ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 3 KUKUSANYWA KATIKA MBIO ZA BUNGE MARATHONI JUMAMOSI WIKI HII JIJINI DODOMA.


Mwenyekiti wa Bunge Bonanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa bunge Marathoni pia ni Mbunge wa Makete Festo Sanga (katikati), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mbio hizo  ambazo zitafanyika jumamosi wiki hii jijini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa mbio hizo  Laysoni Mwanjis na Kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo  Pius Mboya.
Mwenyekiti huyo aliwaeleza waandishi wa habari kwamba mbio hizo ni wazo la Spika Dkt. Tulia Acksoni,  ambapo mbio hizo zinafanyika kwa mara ya kwanza kwa ajili ya  kuchangia ujenizi wa shule ya Bunge Boys Sekondari ambapo ya wasichana shule kama hiyo ilishajengwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Sanga alibainisha kwamba zoezi la usajili linaendelea vyema, wanariadha wengi wamejisajili kwa ajili ya mbio hizo, usajili ya sh elfu 40 tu, amewaomba wananchi na Wanadodoma wenye mapenzi mema na nchi hii wajitokeze kwa wingi kushiriki , bunge linawekeza elimu kwa watoto wa nchi hii.

Mbio hizo zitaongozwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Zitaanzia katika uwanja wa Jamhuri na kupita katika mitaa ya jiji hilo , mshindi wa kwanza kupata Sh milioni 5. 


Wanahabari wakimsikiliza Mwenyekiti huyo huku wakichukua habari






 

Comments

Popular posts from this blog

AMANI YETU TUILINDE NAIBU WAZIRI CHANDE AZUNGUMZA KATIKA IJITIMAI JIJINI DODOMA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.