiza jambo katika kikao hicho








 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA