AWAMU YA SITA IMEVUTIA WAWEKEAJI WENGI NCHINI M----- GILEAD TERI .MKURUGENZI TIC
Wanahabari wakimsikiliza mkurugenzi huyo
Mkurugenzi wa kituo cha uweezaji nchini (TIC), Gilead Teri, akizungumza mbele ya wanahabri kuhusu utendaji kazi wa kituo hicho kwa miaka mnne ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kituo hicho kinaendelea kupokea wawekezaji wengi wa nje na ndani
KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC)
HALI YA UKWEKEZAJI NCHINI
TAARIFA YA MAFANIKIO YA UWEKEZAJI KIPINDI CHA AWAMU YA SITA - JANUARI 2021 HADI JANUARI 2025
1.0. Utangulizi
Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimeanzishwa chini ya sheria ya Uwekezaji kikiwa na majukumu ya kuratibu, kuhamasisha, na kuhudumia wawekezaji kwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kutoa vibali, leseni na usajili wa uwekezaji kupitia Kituo cha Mahali Pamoja (One Stop Facilitation Centre).TIC pia ina jukumu la kukusanya, kuchambua, kuhamasisha na kusambaza taarifa za fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini. TIC vilevile ina wajibu wa kushauri Serikali kuhusu kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.
2.0 Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Kuhamasisha Uwekezaji
Tanzania kupitia serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha minne kuanzia Januari 2021 mpaka Januari 2025 Tanzania imefanyasha maboresho makubwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Maboresho haya yanathibitisha azma ya Tanzania ya kujenga mazingira mazuri zaidi na yaliyorahisishwa kwa ajili ya kukuza uwekezaji hapa nchini.
3. 0 Usajili wa Miradi ya Uwekezaji TIC Katika kipindi cha miaka Minne cha Serikali ya Awamu ya Sita
Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya Sita kati ya Januari 2021 hadi Januari 2025, TIC imesajili miradi 2,020, ambayo ni ongezeko la asilimia 91 ikilinganishwa na miradi 1,057 iliyosajiliwa katika kipindi cha 2017-2020.
Thamani ya mitaji ya miradi hii inakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 23.67, ikiongezeka kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2 katika kipindi cha 2017-2020.
Aidha, miradi hii inatarajiwa kutoa Ajira zilizozalishwa kutokana na usajili wa miradi kumekuwa na ongezeko la Asilimia 284.5 kutoka ajira 136,232 zilizozalishwa kipindi cha miaka minne ya kuanzia mwaka 2017 mpaka 2020 mpaka ajira 523,891 zinazotarajiwa kuzalishwa katika kipindi cha miaka minne ya awamu ya sita kuanzia 2021-2024.
Kumekuwa na ongezeko la usajili wa miradi kutoka nje linalotokana na juhudi zinazofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuitangaza nchi na kuhamasisha uwekezaji kupitia sera yetu maalum ya mashirikano kupitia Diplomasia ya kiuchumi. Na pia ongezeko la miradi linatokana na ushiriki wa Tanzania katika makongamano mbalimbali nje ya Nchi na maboresho mbalimbali yanayofanywa na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini.
3.1 Thamani Ya Mitaji
Thamani ya mitaji ya miradi iliyosajiliwa imepanda kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2 hadi bilioni 23.67, ishara ya kuongezeka kwa uaminifu wa wawekezaji kwa serikali ya Awamu ya Sita.
3.1 Usajili wa Miradi ya Uwekezaji
Katika kipindi mwaka Januari2021 hadi Januari 2025 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili jumla ya miradi 2,020 ambayo ilikadiriwa kuwekeza kiasi cha mtaji wa Dola za Marekani bilioni 23.67 na kutoa jumla ya ajira 523,891. Kati ya miradi hiyo asilimia 35 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya Wageni na asilimia 23.1 ni ya ubia kati ya Watanzania na Wageni.
Aidha, tathmini inaonesha kuwa idadi kubwa ya miradi iliyosajiliwa ipo katika sekta za kipaumbele ambazo ni: Uzalishaji viwandani miradi 538 (45.29%), Usafirishaji miradi 225 (18.94%), Utalii miradi 110 (9.26%), sekta ya ujenzi wa majengo ya biashara miradi 106 (8.92%) Kilimo miradi 106 (8.50%), kama inavyoonesha katika Jedwali Na. 1.Jedwali Na.1: Mwenendo wa Uwekezaji kwa kipindi cha Januari 2021 - Januari 2025
TANZANIA INVESTMENT CENTRE |
||||||||
TIC Registered Projects, Employment & Projects' Value Records 2021 - January, 2025 |
||||||||
Mwaka |
Miradi |
New |
Exp/Reh |
Local |
Foreign |
J/Venture |
Jobs |
Value USD Mln |
2025(JANUARY) |
44 |
42 |
2 |
16 |
17 |
11 |
80,674 |
303.26 |
2024 |
901 |
850 |
51 |
321 |
404 |
176 |
212,293 |
9,312.69 |
2023 |
526 |
469 |
57 |
182 |
214 |
130 |
37,010 |
5,720.36 |
2022 |
293 |
292 |
1 |
99 |
112 |
82 |
40,889 |
4,537.70 |
2021 |
256 |
254 |
2 |
75 |
114 |
67 |
3,025 |
3,791.66 |
Chanzo : Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) 2025
3 2 Mgawanyo wa Umiliki katika Miradi ya Uwekezaji kwa kipindi cha Januari 2021 hadi Januari, 2025
Katika miradi hii, asilimia 34.3 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya wageni, na asilimia 23.1 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni ukilinganisha na miradi iliyosajiliwa katika kipindi cha kuanzia 2017 hadi 2020 ambapo asilimia 27.4 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 44.1 ni ya wageni, na asilimia 28.5 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni.
Juhudi zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita kushusha kiwango cha chini cha kuruhusu kusajili mradi Kituo cha Uwekezaji ili kupata vivutio kutoka dola za Marekani laki moja mpaka dola 50,000 kimesaidia kuongeza usajili wa miradi ya wawekezaji wa ndani.
3.3 Thamani ya Mitaji ya Miradi ya Uwekezaji Iliyosajiliwa TIC Kisekta
Katika kipindi cha Awamu ya Sita, kuanzia Januari 2021 hadi Januari 2025, TIC imesajili miradi 2,020, ambayo ni ongezeko la asilimia 91 ikilinganishwa na miradi 1,057 iliyosajiliwa katika kipindi cha 2017-2020. Thamani ya mitaji ya miradi hii inakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 23.67, ikiongezeka kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2. Aidha, miradi hii inatarajiwa kutoa ajira 523,891, ongezeko la asilimia 284.6 ukilinganisha na ajira 136,232 za 2017-2020.
Katika miradi hii, asilimia 34.3 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya wageni, na asilimia 23.1 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni.
3.4 Mafanikio ya Usajili wa Miradi Kisekta
Tathmini inaonesha kuwa idadi kubwa ya miradi iliyosajiliwa ipo katika sekta za kipaumbele ambapo Sekta ya uzalishaji viwandani inaongoza kwa kuwa na jumla ya miradi 917 sawa sawa na asilimia 45.39 ikifuatiwa na Sekta ya Usafirishaji yenye miradi 348 sawa na asilimia 17.22 na kufuatiwa na Sekta ya Ujenzi wa majengo ya biashara 304 sawa asilimia 15.04. Sekta ya nne inayoongoza kufaya vizuri ni sekta ya Utalii yenye miradi 191 ambayo ni asilimia 9.45 na sekta ya Tano kwa kufanya vizuri katika kipindi cha awamu ya sit ani sekta ya Kilimo yenye miradi 180 ambayo ni asilimia 8.91.
Jedwali Na.2: Mchanganuo wa Idadi ya Miradi Iliyosajiliwa kwa sekta kwa kipindi cha mwaka Januari 2021 – Januari, 2025.
INVESTMENT PROJECTS REGISTERED FROM 2021-JANUARY 2025 |
||||||||
SECTORS |
PROJECTS APPROVED. |
NEW PROJECTS |
EXP/REH PROJECTS |
LOCAL PROJECTS |
FOREIGN PROJECTS |
JOINT VENTURE |
JOBS |
VALUE USD (M) |
Agriculture |
180 |
169 |
11 |
57 |
82 |
41 |
162974 |
1898.16 |
Broadcasting |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0.00 |
Commercial Building |
204 |
199 |
5 |
65 |
103 |
36 |
15,477 |
3,763.80 |
Computer |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
- |
- |
Economic Infrastructure |
20 |
20 |
0 |
10 |
8 |
2 |
69,285 |
672.35 |
Energy |
17 |
16 |
1 |
4 |
9 |
4 |
76,610 |
194.30 |
Finacial Services |
5 |
5 |
0 |
0 |
3 |
2 |
2,897 |
619.52 |
Human Resources |
39 |
38 |
1 |
17 |
8 |
14 |
4,287 |
230.83 |
Manufacturing |
917 |
885 |
32 |
237 |
476 |
204 |
117,773 |
10,026.87 |
Mining |
13 |
13 |
0 |
6 |
1 |
6 |
630 |
54.87 |
Natural Resources |
1 |
1 |
0 |
0 |
1 |
0 |
20 |
0.65 |
Services |
76 |
76 |
0 |
18 |
31 |
27 |
8,248 |
714.46 |
Telecommunication |
9 |
8 |
1 |
1 |
5 |
3 |
964 |
1,015.20 |
Tourism |
191 |
170 |
21 |
76 |
58 |
57 |
14,210 |
972.38 |
Transportation |
348 |
307 |
41 |
202 |
76 |
70 |
50,516 |
3,502.29 |
Grand Total |
2020 |
1907 |
113 |
693 |
861 |
466 |
523,891 |
23,665.67 |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Chanzo : Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) 2025
3.5 Ongezeko la Miradi ya Upanuzi/ Expansion
Miradi ya upanuzi/Expansion projects usajili wake umeongezeka ambapo, katika kipindi Januari 2021 hadi Januari, 2025 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili jumla ya miradi 113 ukilinganisha na kipindi kama hicho cha Januari 2017 hadi Januari 10, 2021 ni mradi mitatu tu ya upanuzi ilisajiliwa. Ongezeko la usajili wa miradi ya upanuzi umetokana na mabadiliko katika Sheria mpya ya Uwekezaji ya mwaka 2022 iliyotoa unafuu wa vivutio vya uwekezaji kwa miradi ya upanuzi ambapo hapo awali ilikuwa haipati vivutio vya uwekezaji hasa vya kikodi. Lakini pia ongezeko husika linatokana na imani wawekezaji waliyonayo juu ya serikali katika masuala ya mazingira rafiki ya uwekezaji nchini
3.6 Mafanikion ya Ongezeko la Miradi katika awamu ya sita yanatokana na yafuatayo:
i. Uboreshaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji umeendea kuonekana kwa ongezeka za uwekezaji katika uzalishaji bidhaa mbalimbali
ii. Biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani imeboreka na kuongeza mitaji katika sekta ya Usafirishaji.
iii. Uanzishwaji wa Kongani za viwanda umeleta mafanikio makubwa katika kuongeza uwekezaji katika sekta ya uzalishaji viwandani.
iv. Maboresho ya upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji,na mifumo ya malipo ya ardhi na hati za ardhi zimeendelea kuongeza uwekezaji katika sekta ya majengo ya biashara/ujenzi na makazi kama inavyoonekana katika Jedwali Na.2
v. Kuimarika kwa huduma kwa Wawekezaji na Ufanikishaji Uwekezaji Serikali imeendelea kufanya maboresho ili kurahisisha uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja na:
i. Kuimarisha Kituo cha Utoaji wa Huduma za Mahali Pamoja kilichoko TIC (One Stop Facilitation Centre). Taasisi 14 za Serikali kwa sasa zinatoa huduma katika Kituo cha mahali pamoja. Taasisi hizo ni Wizara ya Kazi, Wizara ya Ardhi, Uhamiaji, NIDA, NEMC, TRA, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Madini, BRELA, TBS, TMDA, OSHA, TANESCO na TIC yenyewe.
ii. Kuboresha mfumo wa kusajili miradi ya Uwekezaji yaani Tanzania Investment Window (TIW) ambayo inapatikana kwa mtandao (https://onestopshop.tic.go.tz). Hivyo, kwa sasa mwekezaji anaweza kusajili mradi wake TIC akiwa mahali popote duniani bila kufika TIC ndani ya siku moja hadi tatu iwapo mwekezaji amekamilisha nyaraka zote muhimu.
iii. Kuanzisha Mfumo wa Pamoja wa Huduma kwa Wawekezaji Tanzania unaojulikana kama Tanzania Electronic Investment Window (TeIW). Mfumo huu utaunganisha mifumo ya taasisi zote 12 ili mwekezaji aweze kupata huduma kupitia dirisha moja. Kwa sasa mwekezaji anatakiwa kupata huduma kwa kuingia kila mfumo. Hivyo, anatakiwa kufungua akaunti na kuwa na nywila (password) ya kila mfumo hali ambayo inaleta changamoto ya kutoa huduma, kupoteza muda mrefu kutafuta huduma kwenye tovuti mbalimbali. Mfumo wa TeIW unatengenezwa kwa awamu mbili: Awamu ya kwanza ambayo inahusisha taasisi sita (6): Wizara ya Kazi, , Uhamiaji, NIDA, TRA, BRELA, na TIC; imekamilika na mfumo umezinduliwa. Awamu ya pili ambayo itahusisha taasisi sita (6) zilizosalia: Wizara ya Ardhi, NEMC, TBS, TMDA, OSHA, na TANESCO uundwaji wake utanza hivi karibuni.
iv. Idara ya Kazi na Uhamiaji ilianza kutumia mfumo wa Online Work Permits Applications and Issuance System (OWAIS). Mfumo wa OWAIS umeunganishwa na Uhamiaji na mwekezaji anapata kibali kimoja tu chenye taarifa za kibali cha KAZI na kibali cha UKAAZI kinachoweza kutoka ndani ya siku moja (1) tu iwapo nyaraka zote zimewasilishwa.
4 Miradi Mahiri na Mahiri Maalum katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita ni kama ifuatavyo:
Miradi Mahiri na Mahiri Maalum
i. Miradi sita (6) Mahiri Maalum baada ya kukidhi vigezo vilivyoainishwa katika Sheria ya Uwekezaji, Sura 38 na kuidhinishwa na NISC ni Mradi wa Bagamoyo Sugar Ltd; Mradi wa Knauf Gypsum (T) Limited; Mradi wa Itracom Fertilizer Limited; Mradi wa Kagera Sugar Limited; Mradi wa Mtibwa Sugar Estate Limited; na Mradi wa Mihan Gas Ltd (Taifa Gas Tanzania Limited). Miradi hiyo inatarajiwa kuchangia katika uchumi wa nchi kwa kuchachua shughuli za uzalishaji mali na huduma, kuzalisha ajira, kuleta mitaji mipya, kuongeza mnyororo wa thamani, kupunguza urari wa malipo na biashara kwa baadhi ya bidhaa, kuliingizia Taifa fedha za kigeni na kuongeza mapato ya mtu mmoja mmoja, kampuni na nchi.
Kwa ujumla wake, miradi yote sita (6) inatarajiwa kuwekeza kiasi cha mtaji wa dola za Marekani bilioni 1.51 na kuzalisha ajira mpya takriban 204,150 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, kuzalisha tani 345,000 za sukari kwa mwaka na kuchangia kupunguza uhaba wa sukari nchini pamoja na kuokoa fedha ambazo zingetumika kuagiza sukari nje ya nchi, kuzalisha Tani 600,000 za mbolea zitakazowezesha wakulima kupata mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu.
ii. Mradi nane (8) iliyoidhinishwa na NISC ni Mradi wa Kongani ya Viwanda (Industrial Park) wa Kampuni ya Sino Tan Kibaha Industrial Park Limited;Mradi wa upanuzi wa kiwanda cha kuzalisha sukari wa Kampuni ya Kilombero Sugar Limited; Mradi wa kilimo cha miwa na kiwanda cha kuzalisha sukari wa Kampuni ya Mufindi Paper Mills Limited - Kasulu; Mradi wa upanuzi wa kiwanda cha uchakataji Mpunga wa Kampuni ya MW Rice Millers Limited; Mradi wa upanuzi wa kiwanda cha uzalishaji saruji wa Kampuni ya Lake Cement Limited; Mradi wa upanuzi wa miundombinu ya kusindika na kuhifadhi gasi wa Kampuni ya Oilcom (T) Limited; Mradi mpya wa kiwanda cha kuchakata mafuta ya kula kutokana na mbegu za mazao yanayozalishwa ndani wa Kampuni ya Wild Flower Grain & Oil Mills Company Limited; na Mradi mpya wa kiwanda cha kuzalisha Mabati wa Kampuni ya Lodhia Steel Industries Limited.
Miradi hii inatarajiwa kuwekeza kiasi cha mtaji wa dola za Marekani Bilioni 1.4 na kuzalisha ajira mpya takriban 62,719 za moja kwa moja na ajira zaidi ya 489,231 zisizo za moja kwa moja.
5 Kongani za Viwanda (Industrial Park)
Aidha, Serikali imeweka kipaumbele katika kuvutia miradi ya ujenzi wa kongani za Viwanda (Industrial Parks) ili kurahisisha na kuharakisha ujenzi wa viwanda lakini pia kukabiliana na changamoto ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji yenye miundombinu wezeshi. TIC imeweza kuratibu na kuvutia uanzishwaji wa miradi mikubwa ya uwekezaji yenye manufaa mapana kwa Taifa katika Kongani za Viwanda kama ifuatavyo;
i. Kongani ya Viwanda ya ‘’Sino-Tan Industrial Park’’ iliyopo Kwala mkoa wa Pwani yenye ukubwa wa hekari 2500
ii. Kongani ya Viwanda ya ‘’Modern Industrial Park ‘’ iliyopo Kibaha mkoa wa Pwani yenye ukubwa wa hekari 1000
iii. Kongani ya Viwanda ya ‘’Elsewedy Industrial City’’ iliyopo Kikongo mkoa wa Pwani yenye ukubwa wa hekari 600
iv. Kongani ya Viwanda ya ‘’Kamal Industrial Estate’’ iliyopo Bagamoyo mkoani wa Pwani yenye ukubwa wa hekari 279.
Ukamilishaji wa Miradi hii unapunguza gharama na muda kwa wawekezaji wanaotafuta maeneo ya kuweka viwanda na hivyo kuifanya nchi kuweza kuvutia wawekezaji wengi Zaidi katika sekta ya viwanda na kufanya bidhaa zinazo zalishwa katika kongani kuwa shidani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
6. UANZISHWAJI WA JIJI LA KILIMO MKULAZI
Hatua nyingine kubwa ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ni mafanikio ya Uanzishwaji wa Jiji la Kilimo la Mkulazi.,Mtakumbuka kwa kipindi kirefu Serikali imefanya juhudi kutafuta wawekezaji ambao wangeweza kuwekeza kwa kiwango ambacho kingeleta manufaa kwa nchi na wananchi wa maeneo ya Mkulazi ili kupunguza uagizaji kutoka nje ya nchi bidhaa za kilimo hususan Sukari, nafaka, sukari na mazao mbalimbali yatakayoingiza fedha za kigeni baada ya mauzo ya nje.
Hivyo basi , kupitia mchakato wa wazi, TIC kwa kushirikiana na Taasisi na Idara mbalimbali za Serikali ilifanya tathmini ya maombi ya Makampuni yaliyoonesha nia ya kuendeleza shamba la Mkulazi na Makampuni matatu yalijitokeza na kazi ya uendelezaji wa miradi inaendelea. Miradi hiyo inatarajia kuleta mitaji ya dola za kimarekani 575 milioni kuzalisha Ajira 10,000 za moja kwa moja.
7.Tanzania Kinara Duniani
TUZO za Kimataifa za Uhamasishaji Uwekezaji
i. Kituo kimeendelea kuhamasisha uwekezaji wa ndani na nje kwa kuanzisha kampeni mbalimbali za uhamasishaji uwekezaji na kuupa mwaka 2024 kama mwaka wa Uwekezaji.
Katika kipindi hicho Kituo kimefanikisha upatikanaji wa tuzo mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa TUZO za Kimataifa:
a. za AIM 2024 Mei Taasisi Bora ya Uhamasishaji Uwekezaji Kanda ya Afrika 2024.
b. Desemba 2024 World Association Investment Promotion Agency (WAIPA) kama Taasisi bora inayofanya vizuri katika kutumia mifumo kuhudumia wawekezaji katika nchi zinazoendelea duniani.
ii. Uwekezaji katika Miundombinu
Serikali kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu wezeshi kama barabara, reli, bandari, viwanja vya ndege na umeme na miundombinu ya Utalii.
iii. Diplomasia ya kiuchumi
Diplomasi ya Uchumi pia imekuwa kichocheo katika kufanya Tanzania kuwa eneo la kuvutia kwa uwekezaji katika Afrika.
Mafanikio yanayoonekana yaliyorekodiwa katika kuhamasisha diplomasia ya kiuchumi yatasaidia kukuza na kurahisisha wawekezaji wa ndani. Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika nchi mbalimbali imesaidia kuambia dunia kwamba Tanzania ni eneo bora la uwekezaji.
Katika kipindi kilichotajwa, Tanzania imepokea ujumbe wa uwekezaji kutoka nchi mbalimbali ikiwemo China, Saudi Arabia, Ufaransa, Ubelgiji, Ujerumani, Brazili, Afrika Kusini, Pakistani, Uholanzi, Namibia, Falme za Kiarabu, Nigeria, Misri, Poland, Uturuki, India, Oman, USA ETC
7. MATARAJIO YA KUENDELEA KUHAMASISHA UWEKEZAJI
Matarajio ya Kituo cha Uwekezaji kwa mwaka wa 2025, yaliyowekwa katika Mpango Mkakati wake uliozinduliwa hivi karibuni ni kuwa Kwanza, kituo kina lengo la kusajili miradi elfu moja mia tano (1500) ya uwekezaji, katika kipindi cha msimu wa 2025 na kuweka malengo ya kuvutia mitaji ya kigeni yenye thamani ya bilioni 15. Pia TIC imejipanga kuhakikisha kwamba, angalau asilimia kumi ya miradi iliyosajiliwa inalenga katika kuchangia juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuonyesha jitihada za kituo hicho za kusukuma mbele uwekezaji wenye manufaa na endelevu.
Mkurugenzi huyo akionyesha takwimu za wawekezaji nchini
Comments
Post a Comment